Kuna wakati huwa najihisi kama niko tofauti na kila mtu

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Apr 16, 2020
460
1,337
Habarini za uzima. Mimi sijambo pia. Kama afya yako haiko katika utimilifu basi Mwenyezi Mungu akujaalie nafuu ya mapema ujisikie kupona.

Moja kwa moja kwenye mada.
Baada ya maisha yangu kuchukua sura mpya kwa Mwaka mmoja sasa, jana nimepata nafasi ya kujitathmini kujua iwapo niko sawasawa na jamii inayoishi kawaida.
Kwa uchache tu ni kuwa kutokana na changamoto za maisha zilizonikumba kuanzia wakati nikiwa mdogo sana, kuna Mambo hata mimi nilikuwa sijifahamu. Kuna baadhi ya matendo niliyokuwa nikiyafanya zamani nikijiaminisha kuwa hali ya kukosa mahitaji na kuishi mazingira hatarishi ndiyo iliyochangia kufanya baadhi ya maamuzi.

Kwa mfano, ilifika wakati fulani nikiwa mtaani, nikishikwa na njaa na sina ramani kabisa ya kupata chochote au popote pa kwenda kula nilikuwa nakaa chini naandaa mpango wa kwenda kuiba. Mimi na wenzangu (wa mtaani). Sasa ilifika wakati nikatoka katika hali ya kuwa mtoto wa mtaani. Nikapata bahati ya kwenda kusoma shule. nikiwa shule sikuwahi kuiba, ila nilikuwa mtu mwenye hofu na kujishtukia siku zote. Kila muda nilijiuliza rohoni iwapo wizi ni tabia yangu au ilitokea tu kutokana na kukosa chakula. Hali ya uchangamfu na kuongea na watu iliniondoka mara moja kila wakati mawazo hayo yalipokuja.

Ule ukimya na kutozungumza na watu mara nyingi, ukizingatia pia nilikuwa na akili darasani basi nikapata sifa ya mtoto mwenye busara, mkimya, mtulivu, kipanga na mengine mazuri. Wakati wote sifa zote hizo hazikuwahi kunifanya nijisamehe hatia ile ya kuwahi kujihusisha na wizi (Japo wizi ulikuwa ni small scale 😁😁) Kwa mimi nilivyo, najijua kabisa sio mkimya, ila nikiamua, nakua mkimya na nakuwa mkimya kabisa tena sio ukimya wala ustaarabu wa kuigiza, nakuwa kweli mstaarabu. Ila nikiingia mazingira ambayo yatanitaka niongee, nizungumze sana basi utanishangaa... maneno yatanitoka kama vile nimezaliwa pwani. naongea kwelikweli.

Basi watu ambao niko nao karibu nadhani wanashindwa kunielewa kwa kuwa mimi attitude zangu ni periodically. Wasionizoea huwa wananilaumu baadhi ya wakati kuwa nawanyamazia, lakini sio, tatizo sijajua mimi ni wa aina gani. mcheshi au mkimya. Sijui
Akili yangu huwa inazunguka kwa spidi sana nikiwa kwenye hali ya utulivu ila kama nikiwa na watu, huwa inabidi nikae nao kulingana na wanavoamini uwa pace ya akili na maamuzi ya mtu wa aina yangu inapaswa kuwa.
Sasa kuna wakati tena najishtukia kuwa hivi naigiza maisha au naishi maisha yangu? Kama ni maisha yangu, mimi ni mtu wa aina gani? mkorofi au mstaarabu, maana yote najua nayaweza.
Hili jambo linanikosesha sana kujiamini.
Yaani najijua kabisa sina tamaa wala nia ya kuiba chochote ila mtu anapozungumzia wizi yaani mimi huwa sina amani. Natafunwa sana na hatia fulani rohoni.

Mbaya zaidi sasa, mtu akinituhumu, au akihisi pengine naweza kumuibia au kudokoa kitu. Yaani hapo siwezi kujisamehe nafsi yangu. nitatengeneza theory nyingi sana nikivaa viatu vya wanaonitazama nijue wananionaje, nikizungumza, navoishi, navotembea. Basi ilimradi tu, sina amani. Nilishawahi kupata kazi sehemu... nilifanya kazi kwa mapenzi yote, kwa kuipenda na kujituma, hata ikanibidi kufanya muda wa ziada. Ila mawazo ya kuiacha kazi husika yalianza siku ambapo ofisi fulani ilitokea uharibifu na mtu akawa ame-misplace kitu. Mimi nikawa mmoja kati ya waliohojiwa - For good. Nakumbuka nilikuwa nikikaa peke yangu nalia mno. Mimi huwa nalia sana mara nyingi usiku nikilala. Basi nilikaa kwa maumivu hayo, kwa hatia ya jambo nisilofanya, nina tatizo la madonda ya tumbo.... yakazidi nikawa hata kuamka asubuhi kwenda kazini ni tabu.
Ile hatia ilipelekea niiache kazi yenyewe nikaishi maisha mengine.

Sijui wengine huwa wakoje ila mimi binafsi, sijawahi kuhua ni wa namna gani. Niliwahi kuambiwa na mtu "wewe mtoto mdogo sana you are very sensitive" nadhani alikuwa sahihi.
Hivi nyie wengine huwa mnawezaje kuishi maisha mengine ya kawaida bila kufuatwa na majinamizi ya maisha mliyoishi zamani?
Nawasilisha
 
Hii kitu hata kwangu nilikua nayo japo sio sana.
Ni tatizo kweli.
Lakini mimi nilianza kujifunza habari za Mungu kwa nguvu zote, kwa kusoma na kuandika.
Tangu nianze mkakati huo ...
Hiyo shida iliisha yote.

Maisha ya ukristo raha sana.
 
Hapa kipengele cha masuala ya Imanindio unaniacha mbali kabisa
 
Hivi nyie wengine huwa mnawezaje kuishi maisha mengine ya kawaida bila kufuatwa na majinamizi ya maisha mliyoishi zamani?
Nawasilisha
Kukubali past yako>Kujisamehe>kubadilika.

Umeandika haujui wewe ni wa aina gani. You are a good person. The fact that you look back at your past and be embarrassed means you are not the same person anymore.

Jitahidi kukubali past yako na kujisamehe kwa kila kitu kilichotokea. Kila ulichofanya kimeshafanyika hamna vile unaweza ku-change. The past is not accessible anymore ila unachoweza kufanya ni kuhakikisha uliyoyafanya hauyafanyi yena.

Hope you will feel better.
 
Nahisi
JamiiForums352667386.jpg
 
Asante. Ila ni process, nimekuwa nikijaribu ku move on ia mis step kidogo tu huwa inanirejesha mwanzo tena. kwa mfano. pale ambapo mtu ananifahamu japo kidogo, kisha aoneshe hata kidogo kutokuwa na imani na mimi. Bas mimi hjiskia mkosefu sana hata kama sijamkosea mtu. Ndio maana huwa nashindwa kabisa kuwa na marafiki. Huwa na socialize sometime, ila amini kwamba mimi sina rafiki hata mmoja wa kusema ni kampani yangu.
 
Wala haisumbui kabisa niko na mambo yangu tu ukitaka kunigandaganda unachoka mwenyewe unaniacha kama nilivyo

Nilichojifunza kwako, umeshajikubai namna ulivyo, hauhangaiki tena kujibadilisha ili uendane u-fit demo. mimi nashindwa hiyo
 
Asome kitabu cha the subtle art of not giving a https://jamii.app/JFUserGuide kitamsaidia sana naamini kila mtu na sad story kwaiyo sio wewe tu
watu wengine tumejaribu kukubaliana nayo tunaishi maisha furaha kabisa kwa kuangalia future
 
Habarini za uzima. Mimi sijambo pia. Kama afya yako haiko katika utimilifu basi Mwenyezi Mungu akujaalie nafuu ya mapema ujisikie kupona.

Moja kwa moja kwenye mada.
Baada ya maisha yangu kuchukua sura mpya kwa Mwaka mmoja sasa, jana nimepata nafasi ya kujitathmini kujua iwapo niko sawasawa na jamii inayoishi kawaida.
Kwa uchache tu ni kuwa kutokana na changamoto za maisha zilizonikumba kuanzia wakati nikiwa mdogo sana, kuna Mambo hata mimi nilikuwa sijifahamu. Kuna baadhi ya matendo niliyokuwa nikiyafanya zamani nikijiaminisha kuwa hali ya kukosa mahitaji na kuishi mazingira hatarishi ndiyo iliyochangia kufanya baadhi ya maamuzi.

Kwa mfano, ilifika wakati fulani nikiwa mtaani, nikishikwa na njaa na sina ramani kabisa ya kupata chochote au popote pa kwenda kula nilikuwa nakaa chini naandaa mpango wa kwenda kuiba. Mimi na wenzangu (wa mtaani). Sasa ilifika wakati nikatoka katika hali ya kuwa mtoto wa mtaani. Nikapata bahati ya kwenda kusoma shule. nikiwa shule sikuwahi kuiba, ila nilikuwa mtu mwenye hofu na kujishtukia siku zote. Kila muda nilijiuliza rohoni iwapo wizi ni tabia yangu au ilitokea tu kutokana na kukosa chakula. Hali ya uchangamfu na kuongea na watu iliniondoka mara moja kila wakati mawazo hayo yalipokuja.

