Kuna vituo binafsi vya Afya vina uwezo wa kununua vifaa vya kupima COVID-19. Kwanini Serikali isiwaruhusu?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Watu wanapolalamika kuwa serikali haichukui hatua haimaanishi kuwa Lockdown ndyo hatua pekee inayotakiwa kuchukuliwa na serikali. Kunahatua nyingi sana ambazo serikali inaweza chukua ili kusaidia kupambana na janga la coronavirus.

Mojawapo ni kuwezesha vituo vya afya vya private kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa wenye covid 19.

Hapa Tanzania kuna vituo vya afya vikubwa sana vinavyomilikiwa na watu binafsi au vinaubia na serikali ambavyo vinauwezo wa kununua vifaa vya kupima na kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa.

Kuna Mashirika ya kitaifa hivi sasa yanayofadhili programs mbalimbali katika nchi masikini ili kupambana na ugonjwa wa korona. Wanatoa mabilioni ya fedha kusupport huduma za kijamii na afya.

Serikali ingekuwa inaruhusu secta binafsi kuhudumia wagonjwa wa Covid 19, hii ingekuwa fursa kubwa kwa vituo private vya afya. Hivi vituo vya afya vingepata vifaa na mashine za kisasa ili kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wenye covid 19.

Achilia mbali uwezekano wa kupata support kutoka mashirika ya kimataifa. Vipo vitua vya afya vikubwa vyenye uwezo wa kununua vifaaa na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa covid 19. Hata kukopa pesa bank wanaweza sababu hii ni biashara.

Ni dhahiri kuwa serikali haiwezi hudumia wagonjwa wote wa covid 19. Private hospital ziruhusiwe na ziwezeshwe kutoa matibabu ya huu ugonjwa haraka iwezekanavyo.

Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake. Mwenye pesa akatibiwe private na mnyonge akatibiwe Serikalini.
 
Ni kituo gani kinapima covid 19 wakati Tz tunakipimo kimoja mpaka inafikia hatua wengine wanapeleka sampuli kenya zikapimwe ili wapate majibu kwa haraka?

Sent using Jamii Forums mobile app

Zipo hospitali zinapima na kutibu Covid fresh tu, sema mamlaka ya kutangaza ndio inaachiwa maabara kuu ya taifa. Nani amepeleka sampuli Kenya?
 
Back
Top Bottom