Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Huwa nashangazwa saaaaana na jambo hili:
Binti akikaribia kuolewa anatafutiwa mtu wa kumfunda mambo ya ndani (chumbani), wenyewe wanaita Kungwi. Basi anapikwa, anachemshwa, anakaangwa, anabanikwa, anaokwa na kila liwezekanalo.
Hivi maana yake nini?...maana humo ndani binti anafundishwa tu kumridhisha mume na kumfurahisha mume.
Mimi naona angefundishwa sana habari za jinsi ya kulea watoto, jinsi ya kubudget pesa kwenye familia, jinsi ya kumshauri mumewe kwenye masuala mbalimbali ya kimaisha, jinsi ya kuishi na familia yake mpya atakayokutana nayo huko, jinsi ya kukirimu wageni, jinsi ya kujijali yeye mwenyewe kiafya, kimwili, na kiakili kwani mama ndiye mlezi mkuu wa familia.
Kwanza hayo mambo ya chumbani wala hayana tija maana siku hizi vijana sie hadi tuoane tunakuwa tushafunuana kwahiyo huyo dada hadi anaolewa ujue mapigo yake yashakubalika. Cha msingi ni afundishwe tu mambo yenye tija yatakayosaidia ustawi wa familia.
Nawasilisha.