Kuna usalama hapa? Maoni yako ni muhimu

Kwa sheria ya kiislamu hiyo hairuhusiwi nadhani hata kwa mafundisho ya kikristo pia hairuhusiwi kama wapo wajuzi watufahamishe.

Msichana na mvulana mzizoeana kwa karibu sana hata ladha ya ndoa hupungua sana na mara nyingi mara baada ya kufunga ndoa ndoa za aina hiyo huwa hazidumu sana.
Umenena vizuri Mkuu..Ahsante
Ni imani yangu kuwa wewe ni Kiongozi
 
Ukristo si ndio unagharibi wenyewe?
Ni lini hasi na Chanya zikigusana isitokee shoti???.

Mambo ya Boy na Girl friends ni utamaduni wa kimagharibi, utamaduni huo hautokani na misingi ya ukristo.

Yesu anasema; "Si imeandikwa usizini, amin nawaambia mtu akimtazama mwanamke na akamtamani atakuwa amezini---"

Sasa nikuulize inawezekanaje Boy na Girl friends wakae tu kama marafiki bila kutamaniana??!

Katika Qur'an imeandikwa; "wala msikaribie zinaa hakika hicho ni kitendo kichafu"

Hapo Qur'an ndiyo imefunga kazi kwa kusema Msikaribie zinaa sio msizini bali msikaribie yaani tuepuke njia zote zinazoweza kutupeleka katika zinaa.


Hakuna urafiki kati ya msichana na mvulani pakawepo na "usalama".
 
Ukristo si ndio unagharibi wenyewe?


Sio sawa kwamba Ukristo ni Umagharibi, mfano Mambo ya "girl and friend" yanapatikana hasa huko Magharibi na yanachochea sana zinaa miongoni mwa vijana lakini Yesu anasema katika moja ya Injili: "----- si imeandikwa kwamba usizini !!!, amini nawaambia mtu akimtazama mwanamke na kumtamani amekwisha zini".---- sasa utaona kwamba katika mahusiano ya "boy and girl friendship" ni matamanio ya kimwili ndiyo yanayotamalaki na hivyo ni zinaa ndiyo inayotamalaki jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya Bwana Yesu kwa msingi huo huwezisema kwamba Ukristo ni Umagharibi labda useme tamaduni za umagharibi zimeingizwa katika Ukristo kama jinsi upagani ulivyoingizwa katika ukristo, Soma kitabu; "Paganism in our Christianity".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom