Kuna umuhimu gani au lengo kuu la kuwa na uwongozi wa Serikali ya Wanafunzi vyuoni inayoundwa na viongozi walioko chini ya mwamvuli wa chama

Dismas Mmasi

Member
Nov 28, 2020
13
45
Kuna umuhimu gani au lengo kuu la kuwa na uwongozi wa serikali ya wanafunzi vyuoni inayoundwa na viongozi walioko chini ya mwamvuli wa chama cha kisiasi ni lipi /gani?
 

Chief Editor

JF-Expert Member
Feb 18, 2019
775
1,000
Umenikumbusha kipindi ambacho tulikuwa tunazifungia cafeteria kwa sababu tu zimepandisha bei ya chai kutoka mia moja hadi mia mbili ....lazima meneja atoe sababu kama ni sukari imepanda bei au la !!!!
Hapo unalinda waliokupigia kura
 

Dismas Mmasi

Member
Nov 28, 2020
13
45
Vijana wanalenga teuzi
Naamini katika misingi ya kawaida unapoenda kumteuwa mtuu inahitaji uwe unamjua na ili kumjua mtu lazima uwekaribu nae ili uweze kumchunguza, huoni itakuwa ni ngumu kulamba teuzi maana kuna baadhi ya vijana hujiunga na chama kwaajili yakufanikisha lengo la kuwa na uwongozi chuoni
 

Chief Editor

JF-Expert Member
Feb 18, 2019
775
1,000
Katiba ya nchi inaruhusu raia kuwa na chama cha siasa lakini vyuoni hutakiwi kutumia chama chochote cha siasa kama sehemu ya kampeni kupata uongozi ndani ya chuo. Pia hakuna katazo lolote lile juu ya kuwa kiongozi wa chama siasa na chuoni kwa pamoja.

Lengo.

Kwa vyama vya siasa. Kupata viongozi wenye uzoefu wa kuongoza. Ndio maana tuna viongozi wengi kwenye vyama vya siasa. Mifano Silinde D, makonda na samwel sitta
Pia kuandaa wasomi wenye mrengo sawa na vyama vyao kiuongozi.
Ni sehemu ya kukuza propaganda zao.
Ni sehemu ya kukuza idadi ya wanachama.

Kwa wanafunzi ambao ndio viongozi wenyewe. Kwanza tuelewe haulazimiki kuwa na chama cha siasa ili uwe kiongozi wanafunzi.
Malengo ya wanafunzi viongozi kuwa na vyama vya siasa.
Kujiandaa kuwa viongozi baada ya chuo. Ioumbukwe ni ngumu kuwa mwanafunzi na viongozi wengi kijamii hutokana vyama vya siasa.

Mengine watajazia wadau
 

Dismas Mmasi

Member
Nov 28, 2020
13
45
Umenikumbusha kipindi ambacho tulikuwa tunazifungia cafeteria kwa sababu tu zimepandisha bei ya chai kutoka mia moja hadi mia mbili ....lazima meneja atoe sababu kama ni sukari imepanda bei au la !!!!
Hapo unalinda waliokupigia kura
mlifanikiwa kuzifungia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom