Kuna uwezekano wa ndoto hii kuwa na mambo ya kiroho au ni kawaida tuu?

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
10,488
29,684
Salamu kwenu JF members, niombe kwenu tafsiri au maana ya ndoto hii.

Ni mara nyingi nimekua nikimuota msicha mmoja nilie wahi kuishi nae miaka 3, lakini kwa bahati isio njema tuliachana.

Tokea alipo ondoka nimemuota mara nyingi sijaweza kuhesabu na mara nyingi ninapomuota ndani ya ndoto kunakua na kulaumu hivi kwa kilichotokea.

Ila juzi juzi nilimuota nikiwa nimelala nae nikijadaliana nae alivyo niacha na roho huwa inaniuma sana ndani ya ndoto. Nikamuota tena kwa namna hio kwa mara nyingine.

Lakini jana kwa nasibu nilimuona kwa macho yangu kwa mara ya kwanza toka 2014 pasaka na ilikua kanisani, sasa jana niliishiwa nguvu gafla baada kumuona ingawa alikua kwenye pikipiki.

Usiku wake yani wa kuamkia leo nimemuota tena lakini leo ndoto imeenda mbali zaidi, nilikua nimelala nae na nilikua namlaumu hivi, ye akasema sasa mimi ningefanyaje!

Ila kwenye kulala huko nikazini nae nilistuka pale pale nilijikuta nimejichafua ingawa nilikua kwenye ibada ya maombi ya mfungo kwa jambo fulani lakini kitendo hiki kimenifanya nijiulize sana kwanini hanitoki kwenye ndoto? Na kila nikimuota asubuhi yake nakuwa nampenda mpenda fulani hivi.

Na tokea alivyoniacha sijawahi kuwa na mahusiano yoyote kila nikijaribu naishia kutemwa tuu, na kiimani japo ni mdhaifu kibinadamu lakini dhambi naiepuka sana.

Msaada ndugu zangu ni kawaida tuu au kuna jambo lisilo la heri hapo?

Kila la heri.
 
Hakuna njia nyingine zaidi ya kujitenga naye kiroho! Yaani rohoni wewe na yeye bado mpo pamoja...sijajua level yako kuhusu mambo ya kiroho...ila jitenge naye kwa maombi...naam ukifanya hivyo hutamuota tena! Na pia elewa kuwa kama ndoo imejaa maji huwezi kujaza maji mengine...hadi yaliyopo yaishe au uyatoe ndipo unaweza kuweka mengine! Hata kwako poa...kwa kuwa bado uko na huyo mwanamke rohoni ...hata ukipata mwingine hamuzi kudumu kwenye mahusiano kwa sababu hana pa kukaa Mwenye Moyo wako! Sharti umtoe Wa kwanza ndipo waweza kuwa na mwingine. Kila la hero.
 
Mkuu pole sana. Matatzo au magomvi ya familia hua ya kijinga jinga sana, nataka nijiaminishe Kua huenda mliachana kwasababu za kipuuzi sana NA hatimae mwenzio akaondoka. Chakufanya kaa chini tafakar n then muite kirafiki kabisa mkae pamoja muongee wenyewe bila kuita third part yyte. Naamini mtapata suluhisho.

Unamuota sana kwakua wapenda sana NA wamuwaza mda wote. Huenda nae afanya hvyo hvyo!!

Pole sana mkuu.
 
Salamu kwenu JF membars, niombe kwenu tafsiri au maana ya ndoto hii.
Ni mara nyingi nimekua nikimuota msicha mmoja nilie wahi kuishi nae miaka 3, lakini kwa bahati isio njema tuliachana. Tokea alipo ondoka nimemuota mara nyingi sijaweza kuhesabu na mara nyingi ninapomuota ndani ya ndoto kunakua na kulaumu hivi kwa kilichotokea.
Ila juzi juzi nilimuota nikiwa nimelala nae nikijadaliana nae alivyo niacha na roho huwa inaniuma sana ndani ya ndoto. Nikamuota tena kwa namna hio kwa mara nyingine.
Lakini jana kwa nasibu nilimuona kwa macho yangu kwa mara ya kwanza toka 2014 pasaka na ilikua kanisani, sasa jana niliishiwa nguvu gafla baada kumuona ingawa alikua kwenye pikipiki.
Usiku wake yani wakuamkia leo nimemuota tena lakini leo ndoto imeenda mbali zaidi, nilikua nimelala nae na nika nilikua na mlaumu hivi, ye akasema sasa mimi ningefanyaje! Ila kwenye kulala huko nikazini nae nilistuka pale pale nilijikuta nimejichafua ingawa nilikua kwenye ibada ya maombi ya mfungo kwa jambo fulani lakini kitendo hiki kimenifanyanya nijiulize sana kwanini hanitoki kwenye ndoto? Na kila nikimuota asubuhi yake nakuwa nampenda mpenda fulani hivi.
Na tokea alivyoniacha sijawahi kuea na mahusiano yoyote kila nikijaribu naishia kutemwa tuu, nakiimani japo ni mdhaifu kibinadamu lakini dhambi naipuka sana.
Msaada ndugu zangu ni kawaida tuu au kuna jambo lisilo la heri hapo? Kila la heri.
Jini mahaba huyo sio bure
Kila cku umuote yeye
 
