Kuna uwezekano mkubwa Waganga wakatajirika sana wakati huu kuelekea kumpata Mrithi wa Ruge Mutahaba CMG

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Yangu macho tu!

Kuna Watu kama nawaona vile kuanzia leo jinsi Safari zao za kwenda Bagamoyo, Tanga, Rukwa, Kigoma na Pemba ( Zanzibar ) kwa Waganga wa Kienyeji ili tu wawe ' Warithi ' rasmi wa Nafasi muhimu aliyoiacha Marehemu Ruge Mutahaba pale Clouds Media Group.

Nina Watu wangu Wawili hivi tokea Msiba ulipokuwa Dar es Salaam hadi jana kule Kagera kila nikiwaona katika Runinga ( Television ) sioni hata Nyuso za Huzuni ndani yao kama kwa Wafanyakazi wengine hadi nikawa najiuliza Maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Haiwezekana Wafanyakazi wote wawe wanasikitika halafu nyie Wawili tu msiwe hata na ule Huzuni wa Kinafiki ( Uwongo na Kweli )

Ningekuwa jirani na Bwana Joe Kusaga ningemshauri tu kwamba kwakuwa hata katika Mpira wa Miguu pale Mchezaji muhimu akifa / akifariki Jezi yake ' hustaafishwa ' daima na haitumiki tena basi ningemwomba kuwa hata na Cheo cha Marehemu Ruge Mutahaba na chenyewe asipewe Mtu mwingine yoyote na kibaki hivyo hivyo kama Alama Kuu na Kumbukumbu ya CMG kwa Wafanyakazi wajao na hata kwa Watanzania vile vile.

Waganga wa Kienyeji tafadhalini msichoke kututajia Majina ya Watu ambao watafuata ili muwafanyie Ndumba ( Miziziology ) ili Wateuliwe Wao kuwa ' Warithi ' wa Marehemu Jasiri Muongoza Njia Ruge Mutahaba ili tuwaumbue na pia mtakuwa mmetusaidia kuwajua mapema Watu ambao kumbe pengine hawajaumizwa na Kuondoka Kwake.

Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom