Mwakiluma
Senior Member
- Jan 23, 2012
- 120
- 47
Kuna kila sababu ya kusema mh. Mizengo Pinda alibadilishiwa hotuba na boss wake...alipotua dodoma akitokea nchini brazil mheshimiwa rais hakuna cha maana alichokifanya kule dodoma zaidi ya kumwambia pinda abadilishe hotuba yake kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri kwani eti anadai ni upepo tu unapita...katika hotuba ya awali ya pinda ilitarajiwa pinda aseme "tayari tumepokea barua za mawaziri saba za kujiuzulu na kwa sababu ya uwajibika tayari tumeshawarusu kufanya hivyo"...sababu zinazotufanya tuamini kuwa PM alibadilishiwa hotuba yake ya awali ni kama ifuatavyo..
1. Katika hotuba ya jana Pinda alitumia muda mwingi kuongelea matokeo ya darasa la saba kitu ambacho hakikuwa kwenye ajenda zake kwani hata mwezi february angeliongelea hilo lakini hakufanya hivyo na kuifanya ipitwe na wakati
2.Alitumia muda mwingi kuongelea ziara yake ya kanda ya ziwa, ziara ambayo ni ya zamani sana hivyo imepitwa na wakati na hakuiweka kwenye ratiba yake ya awali.
3.Pinda sio mpenzi wa michezo lakini cha kushangaza katika hotuba ya jana alitumia muda wake mwingi kuwapongeza Simba kitu kilichowashngaza wengi.
4. Alipoongea na waandishi wa habari juzi alisema kwamba angeyaweka mambo yote hadharani jumatatu lakini cha kusikitisha aliyaficha mambo hayo.
5. Katika kutaka kujikosha kwa Chadema Pinda alitumia Muda wake mwingi kuwapongeza wabunge wawili wapya wa chadema kitu ambacho hakikutarajiwa...
6. Ilitarajiwa Pinda angetoa hotuba fupi sana kwani bunge lililopita lilikaa february hivyo ni kipindi cha muda mfupi lakini yeye alitumia maneno mengi ili kuwachosha watu na kupoteza ile hali waliyokuwa nayo...
Kwa vielelezo vyote hivyo hapo juu nimejiridhisha kwamba Waziri mkuu alibadilisha hotuba yake ya awali...