Mkuu....
Una kila dalili ya kwamba, bado unayo mapenzi makubwa kwa huyo mwanamke aiseeee
 
Mkuu pole sana. Matatzo au magomvi ya familia hua ya kijinga jinga sana, nataka nijiaminishe Kua huenda mliachana kwasababu za kipuuzi sana NA hatimae mwenzio akaondoka. Chakufanya kaa chini tafakar n then muite kirafiki kabisa mkae pamoja muongee wenyewe bila kuita third part yyte. Naamini mtapata suluhisho.

Unamuota sana kwakua wapenda sana NA wamuwaza mda wote. Huenda nae afanya hvyo hvyo!!

Pole sana mkuu.
Nashukuru saana ndugu yangu, ila sababuu kuu ilikua ni kutomtimizia malengo yake pengine, japo nilijitahidi kadri ya uwezo wangu ila uchumi haukua sawa sababu ndio nilikua naanza maisha kipindi hicho, ndio ilikua sababu kuu japo alisingizia vingine na mimi niliona mengine.
 
Pole sana ndugu yangu naona wewe ni mchanga kiroho ndo mana anakudhibit rohoni Fanya mambo yafuatayo atakuacha rohoni na mwilini itadhihirika kwanza kabisa omba maombi ya kufunguliwa na mapepo ya kifamilia mapepo ya kichawi mapepo ya uzinzi manuizo mabaya zidi ya maisha yako maagano ya kifamilia yote unayakataa kwa jina la yesu ndoto za kuzimu hafu unamkataa kwa mamlaka uliyonayo kupitia jina.la yesu
 
Pole sana kaka,cha msingi punguza hasira na fanya meeting nae hata kwa muda wa saa moja mm nahs ataelewa kama anajua nn maana ya kupenda wala sio jini mahaba au kahaba hayo ni mapenz kwa x wako
 
kama ulifungamanisha nafsi yako na ya kwake itakusupumbua sana.pengine uliapa kutotengana naye wakt mkiwa kwe mahusiano so itakua ngum kumsahau .jitahd kujitoa kwake kiroh ndip utakua huru
 
Tabia yangu ya kutoamini wala kufuatilia ndoto, naona imeniepusha na mengi
^^
 
huenda uliwekeana nae magano ndomaana unatesa tengua hayo maagano atatoka rohon mwako
 
Pole sana ndugu yangu naona wewe ni mchanga kiroho ndo mana anakudhibit rohoni Fanya mambo yafuatayo atakuacha rohoni na mwilini itadhihirika kwanza kabisa omba maombi ya kufunguliwa na mapepo ya kifamilia mapepo ya kichawi mapepo ya uzinzi manuizo mabaya zidi ya maisha yako maagano ya kifamilia yote unayakataa kwa jina la yesu ndoto za kuzimu hafu unamkataa kwa mamlaka uliyonayo kupitia jina.la yesu
Kweli kabisa ndugu ni mchanga kiroho, ila ndio naukulia wongofu.
Kuna wakati fulani nilifanya ibada ya kufunga na kuvunja yaliokua yanaziua kusonga mbele kiroho, na hili la huyu dada nilitubu kwaajili yake na yangu na kutengua ule uwepo wake rohoni mwangu lakin siku si nyingi nikamuota tena! Nimetafakari jibu sipati.
 
huenda uliwekeana nae magano ndomaana unatesa tengua hayo maagano atatoka rohon mwako
Ni kweli kabisa tuliahidiana kuishi kwa uaminifu na kipindi nilikua nae miaka 4 hakuna aliemkosea mwenzake japo kulikua na shida kwa wazazi lakini tulipendana mno ila ndio akawa wakwanza kuvunja ahadi, nilikubali matokeo maana nilishazidiwa ujanja isipokua roho kukubali kua sipo nae tena ndio ilikua shida kidog, baadae kidogo nimsahau japo hata kwa mwezi nanikuta nakumbushwa tena ndotoni
 
Niliwahi ku coment kwenye post moja kuhusu madhara ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu bila ya kuwa na ndoa,

kwenye miaka mitatu lazima kuna muunganiko wa kiroho, kama mwanamke alikuwa na maroho ya kwao na wewe utakuwa umeunganika nayo, cha muhimu tafura watumishi ufanye tengano la kiroho na huyo msichana.

Kama bado wampenda na yeye akupenda ni bora kukaa pamoja na kumaliza tofauti zenu na kuoana kabisa
 
Back
Top Bottom