Kuna wale washkaji zetu na ndugu zetu tukiwa broke wanatuchukulia maandazi. Tuishi nao kwa akili

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,929
7,268
Wakuuu baada ya kuona uzi wa mwenzetu mmoja unaogusia baadhi ya watu ndugu, jamaa na marafiki wakisha pata nafuu kutzidi wengine wanavyo jibu au kuleta madharau kwa kina sie ambao bado tuna suffer na jua la mtaa(kuzisaka). Nimeona nije na mimi na mawazo yangu kuhusu watu wa namna hiyo.

Mambo ya kufanya kwa wale ambao bado tuna suffer na hali ngumu ya maisha ili tuweze kuishi na hawa watu wetu wenye madharau.
1. Tuishi tukijua mafanikio yetu yapo katika juhudi zetu, uvumilivu, kujituma na kuamini katika tukifanyacho.

2. Madharau yasitukatishe tamaa. Yatustue. Ila mchizi au ndugu mwenye madharau tumkatae au kumpunguza kdgo ikiwa hana matokeo chanya katika juhudi zetu.

3. Ni kweli kufanikiwa ni process tena inayohitaji hata kushikwa mkono ila sio kila wakati tutegemee kukubalika. Profesa jay moja ya mstari katika nyimbo yake ya hapo vipi hapo sawa alisema "ili ufanikiwe unahitaji marafiki, ili ufanikiwe zaidi unahitaji maadui".

4. Sio kwa sababu hauna hela ukaamini kuwa mwenye nazo anakuzidi akili, HAPANA. wapo matajiri kibao tu akili hawana.

5.kufanikiwa ni bahati pia, kurithi, elimu, kipaji nk.

Washikaji.wenye dharau tuwatumie na tuwapunguzeje.

1. Kama kuna idea muulize fresh tu akikupa mwongozo uchukue jiongoze mengine. Aki kaza fresh its party of the game.

2. Akidharau unachokifanya mpunguze kwenye ushirikishaji na maamuzi ya mambo yako. ( self defense )

3. Akikushika mkono jishushe kwa muda jichange tujaze kibaba.

4. Madharau yasitupe depression zaidi.

Mwisho hela itafutwe ni jawabu la mambo mengi asee.
 
Yaan uwe tajiri alafu hauna akili? Ebu kuwa serious mkuu

Then unapata wapi muda wa kujadili dharau za mtu? Mara nyingi mnachoita dharau ni kujishtukia tu, mtu yupo busy na mambo yake et ana dharau, ishi maisha yako utaona hao unaodhani wanakudharau.

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
 
Kuwa tajiri hakumaanishi.kuwa unawazidi IQ walikosa pesa ipo Mifano Mwl Nyerere alikua genius ila hukua tajiri km kina bakresa au kina metl nk. Kuwa na akili ni kuwa na maarifa sawa mkuu kufanikiwa au kuwa tajiri kuna mambo mengi saana hela za kurithi, kuiba, bahati, kipaji na njia nyingi tu za haramu mpaka kutoa kafara za kichawi. Tambua hilo
 
Tukiwa wote matajiri watakosekana watu wa kulalamika humu jukwaani.
End of the day ni kweli money buys happiness, tutasema yooote lakini ukweli tu ni kwamba umaskini unaumiza
 
Tukiwa wote matajiri watakosekana watu wa kulalamika humu jukwaani.
End of the day ni kweli money buys happiness, tutasema yooote lakini ukweli tu ni kwamba umaskini unaumiza
Pesa ni jawabu la mambo mengi. Itafutwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom