Kuna vyama vingine ni vibanda vya Tigopesa kwa viongozi

nashicha

JF-Expert Member
May 29, 2021
279
517
Tuwe wakweli katika kupambania kushika Dola Kuna vyama ambavyo Wala haviwazi malengo hayo au hata kubadili mwelekeo wa hii nchi viongozi wake wapo pale kuvitumia kama kule Kenya wanaita VIOSK vya Tigopesa au mpesa kujipatia pesa na umaarufu wakuitwa Wenyeviti na kama Kuna kongamano au mwaliko utawaona hao viongozi bila hata wanachama na havijulikani malengo yake.

Kwa Mfano CHAUMA DP ACT TLP na hata CUF lipumba alikigeuza hiki chama kuwa CHAKA LAKE la kupiga pesa na kufanya njia rahisi kuonana na Viongozi wa serikali kwa kivuli ni viongozi wa vyama Hawana nia thabiti ya kufanya hii nchi itoke ilipo au kuipush CCM ifanye vizuri zaidi.

Sisi kama WANANCHI tunatakiwa kuamka Sasa kuviunga mkono vyama makini kwaajili ya ustawi wa TAIFA letu maana hata kama chama kilichopo madarakani kinafanya vizuri vyama vya upinzani Huwa vinakitisha ili kifanye vizuri zaidi na zaidi tujitahidi kukubali kushirikiana ili chama chochote kilichopo madarakani kila kinapotazama nyuma kiona Kuna chama kinataka kukipokonya madaraka ndio maendeleo yatakuja kwa kasi
 
Hapajawahi tokea mpinzani wa kweli kumzidi Lipumba. Unaowaona wapinzani waliuza kiti cha kugombea urais kwa bilioni 12
 
Hapajawahi tokea mpinzani wa kweli kumzidi lipumba...unaowaona wapinzani waliuza kiti Cha kugombea urais kwa bilioni 12
Leta ushahidi maana lipumba bila kificho amekuwa Chawa wa CCM hasa akimpoozesha MAREHEMU Maalim Seif kila alipokuwa anataka kupigania Haki na yule alipandikizwa CUF kama Mrema na Zitto kabwe na Shibuda ndio amekuja mwishoni kuwa M/kiti TCD akawa Chawa kabisaa
 
Lipumba huyu huyu profwa uchumi..aliyeua chama cuf kwa vipande vya fedha.

Vyama vingi hapa nchini ni matawi ya kijani..hakuna wapinzani wa kweli kwambali labda chadomo..nao hawaaminiki sana sikuhizi baada ya mwenyekiti wao kulambishwa asali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mpemba na mchaga walikula hela za mamvi...lipumba na slaa wakaona ujinga,Ila propaganda zikageuza Mambo,wakweli wakaonekana waongo na waongo wakweli
 
Leta ushahidi maana lipumba bila kificho amekuwa Chawa wa CCM hasa akimpoozesha MAREHEMU Maalim Seif kila alipokuwa anataka kupigania Haki na yule alipandikizwa CUF kama Mrema na Zitto kabwe na Shibuda ndio amekuja mwishoni kuwa M/kiti TCD akawa Chawa kabisaa
Seif aliiuza cuf kwa mamvi wakati mangi aliuza saccos yake,seif alikua Waziri mkuu kiongozi zenji,alimuuza jumbe kwa nyerere kwa kuuza Siri ya jumbe kutaka kujinasua na makucha ya muungano,kwa hiyo ni vizuri kumdhania seif kuwa pandikizi la ccm kuliko lipumba
 
Tuwe wakweli katika kupambania kushika Dola Kuna vyama ambavyo Wala haviwazi malengo hayo au hata kubadili mwelekeo wa hii nchi viongozi wake wapo pale kuvitumia kama kule Kenya wanaita VIOSK vya Tigopesa au mpesa kujipatia pesa na umaarufu wakuitwa Wenyeviti na kama Kuna kongamano au mwaliko utawaona hao viongozi bila hata wanachama na havijulikani malengo yake.

Kwa Mfano CHAUMA DP ACT TLP na hata CUF lipumba alikigeuza hiki chama kuwa CHAKA LAKE la kupiga pesa na kufanya njia rahisi kuonana na Viongozi wa serikali kwa kivuli ni viongozi wa vyama Hawana nia thabiti ya kufanya hii nchi itoke ilipo au kuipush CCM ifanye vizuri zaidi.

Sisi kama WANANCHI tunatakiwa kuamka Sasa kuviunga mkono vyama makini kwaajili ya ustawi wa TAIFA letu maana hata kama chama kilichopo madarakani kinafanya vizuri vyama vya upinzani Huwa vinakitisha ili kifanye vizuri zaidi na zaidi tujitahidi kukubali kushirikiana ili chama chochote kilichopo madarakani kila kinapotazama nyuma kiona Kuna chama kinataka kukipokonya madaraka ndio maendeleo yatakuja kwa kasi
Kikiongonzwa na Chama cha machame a. k. a Saccos. Hili genge ndio lina nyumbu wengi balaa.
 
Back
Top Bottom