Kuna viashiria vyote vya hujuma kwa Taifa, uchunguzi wa haraka unahitajika kuokoa Taifa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehiji hilo, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM.

Usalama wa Taifa ulianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho hadi sasa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence)..., lakini upande wa foreign assets ndo wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi, Hawa wamegawanyika..., kuna wanaofanya kazi kufatilia mienendo na tabia za maofisa na askari ndani ya vikosi hata nje, kuna wakusanya habari za ndani ya nchi zenye maslahi na jeshi, mfano kuna watu kazi yao ni kusoma magazeti daily, magazeti ya ndani na hata ya majirani au kuangalia tv, au kushinda kwenye mitandao kama humu, pia kuna ambao kazi yao ni kunasa mawasiliano ya jirani zenu, na kuna foreign assets.., wanaishi na kukaa nje...., kuna wanaotumwa for a....!!!

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa ofa ya Ushindi wa Chadema katika uchaguzi wa Chama kwa zaidi ya nusu bei, 30,000 tu badala ya bei halisi 80,000/=

Nunua 30,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo. Nje ya dar utachagia nauli 8,000

IMG_20191221_223316_821.jpg
images (1).jpg
 
...Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa ofa ya Ushindi wa Chadema katika uchaguzi wa Chama kwa zaidi ya nusu bei, 30,000 tu badala ya bei halisi 80,000/=

Nunua 30,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo. Nje ya dar utachagia nauli 8,000...
Endelea kupiga miayo. Kitabu hakiuziki. Biashara imedoda.
 
Wakati siungi mkono mengi yanayofanyika huko ndani ya serikali ya CCM; napenda pia kutahadharisha hoja nyepesi nyepesi kama hizi za akina Yericko.

Ndio, tunao watu, waTanzania wenzetu walio tayari kuuza chochote ndani ya nchi hii kwa manufaa yao. Hao wapo.

Lakini pia najua, hata huko ndani ya CCM iliyooza na serikali yao, pia wamo waTanzania wanaoweka maslahi ya taifa hili mbele kuliko kitu chochote.

Hiyo Bagamoyo, ambayo kiuhakika hatujui kilichokuwemo katika mkataba ule hadi usimame, pamoja na kwamba ni mradi wa kuvutia sana kama unavyoueleza hapa, athari zinazotokana na tusiyoyajua ndani ya mradi huo inabidi tuwe na tahadhari ya kulaumu tu kiujumla jumla hivi.
Bagamoyo haiendi popote, itajengwa kwa utashi wetu na kwa faida yetu. Tusisukumwe tu na Nakala sijui Nampula kuuvamia

Nashangaa katika yote hayo hukugusia kabisa "Kurasini" - unaukumbuka mradi ule, hadi wananchi wakahamishwa? Sasa nikwambie, Mombasa wanateremsha "Dongo Kundu" n a jiwe la msingi limewekwa hivi juzijuzi.

Tusiwe na pupa za kukimbilia na kukurupukia mambo wakati hatuna taarifa mhimu za kutuwezesha kutoa maoni makini.

Uzuri wa mradi sio lazima sisi tuwe ndio 'cetre' ya dunia, na tukasahau tunachopata kutokana na mradi huo.

Sawa, upande wa pili pia tunayo matatizo. Kama ndege zetu nazo zitaanza kutegemea ruzuku badala ya kuzalisha faida, huo nao utakuwa ni ukurupukaji mkubwa; pamoja na kwamba tutakuwa tunajihesabu kuwa tunalo shirika letu wenyewe la ndege.
Kinachotakiwa hapa, ni hawa waliofanya uamzi wa kulifufua shirika hili, wasimame kidete kweli kweli, wahakikishe shirika linazalisha faida. Vinginevyo hii itakuwa ni aibu kubwa kwao.

Rwanda watakata Tanzanite, Almas na kuchenjua dhahabu? Kweli?
Unasema Rwanda hawana madini, hayo yanayotumika kwenye simu na waliyokuwa wameamua kuwa wanayasafirisha kupitia Mombasa badala ya Dar es Salaam kwa wizi wetu, sio madini? Acha wajenge, lakini haituzuii nasi kujenga kama uhitaji upo, si biashara?

Siku nyingine ntakuomba uweke mkazo kwenye ujenzi wa miundo mbinu itakayotuunganisha moja kwa moja na waKongo, tuache kutegemea kupita kwa waRundi na waRwanda!

Ngoja nipite pembeni - ulishawahi sikia 'barabara iliyojengwa na waKenya kupitia Tanzania" ili kuwafikia waRundi? Au hata hii nyingine iliyopata ufadhiri hivi karibuni toka Benki ya Afrika (AfDB); inayotoka Mombasa kwenda hadi Bagamoyo? Eti hiyo barabara ni ya kurahisisha kupitisha mizigo toka Mombasa hadi Congo, Burundi, Rwanda, hadi Sudan. Ndio, hilo ndilo andiko lililosaidia kupata hiyo pesa ili barabara ijengwe. Kwa bahati mbaya sisikii barabara zinazojengwa kutuunganisha na Uganda, kila mara ni sisi na Kenya, kulikoni?

Sasa kama sio kupitia pembeni, utakuitaje huko?

WaTanzania, hasa mliopo ndani ya hizi serikali, hata kama ni serikali imeundwa na CHADEMA, acheni kukurupuka kwa mihemko.
 
Tatizo la Tanzania ni ubinafsi wa kutaka kuonekana tunamiliki bila kuwa na uelewa wa uchumi na biashara.


Fahati yetu ni kumiki ndege 11, zinafanya nini eti hilo sio jukumu letu.

Madini ndio hovyo kabisa.. tunazungumzia mapinduzi ya kuongeza bil 100 kwa mwaka wakati tuliamijishwa kwamba tungepokea tr 400.

Nadhani tuache kuchagua viongozi gizani, yamkini tungepata viongozi werevu wa mambo wasio na tamaa ya utajiri. Kalamu1,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom