Kuna umuhimu wa kuwa na wabunge zaidi ya 200?

NGUVUMOJA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,347
325
Huwa najiuliza kama ni muhimu kuwa na mamia ya "Waheshimiwa Wabunge" na utitiri wa Madiwani. Niliwahi kuambiwa "Hao ndio wawakilishi wetu wanaoikoromea Serikali ishughulikie matatizo yetu pamoja na kutuletea maendeleo"
Inamaana Serikali haiyaoni na hivyo haiyashughulikii hayo"matatizo" yetu mpaka iambiwe na "Waheshimiwa?"
Rais, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya yaani Serikali kwa ujumla wake si ndio kazi yake?
Nikilinganisha gharama ya kuwa na hao Waheshimiwa na manufaa ya kuwepo kwao, naona ni mzigo kwa nchi masikini kama hii yetu.
Kibaya na kinachoudhi zaidi ni kukuta wengi wa hao "Waheshimiwa" sio wachangiaji wa kweli kwenye hoja za msingi.
Nawasilisha.
 
We juilize hili
marekani ina watu wangapi na wabunge wangapi????
India ina watu wangapi na wabunge wangapi????????

Halafu linganisha na tanzania...
 
Kila wilaya iwe na mbunge mmoja kubana matumizi,walipwe mshahara tu hamna posho ya petroli sijui vikao wapewe landcruiser hardbody bei mil 35 na waendeshe wenyewe.
 
Back
Top Bottom