Kuna umuhimu wa kuweka sheria/utaratibu kudhibiti safari za viongozi na CAG akague eneo hili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna umuhimu wa kuweka sheria/utaratibu kudhibiti safari za viongozi na CAG akague eneo hili.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, May 9, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,951
  Likes Received: 37,485
  Trophy Points: 280
  Umefika wakati tuweke utaratibu kudhibiti safari za viongozi na hapa hasa raisi.Leo kaenda Ethiopia na majuzi alikuwa Brazil na Malawi.Safari hizi zinagharimu fedha nyingi za walipa kodi wa nchii hii na cha ajabu serikali hii inashindwa kuboresha maisha ya watu wake mfano wafanyakazi wanalipwa mishahara duni sana na sababu ufinyu wa bajeti.Cha kujiuliza huo ufinyu wa bajeti haugusi kabisa hizo safari?Na hivi ni lazima mara zote aende yeye?Mbona viongozi wa nchi nyingine huwa wanatuma wawakilishi tu?Huwezi kuwa unahudhuria kila tukio na siku zote wema usizidi uwezo.

  Ripoti ya CAG imeonyesha ufisadi wa kutisha na labda sasa ni wakati muafuaka kufanyia special auditing safari hizi huenda tukagundua mamilioni mengine yanayofujwa ingawa yanaweza kuhalalishwa na kigezo ni safari za muhimu.

  Mnapohubiri serikali haina hela basi viongozi muwe mfano ktk kubana matumizi ya serikali.Kumbukeni watoto wa maskini ambao kodi zao mnazifuja wanakaa chini,wanakosa huduma za afya,maji na wajawazito wanakufa kwa kutopata huduma za afya kisa hakuna vituo vya afya kwenye makazi yao.

  Inauma sana.
   
Loading...