Ule ukimya na kutozungumza na watu mara nyingi, ukizingatia pia nilikuwa na akili darasani basi nikapata sifa ya mtoto mwenye busara, mkimya, mtulivu, kipanga na mengine mazuri. Wakati wote sifa zote hizo hazikuwahi kunifanya nijisamehe hatia ile ya kuwahi kujihusisha na wizi (Japo wizi ulikuwa ni small scale ) Kwa mimi nilivyo, najijua kabisa sio mkimya, ila nikiamua, nakua mkimya na nakuwa mkimya kabisa tena sio ukimya wala ustaarabu wa kuigiza, nakuwa kweli mstaarabu. Ila nikiingia mazingira ambayo yatanitaka niongee, nizungumze sana basi utanishangaa... maneno yatanitoka kama vile nimezaliwa pwani. naongea kwelikweli.

Basi watu ambao niko nao karibu nadhani wanashindwa kunielewa kwa kuwa mimi attitude zangu ni periodically. Wasionizoea huwa wananilaumu baadhi ya wakati kuwa nawanyamazia, lakini sio, tatizo sijajua mimi ni wa aina gani. mcheshi au mkimya. Sijui
Akili yangu huwa inazunguka kwa spidi sana nikiwa kwenye hali ya utulivu ila kama nikiwa na watu, huwa inabidi nikae nao kulingana na wanavoamini uwa pace ya akili na maamuzi ya mtu wa aina yangu inapaswa kuwa.
Sasa kuna wakati tena najishtukia kuwa hivi naigiza maisha au naishi maisha yangu? Kama ni maisha yangu, mimi ni mtu wa aina gani? mkorofi au mstaarabu, maana yote najua nayaweza.
Hili jambo linanikosesha sana kujiamini.
Yaani najijua kabisa sina tamaa wala nia ya kuiba chochote ila mtu anapozungumzia wizi yaani mimi huwa sina amani. Natafunwa sana na hatia fulani rohoni.

Mbaya zaidi sasa, mtu akinituhumu, au akihisi pengine naweza kumuibia au kudokoa kitu. Yaani hapo siwezi kujisamehe nafsi yangu. nitatengeneza theory nyingi sana nikivaa viatu vya wanaonitazama nijue wananionaje, nikizungumza, navoishi, navotembea. Basi ilimradi tu, sina amani. Nilishawahi kupata kazi sehemu... nilifanya kazi kwa mapenzi yote, kwa kuipenda na kujituma, hata ikanibidi kufanya muda wa ziada. Ila mawazo ya kuiacha kazi husika yalianza siku ambapo ofisi fulani ilitokea uharibifu na mtu akawa ame-misplace kitu. Mimi nikawa mmoja kati ya waliohojiwa - For good. Nakumbuka nilikuwa nikikaa peke yangu nalia mno. Mimi huwa nalia sana mara nyingi usiku nikilala. Basi nilikaa kwa maumivu hayo, kwa hatia ya jambo nisilofanya, nina tatizo la madonda ya tumbo.... yakazidi nikawa hata kuamka asubuhi kwenda kazini ni tabu.
Ile hatia ilipelekea niiache kazi yenyewe nikaishi maisha mengine.

Sijui wengine huwa wakoje ila mimi binafsi, sijawahi kuhua ni wa namna gani. Niliwahi kuambiwa na mtu "wewe mtoto mdogo sana you are very sensitive" nadhani alikuwa sahihi.
Hivi nyie wengine huwa mnawezaje kuishi maisha mengine ya kawaida bila kufuatwa na majinamizi ya maisha mliyoishi zamani?
Nawasilisha
Sio kwako tu, mimi pia natafunwa na maumivu ya mambo yaliyopita, ukichanganya na depression basi mambo yamekuwa mabaya vidonda vya tumbo , mkono wa kushoto unakuwa na ganzi na maumivu, najitenga sana na watu, nakaa mpweke mpweke
 
Nina shida sana ya psychologist / daktari wa Afya ya akili maana nitakufa kwa hali hii
 
Asante. Ila ni process, nimekuwa nikijaribu ku move on ia mis step kidogo tu huwa inanirejesha mwanzo tena. kwa mfano. pale ambapo mtu ananifahamu japo kidogo, kisha aoneshe hata kidogo kutokuwa na imani na mimi. Bas mimi hjiskia mkosefu sana hata kama sijamkosea mtu. Ndio maana huwa nashindwa kabisa kuwa na marafiki. Huwa na socialize sometime, ila amini kwamba mimi sina rafiki hata mmoja wa kusema ni kampani yangu.
I think you are being paranoid. Hamna mtu anakuwazia vibaya bali your brain is playing tricks on you. Always assume positive intent until proven otherwise.

Unapenda kusoma? Mark Manson ana kitabu kinaitwa "The Subtle Art of Not Giving a Fvck" kitakusaidia lakini pia kama unaweza kufanya Meditation itakusaidia pia kuondoka na hiyo Social anxiety disorder.

Look, life is too short to be weighed down by this stuff.
 
Back
Top Bottom