Kuna umuhimu wa sheria za uchaguzi kubadilishwa.

Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
531
1,024
Wakuu Salaam.

Tangu kuanza kwa awamu ya tano kumekuwa na trend kubwa sana ya viongozi kuhama vyama kwa sababu mbalimbali, ingawa hata ktk awamu nyingine za uongozi hili limekuwa likijitokeza lkn naona kwa kipindi hiki limekuwa kubwa na kuna uwezekano likaendelea kwa wengi zaidi kuhama vyama hasa wachaguliwa wa wananchi kitu kinachopelekea kuwa na chaguzi mdogo ambao ni gharama kubwa sana, hasa ukizingatia sababu zinazowafanya watu hao kuhama ingawa na haki yao kikatiba lkn gharama zilizotumika ktk uchaguzi wa udiwani kata 43 na gharama zitakazo tumika katika uchaguzi wa ubunge kwa majimbo yaliyowazi hadi sasa, fedha hizo zingeweza kutumika kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.

Kama nitakiwa sijakosea kwa mujibu wa sheria zetu ni kuwa jimbo au kata ikiwa wazi ndani ya miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu basi uchaguzi mdogo hautafanyika ila hii bado haitoshi, tumetoka kushuhudia Zimbabwe Rais amejiuzulu chama kimeteua mbadala wa kumalizia muhula kazi inaendelea, nadhani ni wakati sasa wa sheria zetu kubadilishwa ili nafasi iliyopatikana iwe ni ya chama na kama ikitokea mtu aliyepeperusha bendera ya chama na kushinda akihama, akijiuzulu au akifariki au chama kikimfukuza, libaki kuwa ni jukumu la chama kutafuta mbadala na maisha yaendelee, maana hawa wanasiasa wanatuchanganya wanapokuwa wanatoa matamko ya kuhama wanatoa sababu zooote ila siwasikii wakigusia japo kidogo gharama zitakazoingiwa kuziba hiyo nafasi anayoiacha.

Waziri mwenye dhamana, chukua maoni haya uyafanyie kazi.

Asante.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom