Kuna umbali gani kuzunguka uwanja wa mpira mkubwa mara moja?

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
218
469
Kuna umbali gani kuzunguka uwanja wa mpira mkubwa mara moja? Nlikua Sina pumzi kabisa lakini nmejitahidi ndani ya wiki Tatu nmeweza kuzunguka uwanja wa mpira wa miguu mkubwa zaidi ya mara 15 nataka nijue nakua nmekimbia km ngapi hapo... Mwenye ujuzi na hili anisaidie.
 
Inategemea kwanza hicho kiwanja ulichozunguka kimepimwa au ni hivi viwanja vya mtaani!
Viwanja ambavyo ni standandard mzingo wake ni m480
 
Mkuu ongeza round hadi zifike 30 hapo utakuwa umeiva kabisa.
 
Kuna umbali gani kuzunguka uwanja wa mpira mkubwa mara moja? Nlikua Sina pumzi kabisa lakini nmejitahidi ndani ya wiki Tatu nmeweza kuzunguka uwanja wa mpira wa miguu mkubwa zaidi ya mara 15 nataka nijue nakua nmekimbia km ngapi hapo... Mwenye ujuzi na hili anisaidie.
Kuuzunguka kivipi? Kukimbia kando ya pichi au ile sehemu wanakimbia riadha
 
Ukiuzunguka Uwanja wa Mpira uliopimwa kwa Standard ya Viwanja ni sawa na Mita 400 hivyo unahitajika kuzunguka Mara mbili na nusu ili iwe umezunguka km 1 hivyo Mara 15 maana yake ni Km 6
 
Inategemea kwanza hicho kiwanja ulichozunguka kimepimwa au ni hivi viwanja vya mtaani!
Viwanja ambavyo ni standandard mzingo wake ni m480
Huu uwanja ni mkubwa Sana una lile duara la riadha ndo nalitumia hilo kuzunguka
 
Uwanja wa mpira mkubwa uliopimwa ni mitaa 400. Kama umezunguka Mara 15 ni mita 6000 Sawa na km 6.thats correct answer
Huu uwanja ni mkubwa Sana kuliko viwanja vya kawaida maana ule ile duara ya riadha na ndo ninaitumia kuzunguka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom