Kuna umuhimu gani Tanzania na waganga wa kienyeji?

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
Karibu watanzania wenzangu tujadili swala la waganga wa jadi kuwepo kwao Na madhara ya kutokuwepo kwao.

Lengo kuu la Uzi huu ni kusoma nyakati kwa nini Tanzania kama ikafuta Na kupiga marufuku shughuli zote za kiganga nchi nzima!

Kuna madhara mengi zaidi yanayofanywa Na uwepo wa waganga wa jadi, ikiwa pamoja Na kusababisha mauwaji mbalimbali mara ya watoto, mara ya wanawake, mara wanaume wenye vipara, mara wanawake wenye ndefu, mara albino nk

Mimi napendekeza nchi yetu ipige stop shughuli zote za waganga wa jadi tukabaki shughuli za kidini tu kwa maana ya tiba za kiroho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kweli umevurugwa. Unajua watu wangapi wanazaliwa au kupona na kusaidiwa matatizo yao na waganga wa kienyeji?. Kwa taarifa yako, wanawake na wanaume wengi hutumia dawa zao katika uzazi. Kuna magonjwa sugu mengi yaliyoshindikana hospital hutibiwa kwao. Huwezi kutumia vivo vya watu 10 kwa nchi nzima kwa mwaka kama sababu ya kufuta waganga wanaosaidia watu zaidi 1000 kwa siku, mpaka ninapopost hapa kuna watu wapo kwenye matibabu. Yaani ni sawa na kuzuia safari za ndege kisa ajali.

Kama wewe unaimani ya kiroho ni wewe, kuna mamilioni ya watanzania hawana imani kama yako.

Siku nyingine uangalie na kupima faida na hasara ya hapo kabla ya kutoa ushauri, na usitazame mambo kwa kufungamanisha na Imani yako. Wanatambulika kama watoa tiba mbadala au tiba asili sio waganga wa kienyeji kama uwaitavyo.

Karibu watanzania wenzangu tujadili swala la waganga wa jadi kuwepo kwao Na madhara ya kutokuwepo kwao.
Lengo kuu la Uzi huu ni kusoma nyakati kwa nini Tanzania kama ikafuta Na kupiga marufuku shughuli zote za kiganga nchi nzima!
Kuna madhara mengi zaidi yanayofanywa Na uwepo wa waganga wa jadi, ikiwa pamoja Na kusababisha mauwaji mbalimbali mara ya watoto, mara ya wanawake, mara wanaume wenye vipara, mara wanawake wenye ndefu, mara albino nk
Mimi napendekeza nchi yetu ipige stop shughuli zote za waganga wa jadi tukabaki shughuli za kidini tu kwa maana ya tiba za kiroho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waganga waneokoa roho nyingi sana , wafutwe kwa misingi gani ? Doctor anaweza kutumia vipimo vyote asione kitu ila mganga wa kienyeji anaona . Unasemaje !!!! Wacha hizo !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom