mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Mtu anachangia 30% ya mshahara wake kama kodi. Zingine anawakopesha ziingie mfuko wa jamii. Anachangia mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na tozo ya maendeleo ya ujuzi (SDL). Kama haitoshi, anachangia REA ya umeme vijijini kupitia LUKU na tozo ya mshikamano ya miamala ya simu
Huyu mtu anaambiwa ajifunze kuwa mzalendo kidogo aache ubinafsi maana hospitali, barabara na umeme vijijini vinahitajika. Hapo anachangia misiba, kuuguza na elimu kwenye jamii yake.Uzalendo kwenye nchi ngumu ni changamoto. Unaweza kutoa roho yako na bado ukaombwa uongeze uzalendo!
Kuna umuhimu wa kuelimishana maana halisi ya haya maneno:
1. Uzalendo
2. Ubeberu
3. Unyonge
4. Vita ya kiuchumi
5. Maendeleo