Kuna Umuhimu wa Kuchagua Mtu Badala ya Chama Kwenye Chaguzi Zetu?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
CCM inahimiza mara kwa mara wapiga kura kuchagua Chama badala ya Mtu! Je, hoja hii wapendwa wanaJF mnaionaje? Japokuwa mtu hafungwi kuchagua chama fulani lakini mimi naona msisitizo huu wa kuchagua Chama umefikia mahali pa watu kusema kwamba Chama fulani hata kikiweka jiwe litachaguliwa tu, hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu! Pia naona kwamba ugombea binafsi uruhusiwe (of course niko aware na rufaa ya Serikali dhidi ya hukumu ya mahakama Kuu juu ya suala la mgombea binafsi)! Tujadili!
 
Wadau nilifikiri kutakuwa na wachangiaji kadha wa kadha kwenye mada hii lakini naona kimya!
 
unampigia mbuzi guitar?hahhaha!
nadhani kutakuwa kulishakuwa na hii discussion huko nyuma! But anyway...Chama kinabaki kuwa kivuli chenye nguvu sana Tz. By kivuli i mean, a major unregulated political player. Chama ndo kinachotoa wagombea, lakini hata katiba haitambui Vyama vya siasi! Ivi Kikwete akirudisha kadi ya chama, hali itakuwaje? Ni sawa na Obama arudishe kadi ya chama chake! I guess we have to look at the law in depth to get this answer.
 
Mara zote wapiga kura huchagua mtu na wala sio chama.

Chama chochote kinaweza kuwaomba wapiga kura wachague chama badala ya mtu. Kwa kuzingatia, hilo haliwezekani, na likiwezekana litakuwa ni kwa kuzingatia propaganda iliyofanywa tu. Sababu ni kama zifuatazo:
1. Wagombea wote ni watu na si vyama. Vyama huteua wagombea tu
2. Kampeni zote hufanywa na watu/wakijinadi uwezo wao na kutoa ahadi za kutimiza matarajio ya wapiga kura wao. Hutumia sera za vyama vyao ili kufanikisha malengo yao
3. Mshindi wa uchaguzi ni mtu. Mshindi hutangazwa dhidi ya walioshindana nae na mtangazaji ni Tume ya Taifa ya uchaguzi
4. Viapo vyote baada ya ushindi ufanywa na watu na wala sio vyama. Hakuna kiongozi wa chama anaesimamishwa ili kula kiapo kutokana na ushindi wa mwanachama wake
5. Uwakilishi wa mshindi (Diwani, Mbunge, n.k) hufanywa na mtu kwa kuzingatia vipaumbele vya watu ambao mtu huyo anawawakilisha. Hakuna chama kinachowakilisha watu
6. Chama kinafaidika kwa kupata support kutokana na ushindi wa mtu katika mabaraza ambayo mtu huyo amechaguliwa kuwa mjumbe (Council, Bunge, Baraza la Mapinduzi ZNZ).
 
Back
Top Bottom