Kuna ushahidi wa kutosha kwamba waziri mkuu alibadilishiwa hotuba yake ya awali...

Mwakiluma

Senior Member
Jan 23, 2012
120
47
Kuna kila sababu ya kusema mh. Mizengo Pinda alibadilishiwa hotuba na boss wake...alipotua dodoma akitokea nchini brazil mheshimiwa rais hakuna cha maana alichokifanya kule dodoma zaidi ya kumwambia pinda abadilishe hotuba yake kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri kwani eti anadai ni upepo tu unapita...katika hotuba ya awali ya pinda ilitarajiwa pinda aseme "tayari tumepokea barua za mawaziri saba za kujiuzulu na kwa sababu ya uwajibika tayari tumeshawarusu kufanya hivyo"...sababu zinazotufanya tuamini kuwa PM alibadilishiwa hotuba yake ya awali ni kama ifuatavyo..


1. Katika hotuba ya jana Pinda alitumia muda mwingi kuongelea matokeo ya darasa la saba kitu ambacho hakikuwa kwenye ajenda zake kwani hata mwezi february angeliongelea hilo lakini hakufanya hivyo na kuifanya ipitwe na wakati

2.Alitumia muda mwingi kuongelea ziara yake ya kanda ya ziwa, ziara ambayo ni ya zamani sana hivyo imepitwa na wakati na hakuiweka kwenye ratiba yake ya awali.

3.Pinda sio mpenzi wa michezo lakini cha kushangaza katika hotuba ya jana alitumia muda wake mwingi kuwapongeza Simba kitu kilichowashngaza wengi.

4. Alipoongea na waandishi wa habari juzi alisema kwamba angeyaweka mambo yote hadharani jumatatu lakini cha kusikitisha aliyaficha mambo hayo.

5. Katika kutaka kujikosha kwa Chadema Pinda alitumia Muda wake mwingi kuwapongeza wabunge wawili wapya wa chadema kitu ambacho hakikutarajiwa...

6. Ilitarajiwa Pinda angetoa hotuba fupi sana kwani bunge lililopita lilikaa february hivyo ni kipindi cha muda mfupi lakini yeye alitumia maneno mengi ili kuwachosha watu na kupoteza ile hali waliyokuwa nayo...

Kwa vielelezo vyote hivyo hapo juu nimejiridhisha kwamba Waziri mkuu alibadilisha hotuba yake ya awali...
 
Hilo linawezekana hasa ukizingatia upumbavu wao wa kulinda chama chao badala ya masuala ya taifa. Naamini msukumo mkubwa uliofanya kujiuzulu kwa wale mawaziri kusikubaliwe ni kuilinda CCM dhidi ya mpasuko na si vinginevyo; kwao kujiuzulu kuna maafa makubwa kwa chama kuliko taifa.
 
Hata jana ukimwangalia Pinda machoni ni kama Nundu vile ili kwamba dhoruba ikipiga ndo aseme nilikatazwa na Jk
 
kwani uwaziri mkuu ni kama umafia wa sicily kusema ukiingia ni kama umetekwa huwezi kutoka!?pinda anavyoburuzwa na jk mpaka ni aibu kwa familia yake kuitwa baba!shameful
 
Ile hotuba ya Waziri Mkuu jana kama imefanikiwa kufanya chochote basi ni kuuthibitishia umma kwamba kati ya makosa watanzania waliwahi kuyafanya katika historia ni kumweka Kikwete madarakani kwa miaka mingi sana. Kumi?

Serikali ya sasa ni utani kwa kweli. Na haileti akilini kwamba solution ya hawa watu ni kujiuzulu watu fulani fulani. Walimtoa Lowassa wakamweka Pinda, nini kimebadilika? Walimtoa yule mhaya na Msabaha wakaweka wahuni fulani akina Ngereja na Malima, nini kimechange?

Solution ya haraka sana inayonijia kichwani ni kuwatoa Ikulu kwa mtutu hawa wahuni. 2015 ni mbali sana.
 
wanasema wakijiuzulu watawapa ushindi chadema kwani chadema wanaunda baraza la mawaziri? wizi uliofanyika ni kwa chadema autaifa kwa ujumla? wanakumbatia wizi wa serekali kwa kujidanganya na chama hakika hii awamu ya pili huyu jamaa haimalizi watu wanasira sana.
 
Mimi nilichonote ni kama kile cha Lowassa kabla ya kuingia bungeni, alikuja na mkewe na familia yake!.

Jana Pinda alitinga na mana Tunu na familia yake!.

Inapotokea wengi wetu tulikuwa na great expectations kuwa Pinda atazungumzia kuwajibika kwa mawaziri, kitendo cha kutozungumza lolote kuhusu hilo, then kwetu Pinda hajazungumza kitu.

Ila tukubali piga ua, Pinda hana makuu, is down to earth, humble na mtoto wa mkulima kweli!.
 
Pinda ni Shock absorber! Anakuwa humiliated kwa kuficha aibu ya JK ya kushindwa kuwasimamia mawaziri wake na serikali kwa ujumla!
 
hili linawezekana na amini angeweza kufanya vinginevyo lakini mwisho wa siku ni maisha ya mtu ni ya msingi zaidi. tukumbuke kuwa vilevile huyu mtu ni usalama wa taifa na anawajibu wa moja kwa moja wa kumtii rais wake.
lakin niliwaambia watu kuwa kikwete yuko tayari waziri mkuu apoteze uwaziri wake kuliko kukubali marafiki zake wapoteze uwaziri kirahisi! kwanza kuna kila dalili hawa watu huenda na wao wanafanya kazi kimkanda mkanda tu hawakubaliani kwa mambo mengi!lakini MUNGU yupo ipo siku
 
Mh. Pinda ni mtu mwenye busara sana, lakini nilivyo muona jana mimi nafikili kuna kitu - cha muhimu hapa tusubiri hotuba ya JK kwa WAZEE; mambo haya yalikuwa mazito sana na yakushtukiza tusianze kumlahumu PINDA.
 
hili linawezekana na amini angeweza kufanya vinginevyo lakini mwisho wa siku ni maisha ya mtu ni ya msingi zaidi. tukumbuke kuwa vilevile huyu mtu ni usalama wa taifa na anawajibu wa moja kwa moja wa kumtii rais wake.
lakin niliwaambia watu kuwa kikwete yuko tayari waziri mkuu apoteze uwaziri wake kuliko kukubali marafiki zake wapoteze uwaziri kirahisi! kwanza kuna kila dalili hawa watu huenda na wao wanafanya kazi kimkanda mkanda tu hawakubaliani kwa mambo mengi!lakini MUNGU yupo ipo siku

pinda anakubali kuonekana hafai ili kuficha siri ya mkubwa wake.
 
nadhani jana Spika aliposema wanaoafiki hoja ya kuarisha bunge, pale bunge CCM waliwazidi wapinzani , lakini aliposema wasioafiki waseme sio... wapinzaini kwa uchache wao walisaidiwa na watu wote tuliokuwa njee ya bunge na kusema sio....
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom