Elections 2010 Kuna walioshawishiwa na ujumbe wa kidini wakati wa kampeni?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
1,225
Inasikitisha sana kwamba kuna Waislam bendera-fuata-upepo waliopotoka, ambao walishawishiwa na ule ujumbe uliokuwa ukisambazwa kwamba Kikwete anapaswa kupigiwa kura na Waislam KWA KUWA ni Muislam, na kwamba Dk. Slaa asipigiwe kura kwa kuwa ni ADUI wa WAISLAM!

Hii nimeipata baada ya kukutana na binti mdogo, tena AISHIYE Ughaibuni (Dubai), aliyenitusi kwa kuniita mpumbavu na Mkristo nisiyejielewa, kila Jumapili niko kanisani "kumuimbia bwana" na kusali, sijielewi, ati!

Inashangaza, Ijumaa kabla ya uchaguzi mkuu nilienda (kutimiza wajibu) masjid, pale BAKWATA, Kinondoni, na Jakaya Kikwete - Muislam Mwenzetu - alikuwapo. Tulimwombea dua, kama Muislam Mwenzetu, na si kwa misingi ya chama chake. Tulimtakia kheri.

LAKINI SIKUMPIGIA KURA!

Waislam sasa wajifunze kutofautisha kati ya MAFUNDISHO ya KIDINI na SIASA. Vitu hivi viwili HAVICHANGANYIKI, ni kama MAJI na MAFUTA. Ukiweka mafuta ndani ya ndoo ya maji, yataelea juu, kwa kuwa hayana DENSITY ya kutosha.

Huyu mwenzetu KWELI KAPOTEA, na inashangaza, kama binti mdogo kama huyu amepotoka, je, waliomzidi umri?

Ukweli ni kwamba, asilimia 90 ya Waislam HAWAIJUI DINI, huku wakidhani wanaijua. Hii ni kwa mujibu wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliyetoa hotuba siku ya Ijumaa, tarehe 29 Oktoba 2010, akiwataka Waislam KUJIFUNZA DINI!

Huyu binti, licha ya kujifanya anaijua sana dini, alikiri kwamba HAKUISOMEA madrassat!

Inasikitisha, lakini, kwetu sisi tunaodai kwamba dini yetu ndiye ya HAKI na UKWELI, matendo yetu YANATUTOFAUTISHA na mafundisho ya Uislam, ambao maana yake halisi ni AMANI!

Amani kwako, amani kwetu wote!

Tukubaliane kutofautiana KISIASA, tuziweke dini zetu pembeni!

-> Mwana wa Haki

P.S. Sijui nilie au nicheke? Ati nimeritadi kwa kumchagua Slaa? Duh!
 
Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,742
2,000

Uchaguzi umekwisha,sasa ni tathmini, kila mtu na yake.
Wengine watakuja na mawazo yao ya kuchanganyikiwa,hawawezi hata kujieleza..Mmojawapo ni huyu mpenda haki.Ameona wapi kuwa kupotoka ni proportional na umri wa mtu!.
Aina ya mawazo kama haya kwa wanachadema walio wengi ndiyo yaliyowazindua waislamu, na si kwamba hawawezi kutofautisha kati ya MAFUNDISHO ya KIDINI na SIASA.Ukweli ni kuwa uislamu umetangulia siasa.
 
reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,202

Mkuu, nimeshindwa kuoanisha kati ya suala la kutompigia kura Dr. Slaa kwavile ni Mkristo na suala la huyo Binti wa Ughaibuni!!!! Mbona haioneshi kama yeye alikuwa anazungumzia masuala ya Siasa?!
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
mtenda haki

hii yako mbona kaa ina fit kwenye complains zaidi au?
 
Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
0
Wanadinisiasa ni wanasiasa wanaochanganya dini na siasa. Nimeunganisha maneno mawili na kupata wanadinisiasa.

Wapo watu wanataka watanzania tuamini kwamba uchaguzi huu ulifanyika kwa misingi ya dini jambo ambalo liko karibu na uongo na linaweza kuumba na huko mbele ikawa kweli.

Tukumbuke kwamba wagombea Urais wa vyama vyote na wafuasi wao ni mchanganyiko wa dini kuu mbili za wakristo na waislamu. Kwa mfano, mgombea wa CCM Jakaya Kikwete ambaye ni mwislamu ana wakristo ndani ya chama chake na serikali lakini wakristo wengi wameanguka nyuma yake ndani ya CCM, mathalan Lawrence Masha, Marmo, Mungai, Malecela, Kamala na kwa Wailsamu walioianguka ni Dr Batilda nk.,.kwa Historia nchi hii ina wakristo wengi katika ngazi za kisiasa kuliko waislamu kwa hiyo kumuangusha kikwete kwa misingi ya dini utakuwa unawaangusha wakristo wengi nyuma ya kikwete kama CCM kitakuwa chama cha upinzani. Hapa ukipiga kura ya udini wa kikiristo unamkomoa nani kama sio ujuha.

Kwa Upande wa Dr Slaa vivyo hivyo ni mkristo mwenye waislamu nyuma ya chadema na kama angeshinda kuunda serikali. Ukipiga kura ya Kupinga (Ya kiislamu) utakuwa unawakomoa pia waislamu walio ndani ya chadema. Kwa maana kwamba kushindwa kwa Dr Slaa ni kuanguka kwa mgombea mkristo sambamba na waislamu kwa pamoja. hapa kupiga kura ya udini wa kiislamu unawakomoa na waislamu nyuma ya Slaa.

Mimi naona mambo haya yalijitokeza kipindi cha uchaguzi kwa ajili ya kukidhi haja za ushindi wa wanasiasa wa siasa za maji taka na si mwananchi mmoja mmoja. Baada ya uchaguzi tutashuhudia kampeni hizo zikifa kifo cha asili.

Hata hivyo, hili ni fundisho kwamba, Watanzania tuwe macho wa wanadinisiasa wanatupeleka kusiko. Dini moja moja haina nafasi katika kujenga umoja wa taifa hili bali ni mchanganyiko wa dini zote.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
0
Nawapongeza watanzania wote waliokataa kupiga kura ya udini katika kipindi cha uchaguzi.
Hatuna wizara hata moja ya dini, hatuna waziri wa dini. Hivyo, sitegemei kwamba dini zetu ndizo zitatuletea maji, barabara, umeme nk. maaskofu na Masheikh hawatakwenda kupeleka miswaada ya kutuletea maendeleo bungeni watabaki makanisani na miskitini.
 
Mamushka

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
1,600
0
Mh huyo binti mdogo kakuumiza pole, usirudie kubishana na watoto wadogo sana wataka kuaibisha na kukukasirisha bure, wanachosema nikile wanachoskia mara nyingi hawachuji, mi nachojua udini Tanzania au ukabila hauna nafasi jamani, cha msingi nikile kilicho bora, 2005 Jk alishabikiwa sana na alichaguliwa japo upinzani haukua na moto sana kama sasa lakini alipendeka kwa kila mwananchi bila kujali mkristo au mwislam, alivoingia madarakani na kuboronga watu wakachoshwa na kuchukizwa na mambo yake, ndo maana wameamua kusimama kwa miguu yao. Hata Dr Slaa angepita then akaharibu wananchi wangemwaga vilevile kwani lazima.
 
Thesi

JF-Expert Member
Aug 8, 2010
998
1,195
Nakubaliana 100% na mwanahaki. Bora umekuwa mkweli. ukweli uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na udini na umewaathiri saana wagombea hasa Dr Slaa na CHADEMA. Hii kwangu kimenishtua sana kuona watu hawajali umoja na ushirikiano tulionao kama watanzania watu wanatumia udini kujihakikishia ushindi kwa vyama vyao. Chama cha mapinduzi kamwe hakiwezi kukwepa lawama hizi. Magazeti yanayoiunga mkono au magazeti yake yametumia sana propaganda hii. Magezeti kama Rai na Mtanzania ambayo yanamilikiwa na kada wa CCM akiwa ana tuhuma lukuki za ufisadi zilijikita kumchafua dokta mbele ya waislamu.
Jamani dini zina msukumo mkubwa na tofauti kwa watu. Hivi ikiwa mtu anaweza kujilipua kwa kudanganywa na kuaminishwa inashindikana nini kutomchagua mtua ukiambiwa ni adui wa Uislamu?
Kwangu namwamini Dr Slaa ila tu kwa mawazo yake ila ukweli imenipa taabu sana kumnadi kwa Waislamu wengi. Wapo wanaoelewa siasa ni mbali na dini katika na wanamjudge mtu kwa matendo yake na si dini yake. Nafikiri kama mwanahaki alivosema kuwa wengi wetu hatuelewi dini hivo mtu akitaka akutumie kisiasa anajua fitina ya dini ndio gia nyepesi.

Kwa kuwa viongozi wengi wa kidini hawakuridhishwa na mwenendo wa kupambana na maovu nchini walitaka mabadiliko hasa dini za kikristo na hiyo ikatoa mwanya kwa mafisadi waislamu(mafisadi wapo pande zote) kujificha nyuma ya Uislamu na kumpakazia Dokta Slaa.

Njia nzuri kupona majeraha na kurudisha umoja ulokuwepo ni kuwasafisha wale tuliowachafua makusudi. Kazi hii inaweza kufanywa vizuri na viongozi wa dini. Si kwamba waliwachafua watu lakini wanaweza kutibu majeraha.

Mi kwa ushauri magezeti ya kidini yote (yawe ya Kikristo au Uislamu) yangepigwa marufuku kuandika habari za siasa ila ni wazo langu. Kama Rwanda wamefanikiwa kutokubali kuandika habari za ukabila kwanini sisi tushindwe kupiga marufuku kwa magezeti ya kidini?
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Uchaguzi umekwisha,sasa ni tathmini, kila mtu na yake.
Wengine watakuja na mawazo yao ya kuchanganyikiwa,hawawezi hata kujieleza..Mmojawapo ni huyu mpenda haki.Ameona wapi kuwa kupotoka ni proportional na umri wa mtu!.
Aina ya mawazo kama haya kwa wanachadema walio wengi ndiyo yaliyowazindua waislamu, na si kwamba hawawezi kutofautisha kati ya MAFUNDISHO ya KIDINI na SIASA.Ukweli ni kuwa uislamu umetangulia siasa.
Mbegu mbaya huanza mwanzo, tatizo ni wale watakaosoma habari yake na KUKURUPUKA nayo badala ya KUTAFAKARI, KUIPIMA na KUMHAKIKI yeye mwenyewe je wakati anaandika alikwa wapi na anawaza nini... :smile-big:
hivi walianzaje na huyo binti mdogo? tena ughaibuni? je huyo binti anajuaje siasa za uchaguzi wakati kule hawafanyi uchaguzi? hapo pana maswali kuliko majibu. huenda akisahau akatuambia ukweli hapa kwamba ilikuwaje:tape:
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,093
2,000
Wanadinisiasa ni wanasiasa wanaochanganya dini na siasa. Nimeunganisha maneno mawili na kupata wanadinisiasa.

Wapo watu wanataka watanzania tuamini kwamba uchaguzi huu ulifanyika kwa misingi ya dini jambo ambalo liko karibu na uongo na linaweza kuumba na huko mbele ikawa kweli.

Tukumbuke kwamba wagombea Urais wa vyama vyote na wafuasi wao ni mchanganyiko wa dini kuu mbili za wakristo na waislamu. Kwa mfano, mgombea wa CCM Jakaya Kikwete ambaye ni mwislamu ana wakristo ndani ya chama chake na serikali lakini wakristo wengi wameanguka nyuma yake ndani ya CCM, mathalan Lawrence Masha, Marmo, Mungai, Malecela, Kamala na kwa Wailsamu walioianguka ni Dr Batilda nk.,.kwa Historia nchi hii ina wakristo wengi katika ngazi za kisiasa kuliko waislamu kwa hiyo kumuangusha kikwete kwa misingi ya dini utakuwa unawaangusha wakristo wengi nyuma ya kikwete kama CCM kitakuwa chama cha upinzani. Hapa ukipiga kura ya udini wa kikiristo unamkomoa nani kama sio ujuha.

Kwa Upande wa Dr Slaa vivyo hivyo ni mkristo mwenye waislamu nyuma ya chadema na kama angeshinda kuunda serikali. Ukipiga kura ya Kupinga (Ya kiislamu) utakuwa unawakomoa pia waislamu walio ndani ya chadema. Kwa maana kwamba kushindwa kwa Dr Slaa ni kuanguka kwa mgombea mkristo sambamba na waislamu kwa pamoja. hapa kupiga kura ya udini wa kiislamu unawakomoa na waislamu nyuma ya Slaa.

Mimi naona mambo haya yalijitokeza kipindi cha uchaguzi kwa ajili ya kukidhi haja za ushindi wa wanasiasa wa siasa za maji taka na si mwananchi mmoja mmoja. Baada ya uchaguzi tutashuhudia kampeni hizo zikifa kifo cha asili.

Hata hivyo, hili ni fundisho kwamba, Watanzania tuwe macho wa wanadinisiasa wanatupeleka kusiko. Dini moja moja haina nafasi katika kujenga umoja wa taifa hili bali ni mchanganyiko wa dini zote.

Mungu Ibariki Tanzania

Unayosema ni kweli. Nimekutana na Wakristo waliokuwa wakimpigia debe Kikwete na Lipumba na pia Waislamu waliokuwa wakimpigia debe Dr Slaa. Ila kuna waumini wasio na akili na ambao wakisikia tu maneno ya uwongo unaoenezwa na wanasiasa wanaamini kabisa kuwa ni kweli. Magazeti kama Al-Huda na Ar-Nuur yako kundi hili na yametumika vibaya kupandikiza udini.
 
Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,742
2,000
Nakubaliana 100% na mwanahaki. Bora umekuwa mkweli. ukweli uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na udini na umewaathiri saana wagombea hasa Dr Slaa na CHADEMA. Hii kwangu kimenishtua sana kuona watu hawajali umoja na ushirikiano tulionao kama watanzania watu wanatumia udini kujihakikishia ushindi kwa vyama vyao. Chama cha mapinduzi kamwe hakiwezi kukwepa lawama hizi. Magazeti yanayoiunga mkono au magazeti yake yametumia sana propaganda hii. Magezeti kama Rai na Mtanzania ambayo yanamilikiwa na kada wa CCM akiwa ana tuhuma lukuki za ufisadi zilijikita kumchafua dokta mbele ya waislamu.
Jamani dini zina msukumo mkubwa na tofauti kwa watu. Hivi ikiwa mtu anaweza kujilipua kwa kudanganywa na kuaminishwa inashindikana nini kutomchagua mtua ukiambiwa ni adui wa Uislamu?
Kwangu namwamini Dr Slaa ila tu kwa mawazo yake ila ukweli imenipa taabu sana kumnadi kwa Waislamu wengi. Wapo wanaoelewa siasa ni mbali na dini katika na wanamjudge mtu kwa matendo yake na si dini yake. Nafikiri kama mwanahaki alivosema kuwa wengi wetu hatuelewi dini hivo mtu akitaka akutumie kisiasa anajua fitina ya dini ndio gia nyepesi.

Kwa kuwa viongozi wengi wa kidini hawakuridhishwa na mwenendo wa kupambana na maovu nchini walitaka mabadiliko hasa dini za kikristo na hiyo ikatoa mwanya kwa mafisadi waislamu(mafisadi wapo pande zote) kujificha nyuma ya Uislamu na kumpakazia Dokta Slaa.

Njia nzuri kupona majeraha na kurudisha umoja ulokuwepo ni kuwasafisha wale tuliowachafua makusudi. Kazi hii inaweza kufanywa vizuri na viongozi wa dini. Si kwamba waliwachafua watu lakini wanaweza kutibu majeraha.

Mi kwa ushauri magezeti ya kidini yote (yawe ya Kikristo au Uislamu) yangepigwa marufuku kuandika habari za siasa ila ni wazo langu. Kama Rwanda wamefanikiwa kutokubali kuandika habari za ukabila kwanini sisi tushindwe kupiga marufuku kwa magezeti ya kidini?
Hapo juu umesema sana mpaka kipovu kimekutoka,hata hivyo bado ulichosema hakijawa na maana sana.
Mimi naamini siku serikali itakapochukua ushauri wako na kujiweka mbali na dini huo utakuwa ndio mwisho wake.Ujuwe maisha yanakwenda na kuwepo dini.Pasipokuwepo dini shetani ana nguvu sana.Mungu humuwacha shetani awatie adabu watu wasiopenda uongozi wake.Mwenyewe huwaongezea adhabu ya dunia watu hao mpaka wakatamani dunia ipasuke waingie kukwepa ladha mbaya ya dunia.
Kwa upande mwengine ukipenda kutafuta mchawi wa udini katika uchaguzi huu anza na kardinali Pengo.Wa mwisho alikuwa Kakobe aliyemchafua vibaya dkt.Slaa kwa waislamu.
 
mbogodume

Member
Oct 30, 2010
43
70
Hii nimeipata baada ya kukutana na binti mdogo, tena AISHIYE Ughaibuni (Dubai), aliyenitusi kwa kuniita mpumbavu na Mkristo nisiyejielewa, kila Jumapili niko kanisani "kumuimbia bwana" na kusali, sijielewi, ati!

huyo binti ana sababu zake za kusema hivyo, Lakini sio kwa upuuzi huu unaotaka kuuleta hapa ili upande mbegu za fitina kwa watanzania.

Inashangaza, Ijumaa kabla ya uchaguzi mkuu nilienda (kutimiza wajibu) masjid, pale BAKWATA, Kinondoni, na Jakaya Kikwete - Muislam Mwenzetu - alikuwapo. Tulimwombea dua, kama Muislam Mwenzetu, na si kwa misingi ya chama chake. Tulimtakia kheri.

Mungu ndio anajua juu ya imani yako...hauhitaji kujitetea.

LAKINI SIKUMPIGIA KURA!

.

Huyu mwenzetu KWELI KAPOTEA, na inashangaza, kama binti mdogo kama huyu amepotoka, je, waliomzidi umri?
inaonesha jinsi gani ulivyo kilaza!

Ukweli ni kwamba, asilimia 90 ya Waislam HAWAIJUI DINI, huku wakidhani wanaijua.

Hiyo research ilifanywa na nani? usilete maneno ya kibarazani na kumzushia uongo shekhe wa watu.
Think positively
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,515
2,000
Unayosema ni kweli. Nimekutana na Wakristo waliokuwa wakimpigia debe Kikwete na Lipumba na pia Waislamu waliokuwa wakimpigia debe Dr Slaa. Ila kuna waumini wasio na akili na ambao wakisikia tu maneno ya uwongo unaoenezwa na wanasiasa wanaamini kabisa kuwa ni kweli. Magazeti kama Al-Huda na Ar-Nuur yako kundi hili na yametumika vibaya kupandikiza udini.
uSISAHAU Lile la msemakweli na...
 
Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,395
1,500
Uchaguzi umekwisha,sasa ni tathmini, kila mtu na yake.
Wengine watakuja na mawazo yao ya kuchanganyikiwa,hawawezi hata kujieleza..Mmojawapo ni huyu mpenda haki.Ameona wapi kuwa kupotoka ni proportional na umri wa mtu!.
Aina ya mawazo kama haya kwa wanachadema walio wengi ndiyo yaliyowazindua waislamu, na si kwamba hawawezi kutofautisha kati ya MAFUNDISHO ya KIDINI na SIASA.Ukweli ni kuwa uislamu umetangulia siasa.
waislamu hapa!!http://www.youtube.com/watch?v=t1IRwgr9dEE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom