Kuna umuhimu wa kuendelea kuwaza mtoto hapa?

mind ur business

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
405
404
Ilikuwa mwaka Jana nilipokuwa nafanya kazi kwenye taasisi Fulani. Alikuja binti mmoja kuajiliwa Aneth (sio jina lake halisi), baada ya kuajiliwa ile taasisi ilikuwa na mambo ya hovyo Sana hasa kwa wanawake, sio mkuu, mkurugenzi, au Rafiq wa mkurugenzi. So nilianza kumwelekeza Nini Cha kufanya ili aepikane na uhayawani huo mwisho was siku tukajikuta tuko kwenye uhusiano.

Tulianza uhusiano sex mwezi wa nane tareh 30, ila kabla hatuja kutana nilimwambia naomba nijue tarehe zako ili tuepuke mimba. Jibu alilonipa Ni kuwa, MIMI CHUONI NILIKUWA NAFANYA HIVYO HIVYO TU. Dah, nikanyamaza tukaendelea na mchezo, nilimuomba tarehe mpaka Safari tatu, lakin jibu alilonipa Ni lilelie

Haya, nikamwambia ikitokea umepata mimba itakuwaje. Jibu, NYUMBANI HAWAWEZI KUNIFANYA LOLOTE. Nikaona isiwe shida acha tuendelee ku do tu. Sasa kweli nilikuwa na Nia nae ya kumuoa, na tulienda mpaka ilipofika mwezi wa kumi.

Kituko Cha Kwanza. Kutoa mimba. Hapa alianza Kila kukicha nataka nitoe hi mimba siwezi Lea mtoto, nikamwambia nilikuuliza mwanzo ukasema HAWAWEZI KUKUFANYA CHOCHOTE, vipi Tena. Akasema by any means I want to abort this pregnant. Nikamwambia ukitoa mimba kuna madhara makubwa yanaweza kukupata ikiwemo 1. Kufa. 2. Kuharibika kizazi. 3. Kuwa na vidonda visivyo pona. 4. Utawapa wazazi wako kazi ya kukutibia.

Akajibu. HATA NIKIFA FAMILIA YANGU HAIWEZI PATA SHIDA.

Duh, hapo ilibidi akili nyingi itumike, ilibidi NIBADILI UHUSIANO NIVAE VIATU VYA KUWA KAMA KAKA YAKE nikawa mshauri na kumridhisha tu kuwa nitakuletea dawa utoe.

Wakati huo nilikuwa nishaongea nae kuhusu kwenda kujitambulisha ili taratibu za kumuoa zifanyike. Kweli mwezi wa 12 nikaenda kujitambulisha, but hakuna alokuwa anajua kuwa ana mimba ya miezi 4. Basi bwana, utambulisho ukafanyika na Kila kitu Kika kaa SAWA.

Vitimbwi vinaanza.

Yule binti 28years akasahau kuwa mimi kazi yangu Ina mshahara mdogo tu by then 180' k kwa mwezi. Akawa anataka nimnunulie vitu vya gharama kubwa as if ana mashindano ya uvaaji, Mf. Niliambiwa ninunue dera, akawa anataka 160k' ya Madera tu, wakati huo alisema hawezi jifungulia hospital nyingine zaidi ya bugando.

Nilipoona Sasa haya sio mahusiano Bali Ni kupigana pesa nikawa nqmzingua, coz niliona kuwa hapo hakuna mke kabisaa. Ilifika hatua akaniambia she was to me just for money and not otherwise. Aisee nilijutia what I did, but sikujua that's a problem. Kweli nilijikaza tu hivyo hivyo ili maisha yaende. But, Kila tukikosana anashitaki kwa kaka yake so kaka mtu anaingilia ugomvi na kunituhumu mm ndio Nina makosa.

Yani Ni kuwa et..yule mdada akinitukana Mimi ninyamaze tu nisimjibu chochote hilo nilifanya mwanzoni kipindi najua kuwa she is my upcoming wife to be. Lakin nilipokuja just tabia yake aoohhhoo nikaona Ni ujinga kuvumilia ujinga. Basi, niliendelea hivyo hivyo na suala la kwenda kupanga mahali nikapiga chini cos she said herself that she is not after marriage but money.

