Kuna umuhimu wowote wa kuwekwa viambata kabla ya majina ya wanasiasa?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,560
46,105
Kwa nini kwenye habari zetu au matukio mbalimbali kila mara tunapowataja viongozi au wanasiasa lazima tutangulize maneno ndugu, Mheshimwa, Komredi/kamaradi, kamanda, mzee n.k mbele ya majina yao?

Huu ni utamaduni, heshima, uungwana au mbwembwe zisizo na mantiki?
 
Ulivyosema Viambata nikajua ni viazi mbatata.

Mtaani kwetu wanaanza kwa kuniita 'mume wangu Ezekiel Mbaga'
 
Mimi naona bora ingekua Waheshimiwa Wananchi. Ingeleta maana Zaidi kuliko kuwaita hao wanasiasa ambao wengine hawastahili hata kidogo uheshimiwa kutokana na matendo yao
 
Kwa nini kwenye habari zetu au matukio mbalimbali kila mara tunapowataja viongozi au wanasiasa lazima tutangulize maneno ndugu, Mheshimwa, Komredi/kamaradi, kamanda, mzee n.k mbele ya majina yao?
Huu ni utamaduni, heshima, uungwana au mbwembwe zisizo na mantiki?
Ni ujinga na uzandiki, Nyerere na Mkapa waliitwa na kuwaita wengine ndugu, hawa wa sasa ni uchwara na hivyo viambata wanavitaka ili kuwaogofya wengine/deffensive mechanism kuficha udhaifu walionao, huwa najiuliza bila hivyo wanapungukiwa nini?
 
Hivi mtu kama Makala, Mwigulu, Muro, Happy and the like unawaheshimu kwa lipi?
Mkuu, hata kule mjengoni kuna baadhi ya wanaoitwa "Waheshimiwa" hawastahili hata kidogo. Neno Mheshimiwa limepoteza hadhi yake hasa linapotumiwa na wanasiasa
 
Back
Top Bottom