Kuna uwezekano mkubwa Watanzania wengi tunatakatisha pesa na hatujui kama twatakatisha

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,014
8,363
Habar ya asubuh wanajamvi?

Niende kwenye lengo,la kuandika kaujumbe ka leo.

Baada ya kukamatwa kwa Dreva tax kwa kosa la kumteka Mo Dewji, na kosa la utakatishaji.

Nimejiuliza swali hivi ili neno utakatishaji ni nini maana yake?je ni watanzania wangapi tunajua maana ya utakatishaji fedha? Je kosa ili kisheria ni kosa gani?

Je kwa tafsiri yyte iwayo,hatuoni kama watanzania wengi tumeisha takatisha pesa paspo kujua?


Nmejiuliza swali ili na baada ya kujiuliza sana basi nilijarbu poa kupitia watu walio karbu yangu hakika wengi hawaelewi neno UTAKATISHAJI lina maana gani na kitendo cha utakatishaji kinafanywaje?

Katika mjadara wetu,tuliitimisha kwa kuomba kila mmoja wetu ajichunguze baada ya kujua ni nini mantiki yake,je yupi aliye salama?
Naomba ndgu zangu wenye uelewa mtuelimishe ili tuweze epuka kufanya makosa haya.

Maana sasa imekuwa very commoni,kila anae shitakiwa kwa kosa ili basi la itakatishaji nalo linaongezeka.
 
Pesa ikiyopatikana kimazabe kisha ukaaingiza Ktk mradi ama mzunguko halali mf biashara ama kununua asset km nyumba ama shamba!
 
Mtu yeyote anayefanya biashara ambayo ni haramu au anapata pesa kwa njia za panya lazima anafanya utakatishaji, mtu mwenye kipato halali anakuwaje mtakatishaji?
 
Ipo haja wabunge wetu kuwekea mipaka na ukomo sheria hii, Inakomoa watu, na kujenga mwanya wa rushwa kubwa. Polisi akiweka charge ya kutakatisha pesa huna dhamana katika kesi.Kuondoa hiyo charge ni mpaka maelekezo toka juu ama rushwa ya kueleweka.Hatua za awali hata judge ,mahakama hawana msaada. Matunda ya wabunge wa ndiooo.
 
Ukiwa na hela ambayo siyo halali yako mfano wizi, utapeli, rushwa, madawa ya kulevya. ujue umetakatisha pesa.
 
Back
Top Bottom