Kuna wakati unajisahau na kukimbilia kulaumu na kubeza bila tafakuri

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,773
730,049
Hii si dhambi kufanya hivyo ni ile hali tu ya kuzidiwa na mambo na kuchukuliwa kwenye ngoma yenye mirindimo mingi na kwa vile tuko ndani ya mduara hatuna budi kwenda na midundo ya mpigaji
Kwenye utaratibu mzima wa maisha yetu haya na mishemishe hukumbana na masahibu mengi, mojawapo ya masahibu hayo ni Kama ajali magonjwa na shida nyingine ambazo huwa kubwa kiasi cha kuleta madhara kwenye mwili na ufahamu kwa ujumla
Sehemu ambazo ni sensitive sana kwenye mwili ambazo zikipata shida uwezo wa mtu kufikiri na kutoa maamuzi hupungua ama kupata mushkeli ni kichwa na uti wa mgongo hivyo viwili ndio vinatengena software na chords za ufahamu
Ni wazi hatukosi mifano kadha ya ndugu rafiki hata jamaa zetu ambao walishakutana na madhila makubwa kiasi cha kuathiri uwezo wao wa kufanya maamuzi au hata kupambanua mambo
Watu wa Jinsi hii hawapaswi asilani kupewa majukumu yenye kuumiza kichwa na kutoa maamuzi kwa wengi.... Hawatakiwi Kuwa kwenye nafasi zozote za uongozi hata za ubalozi wa nyumba kumi kwakuwa wataharibu na badala ya kuangalia tatizo limeanzia wapi tutakimbilia kulaumu kubeza kukebehi make hata kukasirishwa na hayo yatokanayo
Daima tuangalie chanzo cha tatizo... Mwisho wa siku utajikuta tatizo limeanzia kwetu wenyewe kwa kuchukua maamuzi ya hovyo na kumpa fulani dhamama ya jambo fulani kubwa huku tukiwa na historia yake kamili ....kwamba Mshana anatufaa sana kwenye mambo ya ulozi lakini kamwe si dereva mzuri
Mkimchagua Mshana huyu mlozi halafu mumpe gari kubwa lililosheheni bidhaa na watu, Kama atakuwa kiburi na kujifanya mjuaji bila kukubali mashauri atawaletea tingo mbovu konda mwendokasi, atawapitisha barabara mbovu ataendesha hovyo hatazingatia taratibu sheria na Kanuni
Likitokea lakutokea kosa si la konda wala utingo... Tusiwalaumu hawa kuna chanzo kuna asili kuna mzizi.... Twendeni huko
 
bashite yuko na hayo magonjwa basi mkuu sitamlaumu tena maana sie yeye ni ugonjwa tu ule
1200px-Blausen_0114_BrainstemAnatomy.png

Hiyo brainstem ndio chord moja muhimu sana... Ikiwa disturbed kidogo tu utasikia fulani ana file muhimbili... Na ukishaambiwa hivyo jiongeze
 
Back
Top Bottom