Kuna umuhimu wa usanifinishaji wa lugha moja ya kiswahili katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Ndugu wana JF bunge la Afrika Mashariki limeridhia matumizi ya lugha ya kiswahili katika Nchi wanachama changamoto ndogo ambayo lazima ifanyiwe kazi ni nchi wanachama kuongea matamshi tofauti ya lugha ya Kiswahili mfano Nchini Kenya " kujanga hapa, "Tanzania Njoo hapa".

Hivyo basi kuna haja ya aina moja tu ya kiswahili hivyo mamlaka za lugha ya kiswahili kwa nchi wanachama zikae na kukubaliana lugha ipi itumike yaani kiswahili cha Tanzania hivyo basi wataalaamu wa kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam na wataalmu wa BAKITA, BAKIZA na TUKI waanze kujinoa maana lugha yetu ni mali sana hata nje ya Afrika Mashariki mfano Shirika la utangazaji Uingereza BBC, Sauti ya Amerika Voa, idhaa ya kiswahili Japan.

Changamoto nyingine ni mitaala ya vyuo na shule na mahala pa kazi kwa nchi nyingine mimi ninaona Watanzania wenye sifa baada ya kuhakikiwa basi waanze kupitia maktaba zetu na historia ya lugha yetu ili kuondoa misimu katika lugha maana ndio tatizo katika kukua na kuenea kwa lugha ya kiswahili ,aidha vyombo vyetu na Wasanii waache kuchanganya maneno ya kiingereza katika mahojiano maana tutaonekana limbukeni wa nyumbani.

Aidha napenda kuunga mkono matumizi ya lugha yetu yanayofanywa na viongozi wakuu katika vikao na hafla mbalimbali za ndani na nje hasa anavyofanya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama vilevile Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh Dr John Pombe Joseph Magufuli
 
Vyombo vyetu vya habari na Wasanii wana mchango mkubwa sana wa kukuza lugha yetu nimerekibisha sehemu hapo juu kwenye post
 
Back
Top Bottom