Kuna uwezekano Wananchi wa Tanzania kuwa vinara wa unafiki ulimwenguni?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,554
2,000
Unafiki. Ni hali ya mtu kutenda au kuongea maneno tofauti na yale anayowaza akilini. Kama vile kusema jambo fulani ni zuri ilihali nafsini mwake anajua ni baya.

Nchi hii wanaweza kusema wanakuchukia na kukutukana kila kona kumbe ukweli ni kuwa wanakupenda sana ila wanaona aibu kuonyesha hisia zao matukio yanayoendelea yanazidi kudhihirisha unafiki uliopo.

1. Corona
2. Makinikia
3. Kesi za kisiasa
4. Mapato na matumizi
 
Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
589
1,000
Naongezea; Unafiki ni hali ya mtu kutenda tofauti na maneno anayoyasema siku zote. Yaani unahubiri hiki, lakini unatenda kile!

Kwa mfano, unasema: "Rushwa ni mbaya sana" lakini ukienda pembeni unaomba rushwa.

Ni kweli, inawezekana Tanzania unafiki upo. Kwa mfano; Bwana yule alikuwa anapenda kusema maendeleo hayana vyama, lakini ilipofika kwenye uchaguzi wapinzani wakaenguliwa.

Kwa hoja hizi (Corona, Makinikia, Kesi za kisiasa, Mapato na matumizi), tunaweza kusema wasaidizi hawakuwa wanafiki, bali ni njaa na kumwogopa Jiwe. Rejea yule bwana msajili wa hazina, alipompinga Jiwe, ni nini kilitokea.
 
Matokeo ya njaa ni unafiki kwa kifupi njaa na unafiki ni pande mbili za shilling uwepo wa kimoja wapo usababisha uwepo wa kingine..
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,248
2,000
Maisha ya watu wasiohakikishiwa ulinzi na katiba lazima yaendeshwe kwa unafiki plus kujipendekeza vinginevyo ya Ben Saanane yatakuhusu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom