Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.

Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga! akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!

Nyerere yupi yule mtumishi wa kanisa kibaraka aliiyewekwa madarakani Na waingereza baada kupinduliwa?
 
Kaka Pasco.

Nikuambie jambo fulani hapa.
Unajua walichokuwa wanapitia Wapinzani na wadadisi wengi wa kisiasa... Humphrey alikuwa anajua na usikute aliidhinisha projects mbalimbali za kipuuzi dhidi ya Watanzania wenzake.

huyu kimbwenelehi Kiroboto alipaswa kwanza kukiri hadharani ushiriki ama kutoshiriki kwake kwenye madhila ya kubinafsisha siaza kipindi chote alichokuwa Mwenezi.
Mkuu Msanii, mimi ni muumini wa karma, hivyo kama Polepole has a hand kwenye yale madhambi ya wasiojulikana, na udhalimu mwingine wowote, karma imeisha kula vichwa na kama na yeye anahusika, karma yake ipo njiani na lazima itamfikia.

Kwenye kazi za kutumwa, mtu ukitumwa kufanya chochote, hata kama ni udhalimu, kisha wewe ukatekeleza kama ulivyotumwa, huo ndio unaitwa utii.

Watekelezaji wa udhalimu wowote wa kutumwa, karma haiwahusu watekelezaji, inawahusu waliopanga na waliotoa amri ya utekelezaji.

Hata wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu, kama walitumwa kwa amri halali, karma haiwahusu, wao walikuwa wanatekeleza amri halali, hivyo karma haiwahusu, inamhusu yule tuu alie watuma.

Vivyo hivyo kwa Polepole, kama alitumwa then karma haiwahusu!.
P.
 
Mkuu Gobole , asante sana kwa mchango huu. Wewe ni miongoni mwa watu wachache humu waelewa, Polepole ameusema ukweli mchungu supported by facts za kwenye katiba, lakini humu, tuna mijitu mijinga ajabu!, akili zao finyu haziwezi kumwelewa Polepole!.

Kama Mwalimu Nyerere aliwahi kusema serikali yetu imeacha mambo mema na kukumbatia mambo ya kijinga, ndicho hiki hiki Polepole anachokifanya sasa.
P
Tuna jamii isiyopeenda kusoma wala ku verify facts, Jamii isiyopenda kushindana kwa hoja. Jamii inayoamini ktk kujadili watu na sio hoja, jamiii inayopenda majungu na uzandiki, inayoamini ktk personal attacks kuliko kujibu hoja,jamii iliyojaa unafiki na watu wafuata kufuata upepo ilimradi waliskia fulani kasema hivyo ili hali wao wenyewe hawawezi ku prove chochote ktk kisemwacho...jamii inayofurahia wapiga dili na wahuni kwakua tu wanawapa chochote kitu na kuwa dicredit honest men kwakua hawana cha kuwapa.
Dont expect anything good out of them.
Bro ukiweza waelimishe, wakielimika ni jambo la heri wakigoma waache na ujinga wao.
 
Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.

Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga! akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!

Paskali usimtetee huyo kigeugeu anayejifanya mlokole huku akisapoti mauaji na upotevu wa watu ulikuwa ukifanya na Magufuli unasema na unamfananisha na Nyerere?You are better than that Paskali. Huyo Polepole, kinyonga, aliyepewa cheo akasema hakuna umuhimu wa katiba, lakini mwanzo akasema kuna umuhimu wa katika kwa kukazia halafu anabadilika, huyo right handman wa Magufuli aliyehusika na upotevu, upigwaji wa risasi wa raia, mauaji ya wapinzani, na ununuzi wa viongozi wa upinzani unamfananisha na Nyerere?
 
Mkuu Msanii, mimi ni muumini wa karma, hivyo kama Polepole has a hand kwenye yale madhambi ya wasiojulikana, na udhalimu mwingine wowote, karma imeisha kula vichwa na kama na yeye anahusika, karma yake ipo njiani na lazima itamfikia.

Kwenye kazi za kutumwa, mtu ukitumwa kufanya chochote, hata kama ni udhalimu, kisha wewe ukatekeleza kama ulivyotumwa, huo ndio unaitwa utii.

Watekelezaji wa udhalimu wowote wa kutumwa, karma haiwahusu watekelezaji, inawahusu waliopanga na waliotoa amri ya utekelezaji.

Hata wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu, kama walitumwa kwa amri halali, karma haiwahusu, wao walikuwa wanatekeleza amri halali, hivyo karma haiwahusu, inamhusu yule tuu alie watuma.

