Kuna umuhimu gani wa kuulizana makabila wakati wa kupatiwa huduma za Umma?

Hizo tunaziita demographic data, zinasaidia kujua ethnicity ya mtu na mtu.

Mfano, hospitali huwa kuna umuhimu wa kujua dini ya kila client ili kujua utatumia approach ipi kumuhudumia. Pia kuna dini haziruhusu baadhi ya tiba, mfano wale dhehebu la Jehovah Witness huwa hawaruhusu kuongezewa damu.

Hizi ni standards ambazo zinatumika duniani kote, kwa hiyo hamna tatizo lolote sema Watanzania siku hizi tunajistukia kwa kila kitu, hata vitu vidogo kama hivi ambavyo tangu enzi na enzi vinafanyika hivyo lkn leo hii tunavishangaa sijui kwanini.
Lakini mtoa mada kauliza kada ya mahakama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wangu ukiwauliza kabila utawaonea bure. Mimi wazazi wangu ni mchanganyiko wa makabila mawili madogo moja la huko Serengeti (baba) na mama kabila dogo lililoko mwambao wa Ziwa Nyasa. Mke wangu pia mchanganyiko wa mngoni na mzigua. Watoto wangu kabia gani? Hii kuulizana kabila ni ushamba tu wa kuendekeza ubaguzi. Kabila linasaidia nini katika tiba? Kabila linahusikaje kwenye uhalifu?
Ubaguzi tu.
Kabila la baba yako na lako ndilo kabila la watoto wako..ingawa ni upuuzi kuulizana makabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mtu anajua, ni Muzungu aliacha hivyo kama yalivyo mambo mengi kama pf 3, Uchifu kama akina Mbowe, marufuku kuita mtoto wako jina la Kibantu ni lazima aitwe John, Julius, Richard au sijui George n.k. lkn nafikiri lengo lilikuwa ni kukusanya takwimu ili kurahisisha kuwaganya na kuwatawala watu!
 
Shida hapa ni kwamba nyaraka nyingi zinazotumika ni za tangia awamu ya Nyerere ni mwendelezo wa Ku - copy na ku- paste. Nimeliona hili hata kwenye usajili wa wanafunzi kuanza elimu ya msingi kuna kipengere cha kujaza kabila.

Kwa sasa sioni kama kuna umuhimu huo maana hatuna "Genetic Tribe", tuna "Linguistic Tribe" Jamii zimeoleana sana hivyo tabia na mienendo kwa kabila halisi zimebadirika kutokana na miingiliano hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mtu anajua, ni Muzungu aliacha hivyo kama yalivyo mambo mengi kama pf 3, Uchifu kama akina Mbowe, marufuku kuita mtoto wako jina la Kibantu ni lazima aitwe John, Julius, Richard au sijui George n.k. lkn nafikiri lengo lilikuwa ni kukusanya takwimu ili kurahisisha kuwaganya na kuwatawala watu!

Tembeeni kidogo duniani muone mambo yanafanyika vipi, ukishindwa kabisa soma vitabu, and google can be your friend too.
 
Tembeeni kidogo duniani muone mambo yanafanyika vipi, ukishindwa kabisa soma vitabu, and google can be your friend too.

Ni wapi Dunia hii wanatumia ,,Kabila” ukiondoa Afrika na watu wa misutuni huko Amazon?
 
Ni wapi Dunia hii wanatumia ,,Kabila” ukiondoa Afrika na watu wa misutuni huko Amazon?

Ethnicity background ni similar to makabila sababu wao hawana makabila.

Kilichoongezekaa miaka ya leo ni kwamba sasa ni optional kujaza. Haimaanishi huna ethnicity background ila hutaki kudisclose wengi kwa kuhofia ubaguzi.
 
Back
Top Bottom