Kuna umuhimu wa kidato cha tano na sita?

scientist 08

Member
Aug 8, 2017
66
125
Kwa kutumia mfano wa nchi kama Kenya wao wanaishia kidato cha nne na wanaingia vyuo vikuu na vyuo vya kawaida huku content zao karibia ni kama za kwetu na miaka ya vyuo vikuu ni kama yetu.

Kwa mfano aneyesoma uhandisi atasoma miaka 4 kama sisi je kwanini sisi tukawa na kidato cha tano na sita?

Anaeweza kuwa na faida ya huuu mfumo wa 7-4-2-4 na hasara za huu wa 8-4-4 unaotumiwa na kenya asaidie hapa
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,060
2,000
Zambia nao wana system hiyo, masomo yanayohitajika kufuatilia degree fulani yanakuwa covered chuo kikuu.

Hivyo huongeza muda wa kukaa chuo lakini huwezesha vijana wengi zaidi kwenda chuo (mchujo mmoja tu wa form 4) na baada ya mwaka au mwaka na nusu huwa wako vizuri tu.

Vitu ambavyo havihitajiki kwa degree unaviacha na kufocus kwa yale yanayohitajika.
 

Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,140
2,000
Mm kusema ukweli inanisokota kuona kna a-level tz wkat nchi kibao hazina na tunashirikiana nazo kama Kenya nk.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,997
2,000
mkuu a level ni muhimu inapanua knowlege ya mtu sana we angalia tu mtu wa f6 to chuo anakuwa na uelewa mpana tofauti na wa f4 then diploma to chuo
exactly! Kuna gap kubwa kati ya f4 na f6! Kunakuwa na knowledge leap! Mfano hesabu ukienda A level unasoma vitabu say Beckhouse 1 and 2.

Unaona kuna gap kubwa na vitabu vya O level... hivyo hivyo kwenye Biology... Plant and animal biology, gap kubwa na vitabu vya f4 etc.

Ukitoka form 6 university education inaungika vizuri.. ie continuation ni smooth
 

urumrawi

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,492
2,000
exactly! Kuna gap kubwa kati ya f4 na f6! Kunakuwa na knowledge leap! Mfano hesabu ukienda A levle unasoma vitabu say Beckhouse 1 and 2. Unaona kuna gap kubwa na vitabu vya O level... hivyo hivyo kwenye Biology... Plant and animal biology, gap kubwa na vitabu vya f4 etc
Asante kwa kumuelimisha. Elimu inajengwa kama kata vile au V na mtu ambaye hapiti 5 na 6 amepungukiwa kitu kikubwa katika elimu yake. Hakuna shortcut katika elimu.
 

Jick

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
743
1,000
Mada hii inahitaji mtu awe very technical and knowledgeable kuhusu mifumo ya Elimu, sio kama baadhi ya wadau waliochangia awali.

Mleta mada kwa haraka haraka kumbuka Kenya wanasoma mpaka darasa la 8 huku sisi tunaishia la 7, Chuo kikuu minimum duration kwa Kenya ni 4years, sisi ni 3years

Kwa mtaala mpya uliopo sasa Tanzania kuanzia mwaka 2020 tutaanza kuishia darasa la sita kisha Form One mpaka Form Four. Kuanzia darasa la kwanza mpaka Form Four itatambulika kama Elimu Msingi (Basic Education).

Yote haya ni wachache tunaoweza kuona faida na hasara zake. Elimu zaidi inahitajika kwa umma ili kuelewa Faida ya mfumo wa Elimu.

Tatizo letu Watanzania kuna mambo ambayo hatufuatilii na hatuna muda nayo, mojawapo ni kuhusu masuala ya Elimu, wengi wetu huwa tunatahamaki na kuanza kulalamika mabadiliko yakianza kutekelezwa.
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,332
2,000
Baada ya mzigo wa masomo mengi ya O level, unachukua masomo matatu ya kujipima kama unaweza kuingia chuo kikuu.

Kwanza utaongeza upeo wa kufikiri kama mtu mzima. Wenye fujo chuoni ni hawa wanaoingia wakiwa wadogo. Jibu ni kwamba "mfumo unasaidia sana "
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,464
2,000
Yes mada nzuri nami nimechungulia mfumo wa Namibia wao wanaanza grade 1 to grade 7(primary school),then grade 8 to grade 12(matrix) as a high school,and u sit for your final exams on grade 12 and if u pass its straight to university and normally their first degree it take 3yrs but kama uliingia chuo kikuu na alama ambazo sio bora inakuchukua 4yrs kusomea shahada ya kwanza,mimi nimeupenda mfumo huu hasa mwanafunzi anapokuwa High school anajifunza mno kwa vitendo sio kukariri vitabu kama kwetu.
 

Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,140
2,000
yes mada nzuri nami nimechungulia mfumo wa Namibia wao wanaanza grade 1 to grade 7(primary school),then grade 8 to grade 12(matrix) as a high school,and u sit for your final exams on grade 12 and if u pass its straight to university and normally their first degree it take 3yrs but kama uliingia chuo kikuu na alama ambazo sio bora inakuchukua 4yrs kusomea shahada ya kwanza,mimi nimeupenda mfumo huu hasa mwanafunzi anapokuwa High school anajifunza mno kwa vitendo sio kukariri vitabu kama kwetu.
Hii kukariri sana ndio inachosha Tanzania.... Yaani unasoma mpaka unabirukia matokeo zoro.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom