Kuna ulinganifu wa karibu sana kati ya Vyama Tawala vya Siasa na Mafarisayo wa zamani katika nchi nyingi zinazoendelea kwa namna hii

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ukiangalia historia ya zamani katika kipindi ambacho Wayahudi walikuwa wakiishi chini ya sheria ya Musa, kulikuwa na kikundi cha Mafarisayo ambao walikuwa na namna ya usimamizi juu ya jumuiya ya Wayahudi, pamoja na Sheria ya Musa. Hivyo sheria ya Musa ilikuwa ndio katiba ya taifa la Wayahudi.

Walichofanya Mafarisayo kwanza ni kujiona kuwa wao wako juu ya Sheria ya Musa na kuwadharau wanachi wa kawaida, pili waiitumia vibaya na hata kuhukumu watu kifo na adhabu nyingine kwa kuitumia sheria ya Musa vibaya, na tatu waliongeza mambo mengi kwenye sheria ya Musa ambayo yalikuwa ya kwao wenyewe.

Ndio maana baadhi ya manabii waliwaita Mafarisayo wanafiki, waliofanana na makaburi yaliyopakwa chokaa yakapendeza kwa nje kumbe ndani yamejaa uchafu. Na kwa ukosoaji huu wa wazi, Mafarisayo wakawaua manabii wengi hata kuwafungulia kesi za kubambikiza.

Njoo karne yetu hii katika nchi zinazoendelea. Utaona kwamba katika nchi nyingi zinazoendelea kuna ulinganifu wa karibu sana wa viongozi wa vyama vya siasa vinavyotawala na Mafarisayo wa zamani. Unakuta Katiba za nchi zipo, lakini viongozi wa siasa wa vyama tawala wanaamua kuongeza sheria zao zaidi ya zile zilizoainishwa kikatiba, na hata kufunga au kuua watu kwa kutumia sheria hizo za ziada - kama tu Mafarisayo walivyofanya. NI kama kunakuwa na sheria zilizopo kikatiba, na sheria za ziada kwa mujibu wa viongozi wa chama tawala - kama tu Mafarisayo walivyofanya!

Pia kunakuwa na kiburi cha kuona wananchi wa kawaida hawana lolote la maana katika kuchangia mawazo juu ya nchi yao - kama tu Mafarisayo walivyodharau watu wa kawaida. Na mbali zaidi, pale ambapo watu wanajitokeza na kukosoa viongozi wa vyama tawala juu ya mambo fulani fulani kuhusu uongozi wa nchi yao wanajikuta wakifungwa au hata kuuwawa - kama vile tu Mafarisayo walivyofanya!

Hitimisho nililofikia ni kwamba, katika nchi nyingi zinazoendelea, hakuna tofauti kati ya Mafarisayo wa zamani na viongozi wa vyama vya kisiasa vinavyotawala!
 
Watu kama kina Gwijama waliotaka kuingia kwenye siasa ningependa sana wauone huu uzi
 
Back
Top Bottom