Kuna ulazima wa kujionesha na designer products... fikiria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ulazima wa kujionesha na designer products... fikiria

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tausi Mzalendo, Feb 28, 2011.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna kamtindo ka watu kupenda kujionyesha kwa kuvaa labels - ati Gucci, Prada, Versace,dolce & Gabana etc..etc....tabia hii inanifurahishaga sana maana sijaelewa sana hii obsession inatokana na nini au tafsir yake ni nini.

  Je, ni kutaka kuonyesha kuwa kiwango cha umaskini katika ngazi ya kaya kimepungua ?

  Mtanzania hata kama unaishi nje ya nchi huhitaji sana kujifananisha na masupastaa wa Hollywood wanaolengwa na hao designers.Kumbuka Tommy Hilfiger wakati fulani aliwahi hata kutukana na kukashifu watu weusi akisema kuwa products zake hajatengeneza kuwalenga!

  Someni hii:
  "in a taping of the Oprah Winfrey show in Chicago where her guest was Tommy Hilfiger. On the show, sheasked him if the statements about race he was accused of saying were true. Statements like"..."If I'd known African-Americans,
  Hispanics, Jewish and Asians would buy my clothes, I WOULD NOT have made them so nice. I wish these people would *NOT* buy my clothes, as they are made for upper class white people. "His answer to Oprah was a simple "YES". Where after she immediately asked him to leave her show".
  ( iliwahi kupingwa kuwa ni propaganda lakini hata kama ndivyo, bado inatuonyesha kuwa walengwa wa hawa designers ni akina nani!)

  Pia ukiangalia wanaolilia sana kujitafutia kuonekana ni wale ambao siyo kiviiiileeee! Watu wenye uchache wao wanaangalia utility zaidi na uzuri wa product na siyo ati jina!
  Kama ni jina wachina mbona wameweza kuiga products hizo tena wakazipatia na hata bei zake siyo kiviiileee.

  Jiulize, unapong'ang'ania kuonekana umevaa Miu Miu au Louis Vuitton - je ni authentic? Original kwa mtanzania wa kawaida utakuwa ama ni Fisadi au uko na walakini kununua! Kama ni imitation - je inastahili wewe utupe pesa yako kuwanufaisha designers?

  Binafsi sidhani tumefikia kiwango hicho cha kuishi kikubwa ( living large) katikati ya maskini wa kutupwa.

  Ninaomba mawazo yenu.

  ANGALIZO:
  Mjadala huu ni strictly kwa wenye kuweza kuchambua na kuweka mawazo objective na siyo wenye kutaka kutetea vionjo vyao ambavyo si kwa maslahi ya watanzania wengi walio maskini.Ukijiona uko kwenye ile bracket ya wenye kuishi KIKUBWA basi tupishe sisi wengine wasiokuwa na uwezo wa kula milo mitatu kwa siku.

  HAPA PATAKUWA HAPAKUFAI TAFUTA JUKWAA LINGINE.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Umenifanya nifikirie sana; hapa Marekani watu weusi wanadaiwa kuwa wanaongoza kwa manunuzi ya matanuzi hasa viatu kama Nike, n.k n.k na hata ikija kwenyte magari utaona mtu lazima ajitahidi kutoka na cadillac n.k Lakini pia nimewahi kukutana na baadhi ya wabongo ambao wakikuona umeenda Walmart (duka kubwa zaidi la reja reja la US) wanakushangaa kwa sbabu linauza vitu vya bei ya chini; wao watataka waonekane wameenda Macy's au maduka mengine ya bei za juu.

  Wakati huo huo ili kuwa na vitu vya designer utaona hata kwenye maofisi na majumba yetu tuko tayari kununua vitu vya bei ya juu toka Uarabuni au Uchina wakati vitu kama hivyo vinapatikana TZ. Je vitu hivyo ni bora zaidi kuliko vya kwetu? Au ni kweli tunanunua kwa ajili ya majina?
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sorry kama nimekosea kuchangia hii mada nisamehe ila saa nyingine mtu unaangalia quality ya kitu mfano unaweza nunua kiatu cha bei ya kwaida tuu ukatumia kwa shule baada ya mwezi kimeharibika, na kama una uwezo kidogo kwann usinunue chenye unafuu ukatumia kwa miaka 2 au zaidi!!!
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
 5. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante Kang,,utaona hata mimi niliweka hiyo kwenye mabano maana niliskikia kuwa ilikuwa ni propaganda.Bado ishu inabakia palepale...kwanini watu wanajitia mashauzi wakati hawajafikia kiwango hicho?
   
 6. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ASANTE mKUU KWA KUONA POINT YANGU. Kwani ukinunua kitu Walmart na mwingine akaenda Macy's unapungukiwa nini mradi unatumia na kinakufaa? Tz kuna hili tatizo la kununua samani za bei mbaya kutika China badala ya kuhimiza utengenezaji wa bidhaa hizo kutokana na mbao zetu ambazo zitadumu.Kuna ishu ya ubora lakini hili lingeweza kushughulikiwa.


  Maria, wala hukupaswa kuomba samahani kabla ya kuchangia. Umeleta point y aubora.Kweli tunataka ubora lakini siyo kila mtu ananunua kiatu cha dola 300 kwa sababu ya ubora.Wengine wananunua JINA hata kama ni imitation. Nimeona shosti wangu mmoja kanunua bag $100 kisa ni LV hakukaa nayo hata, mara mkanda ulichomoka!BTW ingekuwa ni authentic LV ingeenda hadi $400, 600 NA SIYO 100!
  Kama ni kiatu cha shule, mtanzania kweli unaweza kulenga designer shoe? Acha maskhara Maria!
   
 7. Y

  YE JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu kila mtu ana uhuru wa kutumia kipato chake atakavyo. Kama wewe unaona sio ndio, waachie wanaopenda mashauzi waendelee. Uwezi kumfanya mtu anunue kuatu cha bora wakati anataka Nike....
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Vizuri sana japo nadhani wewe ni mmoja wa wale niliowahisi litawauma hadi wasiione point ninayotaka kuiibua.

  Umesikika lakini.Next!
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tausi,
  Umenikumbusha alichowahi kuandika Dr Onyeani Chika "The Capitalist Nigger". Kuna mtu alihitimisha vizuri..nami namnukuu;
  "After I read a book called capitalist nigger I started questioning myself as a black person and about black people in general.One striking statement that the author made was that white,chinese,indians and all the other races have made great contributions to improving the world except the black race.For starters the pc that I am using was designed and manufactured by a company owned and directed by a white person.Everything that I own was either manufactured in China or Japan and i am referring to things like my cellphone,tv,dvd player,the clothes I wear and everything else that I use in my life."

  Kwa kifupi hatupendi kuonekana tunatumia vile "ambavyo ni vyetu" au vile ambavyo "kila mtu" anatumia.Matokeo yake ni kudumaza uvumbuzi na ubunifu.
  "
   
Loading...