Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,714
- 239,291
Wakuu natanguliza salamu
Nimejitokeza tena jukwaani kutaka kufahamishwa kuhusiana na jambo hili .
Maana sasa ni dhahiri kuna haja ya kutenganisha kati ya UCHA MUNGU na UONGOZI wa dini , ili tuwavue baadhi ya watu lawama ambazo tunawapa kwa kutokujua .
Kauli na matendo ya baadhi ya viongozi wa dini zetu zinaonyesha kwamba si wacha Mungu , mifano ni mingi sana , kwamba pamoja na uvunjifu mkubwa sana wa haki za binadamu ndani ya nchi yetu , lakini wao hawaguswi na chochote ! Wengine wamediriki hata kupuuza maoni ya watanzania kuhusiana na ugumu wa maisha , huku wakibeza kwamba maisha ya sasa ni nafuu , ( HUKU WAKIJUA KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUMKIRI SHETANI , MAANA NI UONGO ) ,
Bali ni wazi kwamba wana vyeo vikubwa kwenye madhehebu yao , lakini je kiongozi wa dini ambaye anashabikia maovu katika nchi , kwa vile tu hayakumgusa yeye binafsi ama familia yake ni MCHA MUNGU KWELI ?
Na je ni kweli kwamba baadhi ya madhehebu yanaruhusu baadhi ya watu wasio wacha Mungu kuwa viongozi ndani ya madhehebu hayo ?