Kuna umuhimu jaman,i wa ........................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna umuhimu jaman,i wa ...........................

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngo, Feb 16, 2011.

 1. N

  Ngo JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  Ni kitu cha kawaida kwa mzazi kumkumbushia mtoto/kijana wake kuhusu suala la mapenzi na mihemuko inayowapata vijana katika umri wa kubarehe au niseme katika level ya sekondari na kurudi chini. Hata vyuoni pia wazazi wanakumbushia vijana kuwa makini katika ulimwengu wa sasa uliojaa vishawishi vya kila namna na athari ya magonjwa yaliyopo. Kwa upande mwingine kwa watu wengi walioko kwenye ndoa suala la kukumbushana hili jambo la kila partner kuwa makini linachukuliwa kuwa ni jambo linalojulikana tunakuwa na assumption kuwa wenzi wetu wako makini hawahitaji kukumbushiwa. Mwisho wake ndo tunaona watu walioowa au kuolewa bado wanazidi kutembea nje ya ndoa zao kama vile hawako katika ndoa. Mifano mingi kuhusu hili inaonekana mitaani na hata huko makazini.

  Kwa upande wangu naonelea, na huwa tunakumbusha na mwenzi wangu kuwa makini kwa kuchukua taadhari zote zinazowezekana katika kulinda, kuimalisha na kuboresha uhusiano wetu wa mapenzi. Na hili kwangu mimi linafanya kazi maana huwa tunaongea kinagaubaga athari ya mmoja wetu kuwa na mausiano mengine pembeni na faida ya kuwa waaminifu. Imefikia maali wengine wanaamua kula viapo tena kwa kwenda kwa mchungaji kukumbushia. Wana JF watu waendelee ku-assume ‘’ukiwa kwenye mausiano unajua athari ya kutoka nje ya ndoa bila kukumbushana?’ Hasa kwa wanandoa.
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kuna haja ya kuzungumza kuboresha mahusiano,lakini uamuzi wa mwisho atoke nje ya ndoa na athari zake ni wa mtu binafsi kutegemeana na sababu zake za kutoka nje ya ndoa......sidhani kama wanaotoka nje ya ndoa hawajui athari zake au kwamba hawajakumbushwa.......
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kukumbushana muhimu ingawa sikio la kufa halisikii dawa.
   
 4. N

  Ngo JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Husninyo;1630266]Kukumbushana muhimu ingawa sikio la kufa halisikii dawa.

  Wa hivyo akija kuomba msamaa asamehewe au ndo kuachana moja kwa moja? Ni kiwa na maana kila mara mnajadili umuhimu wa kuwa waaminifu kwa kila mmoja.
   
Loading...