Kuna ulazima gani wa kuwa na Katiba ya nchi!?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,034
33,512
Kuna ulazima gani wa kuwa na Katiba ya nchi.

Kwani Nchi haiwezi kuongozwa bila ya kuwa na Katiba?

Katiba usipofuatwa kwa maslahi ya wananchi Katiba yenyewe inaweza kujitetea?

Mbona Uingereza haina Katiba "iliyoandikwa" na bado inaendeshwa vizuri zaidi kuliko baadhi ya nchi zenye Katiba zilizoandikwa?

Kwa nini kuwe na makelele kwamba Katiba imevunjwa. Kwani Katiba ikivunjwa nani anakosa mlo wake wa kila siku!?

SOMA KWA MAKINI!!
 
Katiba ndio muongozo, hiyo Katiba ya UK hata kama haijaandikwa lakini miongozo yake inapatikana kwenye kesi mbalimbali za huko kwao, na kwenye sheria zinazopitishwa na bunge lao.

Kwa muktadha huo, kila taifa lazima liwe na katiba yake na ifuatwe, taifa bila katiba ni sawa na wakristu pasipo biblia, au waislamu wasiwe na msahafu, hapo hapatakuwa na dini.

Ukiona mtu haifuati katibu huyo peleka maabara ukachunguze ubongo wake vizuri, atakuwa na tatizo.
 
Unazungumza hivyo mkuu kwasababu wewe hujawa Mhanga wa moja kwa moja wa matokeo ya uvunjwaji wa katiba. Ila ukimuuliza mtu kama T. Lissu au Ben Saanane Ndio utajua upi ni muhimu halisi wa kuwa na katiba mpya ambayo itafuatwa na kuheshimiwa na kila mtu
 
Uingereza wana Magna Carta tangu Karne ya 13 huko!! Ambayo haina tofauti sana na Katiba!

Wenzetu walishagundua mapema akili za binadamu dhidi ya ubinafsi na umungu mtu wao (Absolutism). Ila sisi ndiyo tunataka kwenda huko karne hii ya 21!! Inaguzunisha sana.
 
Soma basi uelewe nilichoandika!!
 
Nimekuelewa mkuu ila umetumia fumbo kama Yesu.Katiba ndiyo MOYO wa nchi ata Rais anaapa kuilinda kwa gharama yoyote.
Nchi bila katiba nisawa na mchungaji bila Biblia ama Imamu bila Kurani.

Katiba ndiyo mwongozo kwa watawala lakini ndio fungamano kati ya Watawaliwa na Watawala,haki zote tunazodai kama katiba haijazitambua basi hizo sio haki mfano:

Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Leo tunapinga sheria mpya ya "Makosa ya mtandaoni kifungu cha sheria 7 na 8 kinapingana na KATIBA ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu hiki kumtaka mtoa huduma za mtandao kutoa habari zake pale serikali itakapozihitaji
hii ilipelekea Mkurugenzi wa Jf kusimama na Katiba sio sheria vinginevyo nyote mngesombwa.

Najaribu kukusaidia ili uone umuhimu wa Katiba ya Nchi. Kwahiyo kitendo cha Rais kuvunja katiba ya nchi si tu kwamba kavunja katiba bali anakosa uharali wa kuendelea kutetea Katiba aliyoapa kuilinda kwamaana nyingine wananchi tunapaswa kuitetea katiba kwa kumwondoa MADARAKANI.

Mpaka sasa tunadai Uhuru wa kutoa na kupata Habari kwa mujibu wa katiba aliyoapa kuilinda ila yeye akatuletea sheria kutuondolea haki iyo.

Haki hii niyakikatiba na inaweza kuingiza nchi kwenye machafuko asiposikiliza sauti zetu.
 
Kuna ulazima wa kufuata KATIBA kama kwa wakati husika iko kinyume cha maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla!!??
 
Kuna ulazima wa kufuata KATIBA kama kwa wakati husika iko kinyume cha maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla!!??
Kwanini uvunje Katiba wakati baraza la mawaziri nilakwako na Bunge nilachama kimoja? Kwanini uselekeze waziri mwenye dhamana apeleke mswada Bungeni warekebishe unakoona panakukwaza? Maswali yako niya msingi ila yamekaa kikada jiandae kupokea haki yako.
 
Unazungumza hivyo mkuu kwasababu wewe hujawa Mhanga wa moja kwa moja wa matokeo ya uvunjwaji wa katiba. Ila ukimuuliza mtu kama T. Lissu au Ben Saanane Ndio utajua upi ni muhimu halisi wa kuwa na katiba mpya ambayo itafuatwa na kuheshimiwa na kila mtu
Ebu msome mleta uzi utamuelewa vizuri sana
 
Uingereza wana Magna Carta tangu Karne ya 13 huko!! Ambayo haina tofauti sana na Katiba!

Wenzetu walishagundua mapema akili za binadamu dhidi ya ubinafsi na umungu mtu wao (Absolutism). Ila sisi ndiyo tunataka kwenda huko karne hii ya 21!! Inaguzunisha sana.
Mkuu sasa tutafanyaje wakati dereva wetu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho na hataki mawazo ya utingo wala kondakta?
 
Kwanini uvunje Katiba wakati baraza la mawaziri nilakwako na Bunge nilachama kimoja? Kwanini uselekeze waziri mwenye dhamana apeleke mswada Bungeni warekebishe unakoona panakukwaza? Maswali yako niya msingi ila yamekaa kikada jiandae kupokea haki yako.
Nadhani hunamuelewa vema mleta uzi, jitahidi kuisumbua akili utamuelewa sana na uta muunga mkono
 
Umeshasema kuwa UINGEREZA ina katiba lakini haijaandikwa. Pamoja na kwamba wana katiba isiyoandikwa ni dhahiri kwamba wana miiko ya pamoja inayowaongoza raia wote.

Nafikiri hujui kuhusu "NON WRITTEN CONSTITUTION." Isome katiba hiyo inayoitwa katiba ya UINGEREZA
 
Katiba ni nini tuanzie hapo kwanza? Hivi ile kauli ya kwamba malkia haitajiki kuwa na leseni ya udereva ni sheria au ni story za kijiweni? Nakama ni sheria basi siipo ndani ya katiba au mie ndio natatizo la kuelewa tofauti ya katiba na sheria?
 
Back
Top Bottom