Kuna viongozi sijawasikia muda katika Vyombo vya Habari tofauti na kipindi cha nyuma. Wewe umemkumbuka nani?

Hahahahaaaa!
JamiiForums1370372167.jpg
 
Awamu ya 5 kuna viongozi waliwika sana hasa kwenye vyombo vya habari na mitandao mbali mbali ya kijamii ambao haipiti siku bila kuwaona au kuwasikia ila kwa sasa imekuwa tofauti wapo kimya mpk kuona kama awapo katika awamu hii ya 6.

Wewe unamkumbuka nani? Mimi Mh Prof Palamaganda Kabudi mzee sijamsikia muda
Makonda
 
Nkamia na kessy vipi hoja zao,kange, bashiru, polepole hawasikiki kabisa.
 
Kuna yule mpuuzi aliyejipa cheo cha Shehe wa Mkoa anaitwa Hadi.. kapotea mazima
 
Awamu ya 5 kuna viongozi waliwika sana hasa kwenye vyombo vya habari na mitandao mbali mbali ya kijamii ambao haipiti siku bila kuwaona au kuwasikia ila kwa sasa imekuwa tofauti wapo kimya mpk kuona kama awapo katika awamu hii ya 6.

Wewe unamkumbuka nani? Mimi Mh Prof Palamaganda Kabudi mzee sijamsikia muda
Huyo unayemsema, mbona juzi tu kaunguruma kwenye sherehe sijui ya wanasheria pale Dodoma!

'Roli modo' wangu Majaliwa wamemkata ngebe hadi vyombo vya habari vimefubaa, vinashindwa kuuza habari hadi vinakopi "sipichi" zake za nyuma za awamu ya5 na kutudanganya kwamba ni habari mpya kasema!

Waziri wa madini Biteko sijamsikia siku nyingi na hata akisikika hapazi sauti tena, anaongea pole pole kwa kunong'ona kiuoga!

Yuko wapi Rc hapi, alipita Tabora muda wa wiki1 tu pakachangamka na kupendeza, sijui alikohamishiwa kaenda zibwa mdomo na nani tu!

Yuko wapi huyu kijana naibu waziri wa elimu Tamisemi, nimemsahau jina, ni huyu kijana aliyehamia sisiem juzi juzi na kupewa cheo, alikuwa akiunguruma pindi akaguapo miradi ya ujenzi wa madarasa hadi nafurahi.

Waziri wa mazingira naye kapatwa na nini jamani, maana kipindi yupo Tamisemi nilikuwa napenda sana ziara zake za ufuatiliaji wa ujenzi wa miradi ya serikali.

Yuko wapi Aweso? Waziri wa maji anaye jiamini, mtunga sera na mfuatiliaji mzuri wa miradi ya maji.
Siku hizi haungurumi tena, anaongea pole pole kama mmisionari!

Yuko wapi waziri wa ujenzi Mbarawa?
Tangu arejeshwe mamlakani, kawa mpole kupitiliza hadi namhurumia, maana ukimya siyo silka yake, nadhani kuna shinikizo linamfanya asiongee!

Kamanda Mroto wa Polisi Dodoma, siku hizi simsikii, kahamishiwa wapi?
Huyu nilivyokuwa napenda kumsikiliza na hiyo 'mother tongue' ya kiswahili chake, wa'alah hata kama nilikuwa nafanya, nilkuwa ninaacha ili kumsikiliza yeye.

Enhee, Cyprian Musiba kwanini haongei?
Uanaharakati wake umeishia awamu ya 5 tu?
Ama Camillius Membe kamkata ngebe kwa mikesi?

Viongozi wa awamu ya6 hawana amsha popo, ukimya wao huu unawaharibia cv, maana inaonekana kama hawafanyi kazi na pia inawapa ari wapigaji kuona kwamba kumbe sasa serikali ya wamu hii ni shamba lao la bibi ndiyo fursa yao ya kupiga.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr Abbas, alifikia hatua ya kumfuatilia na kujibu kila anachoongea jk (lengo kujipendekeza kwa wendazake sababu nae alikuwa mtu wa namna hiyo i.e kumponda j.k) mpaka jk akafikia hatua ya kushangaa nini kimempata bwana mdogo!! Sasa yupo dorooooo
Alisikika akisema magufuli lazima aongezewe muda!!!!
 
Kessy wa Nkasi. Hakurudi bungeni, alishindwa na ' Kipusa' wa Chadema
Kessy sijui aliwezaje kuwa mbunge ingekuwa vizuri tungekuwa na tume huru ambayo inawafanyia vetting baadhi confidante ambao uwezo wao kujenga hoja unafikilisha
 
Back
Top Bottom