Kuna umuhimu mkubwa wa Tanzania kuwa na tume huru ya uchaguzi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
hizi ahadi za abunuwas hazituhakikishii chochote toka kwenye waliojaa uchu wa madaraka

Hatutafanya kosa la Kenya-Lowassa
Hassan Simba, Mtwara
HabariLeo; Tuesday,January 15, 2008 @00:02

SERIKALI imesema imepata somo kutokana na vurugu za kisiasa zilizotokea Kenya na kwamba ipo makini kuhakikisha kasoro zilizosababisha hali hiyo hazipewi nafasi nchini katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika uzinduzi wa maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, uliofanyika katika viwanja wa soko kuu la mjini Mtwara.

Lowassa alisema serikali imejifunza vya kutosha kutokana na machafuko ya kisiasa yanayotokea nchini Kenya na kusababisha watu zaidi ya 600 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa, kuharibiwa mali na kuyakimbia makazi yao, kwa kuhakikisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyika kwa umakini mkubwa.

"Tumepata somo kutokana na vurugu za kisiasa za Kenya baada ya uchaguzi wao uliofanyika Desemba 27 mwaka jana……na hii ni kukosekana kwa umakini ndiko kulikosababisha machafuko yale. Natoa wito kwa Tume ya Uchaguzi kuwa makini katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa, hali kadhalika kwa wananchi mnapaswa kuwa makini kwa kujitokeza na kujiandikisha," alisema Lowassa.

Alisema serikali ina imani kubwa na Tume kuwa italisimamia zoezi hilo kwa umakini ili kuepusha uwezekano wa kutokea kwa malalamiko yatakayoweza kuleta vurugu za kisiasa wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao na kwamba imani hiyo inatokana na Tume hiyo kusimamia vyema Uchaguzi Mkuu uliopita.

"Ni umakini wa Tume yetu uliyotuwezesha uchaguzi uliopita kuwa huru na wa haki na ambao uliwaridhisha wadau wote vikiwamo vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi ule, naipongeza Tume kwa umakini huo, pia kwa maandalizi mazuri ya maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura," alisema Lowassa huku akiwainua makamishina wote wa Tume hiyo ambao wamekuwapo mjini hapa kwa zaidi ya siku tano.

Aidha, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa tume katika kipindi hicho cha maboresho kwa kuwahimiza wananchi wajitokeze kujiandikisha na kufanya marekebisho katika daftari hilo.

Alisema ni jukumu la vyama vya siasa kuweka mawakala katika vituo vya uandikishaji ili kujiridhisha na kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa malalamiko baada ya uchaguzi, jambo ambalo alisema linaweza kuepukwa iwapo viongozi wa vyama hivyo watatoa ushirikiano wa kutosha katika kipindi hiki muhimu.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi huyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Jaji mstaafu Lewis Makame, alisema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kwamba baada ya maboresho hayo yatafanyika tena kati ya 2009, 2010 kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Jaji Makame alisema zaidi ya watu milioni tano wanatarajiwa kuandikishwa katika kipindi hiki cha uboreshaji ambao umeanza jana katika mikoa ya Kanda ya Kusini ya Lindi na Mtwara na baadaye kuendelea katika kanda nyingine sita na kukamilika ifikapo Oktoba mwaka huu. Alisema uboreshaji huo utafanyika kwa siku sita kuanzia jana hadi Januari 19, mwaka huu, hivyo aliwataka wananchi wa mikoa hiyo wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na wale wenye taarifa ya watu waliofariki na waliojiandikisha katika daftari hilo watoe taarifa ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa umakini.

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
Lowasa na JK watakubali Tume kuwa ya Huru kabisa na kuwa na wapinzani kule juu ? Hili ndilo tatizo kwamba Rais ana madaraka makubwa sana na anateua anavyo taka . Hope wamepata somo kweli isije ikawa sasa wanajikta kupanga mkakati mkali zaidi wa wivi wa kura .
 
Lowasa na JK watakubali Tume kuwa ya Huru kabisa na kuwa na wapinzani kule juu ? Hili ndilo tatizo kwamba Rais ana madaraka makubwa sana na anateua anavyo taka . Hope wamepata somo kweli isije ikawa sasa wanajikta kupanga mkakati mkali zaidi wa wivi wa kura .

Kama alivyosema Mch. Kakobe kuwa watanzania ni wanafiki. Hakika alichojifunza EL ni kuwa kuiba kura kunaitaji ufundi na hapa kwenye daftari ya kupiga kura lazima watafanya manjonjo. Kwani CCM ni chama? Siku zote hawana uwakika wa kushinda uchaguzi mpaka watumiye waalimu kuvujisha uchaguzi. Viongozi wa vyama vya upinzani lazima washiriki kikamilifu wakati huu wa uandikishaji na pia kudai tume huru na katiba mpya ya Tanzania.
 
Hawa mafisadi wa CCM kwa kung'ang'ania kuendelea kuwepo madarakani na kufanya njama ili ionekane wameshinda chaguzi wanaweza kabisa kusababisha yaliyotokea Kenya kutokea Tannzania (Mungu apishilie mbali) lakini ukweli ni kwamba hawa wanaojiita viongozi wa sirikali hawawatakii mema Watanzania na Tanzania yetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom