Kuna uwezekano maisha yako yote utakuwa mlalamikaji

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
1,335
1,386
Mimi na umri wangu mrefu huu nimegundua kitu.

Kuna jamaa zangu walikua wanamlalamikia sana Mkapa wakati ni Rais, alipoingia Kikwete walifurahi mno.

Miezi 4 baada ya Kikwete kuapishwa wakaanza kumlalamikia tena. Ikawa hivyo mpaka alipo maliza awamu zake, tena awamu ya pili ndio hali zao zilikua mbaya zaidi.

Alipoapishwa JPM walilalamika sana, baada ya wiki 3 wakaanza kumkubali. Miezi 6 ya JPM wakarudi kwenye kumlalamikia tena kama watangulizi wake. Ikawa hivyo mpaka alipofariki.

Alipoingia Samia wakawa na wasiwasi. Hawana uhakika na hisia zao. Wiki 2 baadae wakaanza kumkubali. Baada ya mwezi na nusu, Samia amekua mwiba tena kwao. Ni kulalamika mpaka basi.

Sasa kwa hesabu za haraka haraka, Tanzania Rais anahudumu miaka 10 kwa ridhaa ya wananchi. Mpaka sasa nimeshuhudia wakilalamika maraisi wanne kwa kipindi cha miaka 25.

Imebaki miaka 25 au 35 wafe, ambayo ni huduma ya maraisi 3 na nusu. Kwa kipindi hiki mpaka leo, wametumia nusu ya maisha yao kulalamika.

Tutafute furaha ndani ya mambo madogo madogo, tunapoteza mufa mwingi kuwa na huzuni.

Tusije tukafa tukiwa hatujaishi.
 
Back
Top Bottom