Zamaulid
JF-Expert Member
- May 25, 2009
- 18,654
- 13,475
Ilikuwa 90's nilizama chumbani kwa binti nipige mzigo,huyo binti tulikuwa tunasoma naye secondary. Basi bana zile wanazosema za mwizi arobaini ndo zilikuwa zimetimia. Kabla sijaanza kupiga mzigo nikawa nimepewa chakula nakula!mara paaa baba wa binti akapiga hodi anataka kuja kuchukua kitu kule ndani kwa binti,tulichenganyikiwa kwa muda...nikaingia uvunguni nikatulia tuli!dingi kaingia kafanya yake wakati anatoka akashitukia kuna chakula mezani ambacho kinaonekana kilikuwa kinaliwa!mshua akamuuliza nani yupo humu? binti kimya...akatishiwa kupigwa kibao...akafunguka kila kitu hadi siku hiyo ilikuwa ya ngapi kuingia chumbani...niliishiwa nguvu...mzee akaniamru nitoke uvunguni, kwanza nikajifanya sisikii akarudia mara ya pili tatu...ikabidi nisalende..."natoka...nilikuja kuazima daftari"kilifuatia kipigo heavy cha mkanda wa jeshi...nilipopata upenyo nilitimua mbio nikiacha shati na viatu...tukio hili nikilikumbuka huwa naona akili ilifanya kazi baada ya kutenda!we uliwahi kutenda lipi ambalo unadhani hukuwa umeishirikisha akili ipasavyo
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app