Kuna viongozi wa dini na viongozi wa majini

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,990
37,053
Utofauti kati ya viongozi wa Dini na viongozi wa Majini ni huu;

1.Viongozi wa dini hawapendi fedha, fedha kwao ni kama tu basic instrument ila si kipaumbele kwao.
Viongozi wa majini ni wapenda fedha.

2. Viongozi wa Dini huongozwa na kweli, huku viongozi wa majini uongo ndio ngao yao. Haijalishi mazingira gani yupo ila viongozi wa dini ukweli ndio silaha yao.

3.Unafiki ni mwiko kwa kiongozi wa dini, anachosema mdomoni ndicho kilicho moyoni. Viongozi wa majini hunena tofauti na matendo yao.

4.Kiongozi wa dini ni mwepesi kuyasema mabaya ya mtu ili atubu na si mwepesi kumsifia mtu kwa jema alilolitenda. Jambo jema linapaswa kutendwa na kila mtu, yaani kutenda jambo jema ni wito kwa wote . Ukitenda jambo jema usitarajie kupongezwa na viongozi wa dini labda viongozi wa majini.

Unakemewa kwa uovu ili utende mema ufike mbinguni, na unapotenda jambo unalostahili mbingu husifiwa maana thawabu utaikuta mbinguni.
 
Back
Top Bottom