Vivyo hivyo kwa Polepole, kama alitumwa then karma haiwahusu!.
P.
Hata ukitumwa ukafanya kitu ambacho ni dhalimu lazima Karma ikuhusu na hiyo inakuwa responsibility yako. Mbona waliohusika na Hitler wakati wa Holocaust wote walinyongwa...refer the trial of Nuremberg. Unaambiwa ukaue mtu na unaenda kichwa kichwa halafu unasingizia wengine? Come on Paskali, you are better than that!
 
Nashukuru sana kwa majibu mazuri uliyoweka.

Ni kwamba kuna syndrome inatutafuna Waafrika hususani Watanzania. Ibara ya Katiba inayotoa haki ya kuishi imeiwajibisha serikali kwamba hukumu yeyote ya kutoa uhai wa mtu lazima iwe imetolewa na mahakama. Tukija kwenye uhalali wa amri unakuta kwamba kichwa kinachoamua kupanga wizi kisha miguu na mikono vikatekeleza amri halali ya kichwa, basi vyote hujikuta matatani endapo mwizi atakamatwa na kuhukumiwa.

Humphrey anajitahidi kujipaka manukato ili anukie lakini uhalisia ni kuwa hajaoga, hajawa msafi hivyo ajisafishe kwanza ndipo aweze kuja na hoja tunduizi.

Najaribu kukushaeishi, jaribu kuwaza endapo angeendelea na nafasi yake chini ya SSH, je angekuja na hizi hoja za kuwaita wakubwa zake WAHUNI?

Kuna namna ya kuweka mambo sawa lakini siyo kwa kuwachafua wengine.

Nakumegea siri ndogo. Humphrey na wenzake wanapiga drama tutoke kwenye hoja za Katiba Mpya.

Nimelipia kadi yangu ya CCM hadi 2026, na sihami
 
Tuna jamii isiyopeenda kusoma wala ku verify facts, Jamii isiyopenda kushindana kwa hoja. Jamii inayoamini ktk kujadili watu na sio hoja, jamiii inayopenda majungu na uzandiki, inayoamini ktk personal attacks kuliko kujibu hoja,jamii iliyojaa unafiki na watu wafuata kufuata upepo ilimradi waliskia fulani kasema hivyo ili hali wao wenyewe hawawezi ku prove chochote ktk kisemwacho...jamii inayofurahia wapiga dili na wahuni kwakua tu wanawapa chochote kitu na kuwa dicredit honest men kwakua hawana cha kuwapa.
Dont expect anything good out of them.
Bro ukiweza waelimishe, wakielimika ni jambo la heri wakigoma waache na ujinga wao.

Usiilaumu jamii kwani huyo aliyewalea aitwaye baba wa Taifa lao aliwalea katika somo hilo
 
Pascal Mayalla

Hakuna CCM yoyote wa sasa mwenye kufanana mitizamo ama mawazo na Mwl Nyerere, hakika hakuna...

Huyu Polepole ndani tu ya miaka kama minane au kenda hivi, ameweza kuwa na kama rangi tatu tofauti, mosi rangi ya bunge la katiba; mbili, rangi ya serikali ya JPM; tatu, rangi ya sasa isiyo na jina bado...

Huyu Polepole ndio wa kutuhubiria sasa kwamba watu waachwe waongee kwa kuwa uhuru wa kutoa mawazo kila mwenye mdomo anao!! Huyu si alikuwa ni sehemu ya serikali iliyowaziba midomo wapinzani huyu???
rangi ya sasa isiyo na jina bado...

Imeshajulikana, ni kiroboto"
 
Hata ukitumwa ukafanya kitu ambacho ni dhalimu lazima Karma ikuhusu na hiyo inakuwa responsibility yako. Mbona waliohusika na Hitler wakati wa Holocaust wote walinyongwa...refer the trial of Nuremberg. Unaambiwa ukaue mtu na unaenda kichwa kichwa halafu unasingizia wengine? Come on Paskali, you are better than that!
Karma operates on conscious, mtu ukitumwa kufanya udhalimu wowote kwa amri halali, hata kama conscious yako ikikutuma ukatekeleza, karma is not upon you, but upon aliyekutuma.

Lakini kama ukitumwa kufanya udhalimu wowote kwa amri batili, na conscious yako ikakuambia hiyo ni amri batili na bado ukafanya karma inakula both, kwako na kwa aliyekutuma!.
P
 
Wewe Mkuu VinJoe , ni mjinga!.
Kuwa mjinga sio tusi, ni ile hali tuu ya kutokujua jambo, ukifundishwa unafundishika, ujinga unakutoka, unakuwa mwerevu!.

Nyerere aliichukua nchi ikiwa na mfumo wa vyama vingi, akaifanya kuwa nchi ya chama kimoja. Ni Mwinyi ndiye aliyerudisha vyama vingi ile 1992.
Now you know, sasa wewe sio mjinga tena!.

Kuna wengi wasiomuelewa Polepole, ni wajinga tuu!. Waerevu tunamwelewa, kuna vitu anasema kweli.
P
Ndugu kweli ina maana hujui ni kwasababu gani Mwl. Aliingiza Tanzania kwenye mfumo wa chama kimoja mwaka mmoja baada ya Muungano?
Na pia hujui kwanini miaka ya 1990's ndio nchi nyingi za Afrika zikarudi kwenye mfumo wa vyama vingi?
Ina maana hujui Kihistoria mifumo hii ilitokea katika mazingira ya Ukomunisti, Ujamaa au Ufashisti?
Ina maana pia ulikua hujui kua Mwl. Utawala wake na hata seara zake zilikua zimeadhiriwa kwa kiasi kikubwa na mivutano ya kambi za mashariki na magharibi.. na ndio maana baada tu ya mfumo wa kikomunisti ulivyoanza kuporomoka Jamhuri za Kisovieti na nchi za Ulaya mashariki siasa za mataifa mengi ya Afrika hazikua salama na ndipo mfumo wa vyama vingi ukarudi.

Nilichokimaanisha ni hiki ndugu yangu Dr. Nyerere aliachia madaraka nchi bado ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja(Angekua JPM ndio rais kipindi hic ho na HPolepole ndio wapambe 😂 sijui nini kingeikuta Tanzania yetu) ambapo tuliingia kwenye mfumo wa chama kimoja kutokana na imani ya mwalimu juu ya ujamaa na pia ni mtu asiekua anapenda ukabila na udini na alifanikiwa maana ni ukweli usiofichika kwa leo ni hii tu TANU》CCM isiyokua na udini sana na ukabila ndani mwake lakini vyama vingine vilivyo vingi vinatajwa na tabia za ukanda udini na hata ukabila pia.
Kwahio tunaona nini sababu ya Mwl. Nyerere kuingia katika mfumo wa chama kimoja.. alikua ana malengo yake yakutimiza sera zake za kiujamaa alizoishi akiziamini kua ndio zitatutoa katika ujinga umaskini na maradhi.

Huyu H. Polepole unayemtetea hapa na kuthubutu kumlinganisha na muasisi wa hili taifa kwangu na labda uelewa wangu huu mdogo unanifanya ni hisi unamtukana Dr. Nyerere. Kwangu si sawa hata kidogo maana nimezaliwa Dr. Nyerere hayupo madarakani na sikuweza hata kusikiliza hotuba zake live ila najua mawazo yake misimamo yake na nini ilikua mawazo yake juu ya Elimu uchumi na hata siasa za nchi hii.. maana vilikua vipana na vyenye maslahi kwa taifa Zima.
Sasa huyu unayemfananisha namsikiliza namsoma ila sijui mawazo yake mapana yenye maslahi mapana kwa taifa hili zaidi najua ni mtu mwenye kubadilika na muoga huku akibonyeza panapobonyea tu. Polepole yule wa kipindi cha mchakato wa katiba na kipindi chote cha utawala wa JK na huyu wa sasa hivi mwenye kujutia kushindwa kuwashuhulikia wahuni sidhani kama ana stahili mfananisho unaompa huyu si kiongozi wa wananchi ila wa watu wachache na wasukuma😂
Kama kweli ni mtu wa misimamo angetakiwa kuhoji sana kipindi cha uongozi wa Dr. Pombe sio sasa hivi au sio kipindi kile cha JK.
JAMAA ANABONYEZA PANAPO BONYEA NA SI MTU WAKUAMINIKA AU WAKUSIKILIZA SERA ZAKE NA KUZIFUATA MAANA ATABADILIKA VILE USIVYOAMINI
ALICHOKUA ANAONGEA KWENYE MIDAHALO MIAKA KAMA 10 ILIYOPITA NI TOFAUTI SANA NA ANACHOKIAMINI LEO HII.
BROTHER SIJASHAWISHIKA BADO KUA ANAFAA HATA KUFANANISHWA NA MTU KAMA OSCAR SALATHIEL KAMBONA
 
Mkuu koma kumfananisha Hayati Mwl. JKN na viwatu vya ajabu!!
NB: Walahu yule Pole Pole wa Katiba Mpya alikubalika sana... Yule alojiunga na serikali ya JPM alichafuka mazima...
Huyu wa sasa amekosa moral audacity!
Asitufanye wajinga!
 
Karma operates on conscious, mtu ukitumwa kufanya udhalimu wowote kwa amri halali, hata kama conscious yako ikikutuma ukatekeleza, karma is not upon you, but upon aliyekutuma.

Lakini kama ukitumwa kufanya udhalimu wowote kwa amri batili, na conscious yako ikakuambia hiyo ni amri batili na bado ukafanya karma inakula both, kwako na kwa aliyekutuma!.
P
Unatakiwa ukatae kama kuna options ya kujiuzulu au kutofanya na ukatafuta hifadhi yoyote pale. Kwa hiyo ukiambiwa kamuue jirani yako na ukifanya hakuna Karma?
 
Kama wewe ni muajiriwa na moja ya majukumu yako ni kuua, ukipewa amri halali ya kumuua yoyote, na sio tuu jirani yako, sometimes hata ndugu yako wa damu na ukaitekeleza, hapo unakuwa ni umetimiza tuu wajibu wako wa kuua, hakuna karma kwa upande wako, bali ni kwa aliyekutuma. Ndio maana jeshi, polisi, usalama, na wauawaji wengine wanaweza kuua with impunity na tunawaona, wanaendelea kudunda.

Karma ni aliyetoa amri, na ndio maana tumeshuhudia karma ikila vichwa vya watoa amri, huku watekelezaji wakidunda.

Ahsante kwa kufahamisha...well said Paskali
 
Ni kweli jamaa ana akili Sana Hilo lipo wazi lakini tatizo ni mnafiki mkubwa Sana .Hana msimamo maana ana tamaa ya Mali .Yule mtu aliekua anapigania katiba mpya kapewa cheo zen kaisaliti Sasa inakuaje umfananishe na Nyerere.Au ungetuwekea ufanano wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.

Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga! akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!

Ivi ni watu wenye akili ndio wanaotoa likes au?
 
Mkuu Eng. Zezudu , mtu kufanana na mtu mwingine sio lazima wafanane akili!, akili ni nywele, kila mtu ana zake!.
Polepole anafanana na Nyerere, anavyoongea, he speaks in parables, hivyo only the few privileged ones ndani ya CCM ndio wanaomwelewa. Ameamua kuifuata falsafa ya Mwalimu, "Nitasema kweli daima". Anachosema ni kweli japo ni ukweli mchungu.
P
Yaani unadiriki kumuita Polepole "msema kweli" Yaani katetea katiba moya, kashiriki kuiandaa, then kabadili gia mara baada ya kupewa cheo!!!! Huyu mi namwita mchumua tumbo si msema kweli.

Kama wewe kweli ni mchambuzi jiulize je asingepewa cheo angebeki na msimamo wake ule ule wa katiba mpya au angebadilika?
 
Mkuu Msanii, mimi ni muumini wa karma, hivyo kama Polepole has a hand kwenye yale madhambi ya wasiojulikana, na udhalimu mwingine wowote, karma imeisha kula vichwa na kama na yeye anahusika, karma yake ipo njiani na lazima itamfikia.

Kwenye kazi za kutumwa, mtu ukitumwa kufanya chochote, hata kama ni udhalimu, kisha wewe ukatekeleza kama ulivyotumwa, huo ndio unaitwa utii.

Watekelezaji wa udhalimu wowote wa kutumwa, karma haiwahusu watekelezaji, inawahusu waliopanga na waliotoa amri ya utekelezaji.

Hata wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu, kama walitumwa kwa amri halali, karma haiwahusu, wao walikuwa wanatekeleza amri halali, hivyo karma haiwahusu, inamhusu yule tuu alie watuma.

Vivyo hivyo kwa Polepole, kama alitumwa then karma haiwahusu!.
P.
Acha ujinga wako wewe sijui hata sheria umesoma wapi. Kwenye chain of command ya criminal responsibility yupo mtoa amri na mtekelezaji. Na yule mtekelezaji kama haridhiki na kinachoendelea alitakiwa at least ajiuzulu hata kimya kimya akae pembeni....
 
Back
Top Bottom