Na, hapo she is a graduate student from udom 2019. Nilishangaa Sana graduate unaleta mambo ya kipuuzi kwenye mamboyamsingi. Muda was kujifungua ulifika, akaenda kujifungua bugando na nilijitahidi walaunikatoa pesa yote ya kukifungulia by then it was may. So akawa amejifungua.

Shida ikaja Tena, kuna nguo za mtoto ambazo nilikuwa nimemuandalia zilikuwa ximetumika kidogo na watoto wa sister na zingine baadhi tukanunua, akamtuma mtu akaja kuzichukua

Sijui alikuwa anawaza Nini hata sielewi (nilishangaa) anaanza kusema mtoto wangu hawezi kutumia nguo zilizotumika but anatakiwa atumie nguo mpya tu aisee nilichukia ila Basi nika kaa kimya.

Jina nalo nilikuwa nimeshaliandaa la kumpa mtoto, haa alipojifungua ikawa kesi Tena eti unatoaje jina hata mtoto hajazaliwa nikamuuliza kwani shida iko wapi hasa..et kutoa jina mapema ndio shida ikawa kesi Tena.

Basi bwana, nikaja kwenda kwao coz kuna sister ake aliniambia unatakiwa umuone mwanao. Nikampigia kumpa taarifa kuwa nakuja huko hakupokea cm nikaona isiwe shida mimi naamsha tu liwalo na liwe what matters is to see my kid ambae nilisimama Kama malaika coz angekufa Bado tumboni.

Kufika kwao, mzee anakuja anasema kwa kuwa nilimpa ujauzito Basi sio rahisi kumuona mtoto, Mimi Ni mtu flani najijua na najua kupuuzia (nikapuuza nikajisemea moyoni sio kesi) labda ningekuwa nimeua sawa.

Akasema ili nimuone mtoto inabidi mzee wangu aende wakapange pesa ya kulipia ndipo nitaruhusiwa kumuona. Shida ikaja sisi Mila zetu haziruhusu kulipia mtoto Kama Ni wangu. Nilirudi home nikamwambia mzee Kama mtoto Ni wangu sitaki uende kupanga pesa ya kumlipia, labda ningekuwa sijatoa pesa yoyte toka mwanzo ndio ukaamlipie.

Ikawa hivyo, tukaendelea na mawasiliano ya hivyo hivyo wakati huo Mimi hisia na yeye zilisha Isha mpaka moyo umebaki Kama chungu empty. Baada ya hayo mambo kuwa yameisha, tarehe 30.8.2021 akanitafuta kwa chokochoko zake sikutaka shida saana Bali kumuigizia tu ili akae kimya.

Siku hiyo, nilirudia kauli zangu kwake
1. UKUBALI KUWA NA MIMI AU UACHE YOTE SAWA.
2. HUYO MTOTO SIO LAZIMA SAANA TUMGOMBANIE CHA KUFANYA WEWE ISHI NAE TU, ILA KUMBUKA MWANZO ULITAKA KUMUUA AKIWA TUMBONI. KWA SASA JIVUNIE KUWA NAE.

Hapo kwa upande wangu ndio nilikuwa na finalize relationship. And in short Mimi nilikuwa nimesha apa siwezi oa huyo Dada. Ni mzigo Sana.

Siku moja akanitumia text...zinasema.
1. Ni Bora huyu mtoto aishi bila baba
(Nikamjibu ok)
2. Huyu mtoto hutamuona, hata kanyaga kwako Wala kwenu (kwa Bibi na Babu yake)
( Nikamjibu sawa)
3. Huyu mtoto hujawahi kumchangia chochote mpaka Sasa so unajivuna vipi kuwa Ni wako
(Nikamjibu ahsant)
4. Huyu mtoto atabaki kuwa wangu na itakuwa hivyo.
(Nikamjibu sawa)

Wakati anamitumia hizo txt zote nilikuwa namforwadia kaka ake ili aone Kama Ni kweli alichokuwa anaambiwa kuwa Mimi Ni mkorofi, nilitaka kuchezea maisha yake

Mbaya zaidi alimweleza mama yake kuwa Mimi nilitaka KUMUUA (Hapo nikakumbuka kuwa Ni kweli walioko gerezani sio wote wenye makosa) Nilianza kujiuliza huyu ndio mke nilitaka kumuoa??? Kweli....mhhh. Mbaya zaidi, baada ya kujifungua akawa akipigiwa simu na wazazi wangu hapokei, alafu nikipiga kumuuliza anasema et..apokee simu zao zitawasaidia Nini??

