Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Unakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa katikati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda.
Mezani mpo nane. Wewe ni mtu wa tatu kujiwekea chakula, utamsikia shemeji leo umenipatia kweli, hawa samaki ndiyo ugonjwa wangu. Anachukua vipande vitatu pasi kufikiria watano wanaomsubiri watapata samaki.
Ustaarabu ni kuchukua chakula kidogo, subiri round ya kwanza iishe. Kama ulipenda sana samaki unaweza kujiongezea katika round ya pili kama watakuwa wamebaki. Wakati huo ndiyo unaweza kusema kama hakuna anaeongeza ninatongeza hawa samaki maana hiki ndiyo chakula ninachokipenda, leo shemeji umenipatia.
Kuna wengine anakula huku anashika smart phone yake mezani anaangalia messages. Jamani hao wanaokutumia hawawezi kusubiri mpaka umalize kula na wenzako? Kama una ujumbe wa muhimu sana deal la mahela unaweza kuwataarifu wenyeji wako kuwa kuna ujumbe ninautegemea lakini ni ustaarabu kuachana na simu wakati mko mezani.