Kuna wana JamiiForums wenzetu wanapitia nyakati ngumu mno

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Nilikuwa macho toka saa nane usiku na kuna mtu nikaongea naye kwa simu kama dakika kumi hivi. Kufika saa tisa hivi nikasikia kama kitu kinanyata nje ya nyumba. Nilidhani ni mbwa. Hivyo nikafunua pazia kidogo nikachungulia nje. Lahaulah grill la jikoni lilikuwa wazi. Lakini mlango ulikuwa umefungwa nikajua wa mwisho kuingia alipitiwa.

Dakika 20 hivi baadae dogo kanigongea mlango kuwa kuna mtu kafungua dirisha na alikuwa anamulika na tochi. Kuja kuchunguza nyumba yote. Jumla ya madirisha mane haya ya aluminum yalikuwa yamefunguliwa yote.

Kilichosaidia ni ma grill, TUMENUSURIKA KUIBIWA. Mungu ni mwema wakati wote.

Baada ya hapo nikaingia JF na kukutana na hii habari ya folk aliyesema atafariki baada ya miezi minne kutokana na kansa ya kongosho.


Ni kupitia uzi nikakumbuka masahibu mengi wanayopitia wa JF wengine muda huu lakini kamwe hawajayaandika hapa. Naomba nisimulie machache bila kuathiri privacy zao. Kwa njia hii tunaweza kuona magumu mazito wanayopitia wenzetu hawa. Na pengine hata wewe uyakayesoma hii mada kuna mazito magumu unapitia. Basi mada hii ikawe faraja, kupeana moyo, kupeana pole na ikiwezekana kupeana ufumbuzi. Unakaribishwa nawe kuweka kisa chako. Kwa kusimulia tu unaweza kupata faraja ya ajabu na huenda ikawa mwanzo wa kupata ufumbuzi.

Watu wamekamatwa katika magonjwa makubwa yasiyotibika. Watu wamefungwa kwenye vifungo na laana za ukoo. Watu hapa wamedhulumiwa mali, fedha, mahusiano, kazi nknk

Watu hapa wamegombanishwa na wenza wao, familia, koo, marafiki, kazi. Watu hapa wamefungwa kwenye uchawi na ushirikina na kufanyiwa mambo machafu mno.

Jamii Forums kwa weledi wake ina nafasi ya kuokoa roho nyingi na kuponya maumivu mengi.

Niandikapo mada hii kuna mwanaJF mwenzetu yuko kwenye maumivu makubwa kitandani akisubiri kukatwa mguu wake muda wowote wiki hii. Bado ni kijana lakini ndio hivyo tena. Anaenda kuwa mlemavu. Hujafa hujaumbika. Lakini ulemavu ni wa kimwili tu. Bado ana nafasi ya kusimama na kusonga mbele baada ya kupona. Tumuombee sana

Tuna wana JF wenzetu hapa kwao ajira imekuwa ni jinamizi linalotisha sana. Pamoja na kisomo kizuri na CV nzuri lakini kila walipopita wameishia kuahidiwa ahadi tasa. Wengine wanafamilia na wanategemewa na wazazi. Wanapitia kipindi kigumu mno. Wanahitaji faraja yetu.

Kuna wanaJF wenzetu hapa wanapitia kipindi kigumu mno kwenye ndoa na mahusiano yao. Inawezekana hata wewe ni mmojawapo.

Mume mlevi, malaya, mke si mwaminifu, wengine wameishia kutendwa na kudhulumiwa. Mmechuma wote mkaishi kwa dhiki lakini unakuja kugundua kumbe mwenza wako hakuwa na mapenzi ya kweli kwako.

Kuna wanaJF wenzetu hapa wanapitia kipindi kigumu mno cha mafarakano kwenye ukoo. Kuoneana wivu na kijicho. Kufanyiana fitina, kurogana, kudhulumiwa na mambo mengine mabaya sana.

Kuna wanaJF wenzetu hapa wamechafuliwa nyota zao na kujikuta hawana kinga za kiroho tena. Roho la kukataliwa limetamalaki kwao. Hakuna wanachoshika kikasimama. Mambo hayaendi na wanajikuta ni watu wa kuharibu na kuchukiwa bila sababu.