Ilibidi niwashirikishe wazazi wangu na kuwaeleza Mimi huyo mwanamke siwezi kuoa, na kuanzia mwaka Jana sijawasiliana nae mapka Sasa. Flashbacks, nilifuatilia kipindi Fulani simu yake no ikakuta kuna message amechati na wanaume I miss you n.k..

Sasa mpaka Sasa sijui huyo mtoto kweli Ni wangu au sio. Na Sina hata hamu ya kutaka kumjua Wala kurudiana nae. Akaekimya milele namm nikae kmya milele. Basi. Uzuri nilikuwa na mtoto ambae nilikuwa nimesha zaa na mdada mwingine kutokana na situation Fulani Fulani na kauli lakin mahusiano yalikuwepo na ilifikia hatua nikamsamehe kwa makosa tutaendeleza maisha.

Jamani ivi kweli hapo huyo Dada alikuwa na Nia ya kuolewa, au alikuja tu kwangu kupumzika kwa muda. Kwa kweli Mimi sioni haja ya kwenda kumlipia huyo mtoto. I'll aje kwangu au nimuone. Sidhani Kama nitakuwana makosa katika Hilo.

Je, kuna madhara yoyote Kama Nina mtoto nje, but mama watoto huyu hajui Kama nilisha zalisha litoto la watu huko mbali Sio mjuzi Sana wa kuandika, so wajuzi wa mambo mnaweza sema chochote hapa. Farewell single mother "Kim Aneth"

Povu na matusi sitaki.
By "mind your own business"
 

Sokulu Mkombe

Senior Member
Oct 31, 2018
108
139
Tulianza uhusiano sex mwezi wa nane tareh 30, ila kabla hatuja kutana nilimwambia naomba nijue tarehe zako ili tuepuke mimba,

Jibu alilonipa Ni kuwa, MIMI CHUONI NILIKUWA NAFANYA HIVYO HIVYO TU.
Mimi naona shida iko hapa ungejiongeza mapema kwamba hakuna mke hapa bt mungu ni mwema kma hukupata maambukizi, ungesimama kama mwanaume na sio kimvulanavulana kama ulivyofanya.
Ukivumilia mahusiano ya kipuuzi tegemea kuwa na ndoa ya kipuuzi pia, tabia ni kama ngozi kupotea hadi uchune.

☆Damu haipotei kma mtoto ni wako atakutafuta tu tuliza mori mungu ni wetu sote
 

mind ur business

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
405
404
Makosaaa akapigwaa makagare

Mkuu umeteseka sana

Kunyaa maji upate na upepo wa bahari

Ayiiiii bia tamu
Shukrani..yule binti kwakweli ilibidi niishie kutoa kishika uchumba, nguo za wazazi wake Basi.

Mola atanilipia kwa yaliyotokea
 

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,932
7,238
Komaa na life mwanangu kama damu yako.atakuja japo anaweza kuja afu tabia walizomlea zikawa mbaya.
 

mind ur business

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
405
404
Mimi naona shida iko hapa ungejiongeza mapema kwamba hakuna mke hapa bt mungu ni mwema kma hukupata maambukizi, ungesimama kama mwanaume na sio kimvulanavulana kama ulivyofanya.
Ukivumilia mahusiano ya kipuuzi tegemea kuwa na ndoa ya kipuuzi pia, tabia ni kama ngozi kupotea hadi uchune.

☆Damu haipotei kma mtoto ni wako atakutafuta tu tuliza mori mungu ni wetu sote
Shukrani kwa mawazo yako mazuri..mkuu
 

Bangida

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
1,476
5,593
Mkuu we muache nae. Kuna msela wangu alipata the same issue, tena na matusi juu. Mpka kujitambulisha alienda, alipofika hawakumfungulia hata mlango akaishia nje. Mwisho wa siku akachora. Baby mama akawa anajisifu kua ye anaeza kulea asibabaishwe n.k. hata miez 6 haijapita simu nyingi kwangu, ooh shemeji ongea na mwenzako, watoto wanahitaji matunzo na mambo meeengi. Nkamwambia mcheki mwamba. Mwamba kakaza uzi kua hatoi hata senti. Imebidi mimi nkwepe msala. Kila siku akipiga sim hua naishia kumwambia kua mimi ni rafiki tu mambo ya familia siez ingiliA.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Top Bottom