Kuna vitu mwanadamu huvifanya kuendana na umri

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Miaka 8 mtoto anaanza kujitambua kama amependeza. Hapa ukimvalisha maroronya mnakwenda kwenye party anaweza kugoma kwenda. Hapa mzazi kuwa makini kuhakikisha mtoto ni msafi hii inamjengea kujiamini akiwa mbele ya wenzake.

11-12 wengine wanaingia puberty age, hapa anaanza kupenda kupendeza hasa kwa machoni mwa jinsia tofauti. Ni vyema kukazania usafi wa mwili kwa mtoto. Hasa pale wakiume wanapoanza kupata wet dreams na wasichana kuingia mwezini. Muonekano ni muhimu kwao.

19-20 kuendelea ni muhimu kufahamu casual wear, formal wear. Hapa walio endelea na masomo wanakua elimu ya juu na wengine wanaanza soko la kutafuta kazi. Hapa wengine wanakutana na wachumba.

Miaka 30 ni kijana ameoa au ameolewa. Ana majukumu nyumbani. Pesa anawaza kulipa kodi, kusaidia wadogo zake, kusaidia wazazi nk. Anaweza apitishe miaka miwili hajanunua nguo mpya. Wengine wanaanza kununua kiwanja.

Miaka 40 watoto wanasoma, majukumu yameongezeka. Unavaa zilizo kabatini. Ni mwendo wa kupiga pasi vizuri. Ukimuona mtu wa 40+ bado anawaza kuvaa viatu na mkanda wa Gucci au kubeba handbag, gauni na viatu vya Gucci inawezekana amefanikiwa sana, au wazazi walimuandalia vingi haku hustle sana au kuna kitu hakiko sawa.
 
Angalia kinachohitajika ukifanye kifanye tu kwa wakati sahihi,

Ukiiona chochote unajaribu then kinakusumbua na kukuachia makovu na sononeko jua ni expensive kwako kitakuumbua

Swala la kuvaa na kununua nguo nzuri halihitaji umri linahitaji mifuko yako tu

Hongera sana mwenye nyuzi umetafakari
 
Maisha yangu yote toka nikiwa 17 nimeyaanza hapo kwenye 30 still nipo 30s ila naishi hapo kwenye 40.

Hakuna kuzubaa!
 
Back
Top Bottom