Kuna wanaJF wenzetu hapa wanaumwa lakini wakifika kwenye hospital za kizungu hakuna ugonjwa unaoonekana na katika harakati za kusaka tiba wanajikuta wanaangukia Kwa matapeli ambao wengine tunao humu na wanasoma hii mada.
Ni maumivu juu ya maumivu

Kuna wanaJF wenzetu hapa wanapitia kipindi kigumu mno cha madeni yasiyolipka mpaka wanaziogopa simu zao na nyumba zao. Wanaishi kama digidigi. Hawana amani hawana furaha

Kwakweli list ni ndefu na waliovurugiwa ramani za maisha si haba
Wapo wasaka mafanikio
Wapo wasaka ndoa
Wapo wasaka umaarufu
Wapo wasaka utajiri nk..

Wote hawa ni sehemu yetu ndani ya Jamii Forums. Natambua una magumu na changamoto unapitia. Lakini inawezekana lako lina nafuu kuliko la mwenzako. Sema neno la faraja sasa. JF ina impact kubwa sana. Ni kisemeo cha kuaminika cha jamii.

Neno lako moja linaweza kuwa tiba kubwa kwa wengi.

 
Simama kwenye kioo, zungumza na yule unayemuona mbele yako, Muambie 'kila kitu kinakwenda kuwa sawa, hili ni la muda tu, japo ni gumu ila nalo litapita, hakuna kitakachodumu milele,'..!

In whatever hard situation you're passing through learn to see positivity in it, Naamini Mungu hawezi kukupitisha kwenye jaribu litakalokushinda uwezo! Kama ameruhusu upite then you're strong enough to conquer it..!!

You're gonna make it sooner or later, Wewe ni dhahabu na dhahabu ili ing'ae ni lazima ipite kwenye moto.!!
Kamwe usiuogope moto 'DHAHABU'..!!
 
Waliopo JF ndio hao hao waliopo mtaani...

Vile mtaani hakuna sana fursa ya kujua habari za watu ndio maana pengine hatuoni tabu, dhiki, shida na maswaibu watu wanapitia...

Ukipata kuwa mtumishi katika sekta za afya, ustawi wa jamii, jeshi la polisi, elimu, taasisi za dini na kada zote zihusianazo na jamii, unaweza ukapata fursa ya kuona namna Watanzania wengi wanavyodumu...

Asilimia kubwa ya Watanzania hawaishi vile mwanadamu anapaswa kuishi, peeps are just struggling to exist (wanadumu)...

Lakini pamoja na hayo yote, life has to go on. Mwanadamu hajawahi kuacha kuwa na changamoto, luckly tumeumbwa na utashi mkubwa kuliko chochote chenye mwili...

Siku zote tumekuwa tukitafuta namna ya kupambana ili kuishi hata kama nature inataka otherwise...

Kama wewe umejaaliwa maisha mazuri ishi ukishukuru aliyekupa maisha mazuri, ukiweza wakumbuke wawili watatu upate swawabu...
 
Naamini kila kiumbe kinapitia magumu yake. Ubarikiwe tu Mshana Jr maana hii post imenitoa machozi. As I know what am passing through Ila sichoki na kila siku yangu inaanza na reminder kwenye simu yangu "All will be well, you will become successful".

Yote yanafanya maisha yawe hivi yalivyo. Kuna muda unapitia magumu miezi inakatika hakuna ulilofanikisha. Kwa haraka naweza sema kushindwa au kufeli Kuna effect kubwa Sana kwa binadamu Ila unayesoma hapa jua kwamba

"One day all will be well and everything will be in it's place".
Utafanikiwa utapata kile unachokitaka as long as bado tunapumua njia ipo na Mungu atafanya njia. Never Give up
 
Tumtwike Yesu taabu na fadhaa zetu na shida na magonjwa yetu, yeye atatupa raha, faraja, uponyaji na amani ya kweli.

Asubuhi njema.
IMG_20191113_060259.jpeg
 
Maisha yana majaribu mengi. Kuna wakati unatamani ufe ila kwa kuwa kufa kunakuwa siyo suluhu ya utatuzi wa mateso bali kutaongeza machungu, unamwachia Mungu aliyekuumba afanye njia pasipo na njia.

Lakini mwisho wa yote ikiwa ungali hai usikate tamaa haijalishi unaona muda umekutupa mkono kiasi gani unapitia machungu yasiyo elezeka NASEMA USIKATE TAMAA.

Mungu wetu ndiye ajuaye Baade yetu.
 
Back
Top Bottom