Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alifanya ziara nchini India hivi karibuni na ziara hiyo imezaa matunda makubwa kwani mbali na kusaini mikataba mbalimbali yakibiashara na serikali ya India imeipatia Kenya mkopo wa dola milioni 100 yenye riba nafuu.
Ni wakati muafaka wa Rais Magufuli atafakari upya sera zake za kutosafiri kwenda nje kwani Tanzania kama taifa tunaonekana tunajitenga na jumuia ya kimataifa wakati sisi ndio tunawahitaji wao kwa maendeleo ya kibiashara na uwekezaji.
Nakumbuka wakati wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete alifanya ziara nyingi na tuliona Tanzania ikifaidika na mambo mengi ikiwa pamoja na uwekezaji.
Tanzania haiwezi kujitenga na jumuia ya kimataifa kwani Tanzania ilikuwa ni nchi siku zote upo mstari wa mbele katika ushirikiano na jumuia ya kimataifa ndio maana serikali za awamu zote zilizopita zilikuwa zikipata misaada ya haraka pindi inapotokea shida.