Kuna uwezekano wa mtu ambaye si mwajiriwa kupata bima ya NHIF?

future mind

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
221
227
Wakuu eti kuna uwezekano wa individual wa kawaida ambaye si mwajiriwa kupata bima ya NHIF?
Na kama upo garama zake zikoje? Au hata kama kuna mfuko mwingine unaotoa huduma iyo naomba kujua,

Nawasilisha....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bima nyingine inaitwa TIKA(matibau kwa kadi) gharama yake mkubwa ni T shiring 10000 kwa mwaka na watoto ni shiringi 2000, hii ni Kwa jiji la mbeya kwingine cjui, kwa kadi hii unatibiwa kwenye vituo vya afya na hospital za serikali pekee, NHIF kwa mtu mmoja, mtu binafsi ni T shiringi 1,600,400 Kama sikosei, wanaojua zaidi watakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana, gharama yake kwa mwaka si chini ya millioni moja.
Kuna mifuko ya jamii mfano NSSF kwa wasio ajiriwa unapata bima ya matibabu kwa kuchangia elfu 20 kila mwezi. Baada ya miezi mitatu utatibiwa wewe na tegemezi wako.
 
Naweza kujiunga na bima za nssf bila kufanya malipo ya uzeeni?. Maana kwa sheria mpya sitaki kuweka akiba katika hifadhi za jamii kabisa!!.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa uelewa wangu sidhani kama hili linawezekana kwasababu primary purpose ya mfuko ni hifadhi ya jamii na siyo bima, na ndio maana kuna mifuko ambayo primary purpose yake ni hiyo bima ya afya. Hao nssf wali add hiyo product ya bima kipindi kile mifuko iko ming ili kuvutia wadau wapya! Tusubir wajuzi watujuze
 
Mkuu sure ni only one selected hospital?!? Na what if unafanya normal contribution ile ya kuajiriwa na unatibiwa kama kawa let say after some years uka quit job, utaendelea kutibiwa? Au ndo itakua imekomea hapo?
Inakoma iwapo tu NSSF haitapoke michango yako kwa miezi mitatu mfululizo. i.e. hata kama umeajiriwa na mwajiri wako hakupeleka michango kwa miezi mitatu mfululizo basi ndo imekula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nina bima ya afya binafsi ya NHIF.. nimelipia shillingi 1,501,200 kwa mwaka...
Inakoma iwapo tu NSSF haitapoke michango yako kwa miezi mitatu mfululizo. i.e. hata kama umeajiriwa na mwajiri wako hakupeleka michango kwa miezi mitatu mfululizo basi ndo imekula

Sent using Jamii Forums mobile app
Bima ya NSSF kasoro yake ni kuwa na huduma ya hospitali moja utakayotibiwa nchi nzima. Pia kwa maana hiyo sijui kama hata referal itahusika hapo. Sijua ni akina nani walitunga haya mawazo maana ukisafiri ukaugua, itabidi urudi kwenye hospitali uliyoandikisha kutibiwa!!!
 
Wakuu eti kuna uwezekano wa individual wa kawaida ambaye si mwajiriwa kupata bima ya NHIF?
Na kama upo garama zake zikoje? Au hata kama kuna mfuko mwingine unaotoa huduma iyo naomba kujua,

Nawasilisha....

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo, kuna namna mbili.

1. Kupata kadi ya mchangiaji, unaweza lipia 1,700,000/-, halafu unaingiza wategemezi wako watano. Hiyo ni kwa mwaka.

2. Unaweza jiunga kwenye kikundi cha ujasiria mali, ambapo mnakuwa na katiba, usajili n.k. Mkisha pata vitu hivyo, mnaomba kuanzia 10, kila mtu analipia 70,000/-, mnapata kadi ya mchangiaji, ukitaka kuwaongeza ndugu zako, unawalipia kila mtu 50,000/- kwa mwaka.

Vikundi vya bodaboda baadhi wamenufaika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bima nyingine inaitwa TIKA(matibau kwa kadi) gharama yake mkubwa ni T shiring 10000 kwa mwaka na watoto ni shiringi 2000, hii ni Kwa jiji la mbeya kwingine cjui, kwa kadi hii unatibiwa kwenye vituo vya afya na hospital za serikali pekee, NHIF kwa mtu mmoja, mtu binafsi ni T shiringi 1,600,400 Kama sikosei, wanaojua zaidi watakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ifafanue hii ndugu nami nipo Mbeya wanapatikana wapi hao TIKA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliuliza wiki iliyopita nikajibiwankuwa gharama ya mtu binafsi NHIF ni shilingi 1,501,200/= kwa mwaka. Na wanufaika ni:
1. Mwenza wako (mke au mume)
2. Watoto 2
3. Wazazi 2 (baba na mama). Mwaka ukiisha una renew.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom