Kuna wale ambao deni la Mwezi Juni kwenye salary slip limekuja kama lilivyo kwenye Salary slip ya Mwezi Mei 20121

Farm boy

Member
Sep 8, 2015
60
104
TAHADHARI KWENU NDUGU ZANGUNI MNAOKATWA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWENYE MISHAHARA YENU
KUNA SUALA INAWEZEKANA HAMJALIGUNDUA KAMA HAMJACHUNGUZA KWENYE SALARY SLIPS ZENU ZA MWEZI MAY NA MWEZI JUNI 2021

Kuna wale ambao deni la Mwezi Juni kwenye salary slip limekuja kama lilivyo kwenye Salary slip ya Mwezi Mei 20121 yaani deni halijapungua ukilinganisha na mshahara uliopita, na kuna wengine ambao deni lao limeji-double yaani kama Mwezi mei ilionekana unadaiwa Mil 2 basi Mwezi Juni waweza kuta unadaiwa Mil 4, pia kuna wengine ambao Salary slip zao zinaonesha labda Mwezi Mei amekatwa Laki na 41 elfu lakini ukichukua deni la Mwezi Mei ukatoa Deni la Mwezi Juni utapata makato ni kama elfu 31 kitu ambacho sio kweli Kimahesabu
Binafsi sijafanya mawasiliano na HESLB Kujua shida ni nini, ila nimeona niwastue ndugu zangu ili kila mtu achunguze salary slip yake ili kama na wewe yamekukuta kama mimi basi uchukue hatua as soon as possible_. Inawezekana hii hali imetokea siku nyingi ila kwa sababu hatudadisi vizuri kwenye hati zetu za mishahara tunajikuta tunalipa kila mwezi mpaka miaka 10 lakini bado deni haliishi

NAWATAKIA UDADISI MWEMA

CC: HESLB Kwa taarifa
CC: BENKI KUU KWA UFUATILIAJI.
Nisamehewe kama Sikutafsiri vizuri nilichokiona kwangu na kwa Wenzangu
 
Back
Top Bottom