Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,974
13,606
Tunasoma katika bibilia kuwa wana wa israel walichukua muda wa miaka 40 kufika nchi ya ahadi wakitokea utumwani misri. Hapa najiuliza sana. Miaka 40 kutoka hapo kairo kwenda yerusalemu?

Mbona ni miaka mingi sana? Au walikuwa hawajui njia? Mimi napata mashaka, miaka waliyokuwa wanahesabu cyo hii tunayohesabu sisi.

Hivi kuna umbali gani kutoka misri (cairo) kwenda israel (yerusalemu)?

====

Yericko Nyerere
Huwa nasoma maandiko yote yaliyombele yangu, yawe ya wasomi na wanamajumui ama ya wajinga na yakijinga, mimi husoma tu. Hii imenipa uwezo na ujasiri wakuyajua mambo mengi yaliyohifadhiwa kwa maandishi,

Lakini kuna jambo hakika kwa miaka mingi nimekuwa nikiumiza akili yangu bila kupata jibu, nimejaribu kuzama kiroho imeshindikana, nimejaribu kuzama kihistoria imeshindikana,

Umbali kati ya Misri na Israel ni km 613, kwamjibu wa Biblia inasema wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40, inamana kila siku walisafiri mita 43?

Mafanikio ya binadamu duniani hutazamiwa afikapo miaka 18-40. Inaelezwa kwamba huo ndio mwenendo pia wa mafanikio ya taifa.

Wanamajumui wanasema ukizidi umri huo wewe uwe unatafuta hela ya kula tu, utajiri na hekima utavisikia tu

Wachungaji naomba msaada wa ufunuo hapa hapa.
img-20160920-wa0176-jpg.403864
 
Ni kama Tanzania tu mwaka wa 50 bado hatujaweza kujivunia utaifa wetu siku tukipata ukombozi wa kweli kifikra na tukaweka kwenye historia wajukuu zetu kipindi hicho wataumiza vichwa sana ilikuwaje babu na bibi zetu wakaishi maisha ya ukoloni mambo leo miaka yote hiyo?
 
Ni kama Tanzania tu mwaka wa 50bado hatujaweza kujivunia utaifa wetu siku tukipata ukombozi wa kweli kifikra na tukaweka kwenye historia wajukuu zetu kipindi hicho wataumiza vichwa sana ilikuwaje babu na bibi zetu wakaishi maisha ya ukoloni mambo leo miaka yote hiyo?

Hahaa haah ahaa! Mkuu lyinga umenichekesha sana. We unadhani walikuwa wanafanya nini miaka yote hiyo njiani.

Eti kama kulikuwa na mama mjamzito, then akajifungua alikuwa na uwezekano wa kupata mjukuu akiwa safarini .emegine!
 
Last edited by a moderator:
Wangeweza kutumia siku 8 kuingia nchi hii. Lakini njia hii ilikuwa na maadui wengi na vikwazo vingi. Wangeweza kukata tamaa njiani.

Lakini Mungu akawazungusha toka bara sini kuuzuka mlima Sinai ambapo kulikuwa na maadui wachache na vikwazo vichache. Pia Mungu alitaka kukichuja kizazi kilichozoea ibada za miungu Misri awatakase ili nchi ya ahadi kiingie kizazi kipya.

Hata hivyo historia na urithi havipotei, walirejea ibada hizi za sanamu. Mungu akawapa waamuzi(soma the book of judges). Waliasi, wakapewa mtetezi kila mara. Kitaalam tunaita apostance circle(kuasi na kurejea kwa Mungu). Wabillah Tawfiiq.
 
Jaribu kuwaza, ni safari ya siku ngapi kutoka duniani kwenda mbinguni aliko Mungu; tangu mwanadamu alipozaliwa duniani ?

Kwani kuna safari ya kwenda mbinguni toka duniani.? Aaah, story za mbinguni zipo kiimani zaidi. Kwenda mbinguni lazima kufa kwanza.
 
Safari ya Wana wa Israel toka Misri hadi nchi ya ahadi walikua wanaongozwa na Mungu mwenyewe kupitia ishara ya wingu likisimama wanasimama hivyo hivyo hata likitembea nao wanatembea, Kizazi hiki kilimkufuru Mungu na adhabu aliyowapa ni wote kuangamia njiani hata Musa mwenyewe aliishia kuiona nchi ya ahadi ila hakufika wote waliotoka Misri waliishia jangwani.
 
Miaka 40 ya Waisrael kutoka Misri kwenda Kanaani waiona mingi mno kiasi cha kuwa na mashaka.

Ukimwasi MUNGU na kuigiza kama vile unamtumikia na yeye amekuchagua lazima akurudi kama baba amrudivyo mwanawe anayempenda.

Nitakupa mfano rahisi wa kibinadamu unaoujua au waweza kuutafuta na kuupata. Miaka Tanganyika iliyojitawala (pamoja na muda wa muungano) ni miaka 53 sasa. Huu ni muda mrefu kuliko safari ya wana wa Israel na vikwazo vyake.

Pima kiwango cha maendeleo na mafanikio yetu. Kufikia mwaka 1971 tulifanya makubwa mno ambayo tumeibomoa na sasa tunaanza upya. Tuliweza kutengeneza nguo zetu,viberiti vyetu,viatu vyetu.

Tukaviharibu.Tunashangaa hakuna ajira. Tunatamani kuvifufua wengine wanaona bora Mwingereza arid I( kama Waisrael walivyokumbuka nyama Misri)
Ni kanuni ya MUNGU Taifa lisipomtii litazunguka tu. Walipoisha kizazi cha kuasi kwa kuabudu Ndama na kujitukuza fahamu zikafunguliwa. Joshua akakiongoza kizazi kipya kuingia kanaani.
 
Tunasoma katika bibilia kuwa wana wa israel walichukua muda wa miaka 40 kufika nchi ya ahadi wakitokea utumwani misri. Hapa najiuliza sana. Miaka 40 kutoka hapo kairo kwenda yerusalemu? Mbona ni miaka mingi sana? Au walikuwa hawajui njia? Mimi napata mashaka, miaka waliyokuwa wanahesabu cyo hii tunayohesabu sisi.

Hivi kuna umbali gani kutoka misri (cairo) kwenda israel (yerusalemu)?


Ahahahaaaaa......i second you,..hapo ndio tujue hizi hadithi za mashariki ya kati ni abrakadabrah.
 
Back
Top Bottom