Kuna ulazima au umuhimu utaratibu huu kufuatwa?

rbsharia

Member
Sep 14, 2011
41
6
Hapa nchini kwetu kuna utaratibu unaotumika ambao ni usumbufu kwa wadau wa elimu hasa wanaoenda kusoma nchi za nje.
Mtanzania anapomaliza elimu katika nchi fulani kisha akarudi Bongo land kuna booooonge la usumbufu. Check hapo chini....

1. Aende TCU akathibitishwe.
2. Aende Wizara ya Elimu akapewe namba ya utambulisho.
3. Aende Wizara ya kazi akaandikishwe
4. Aende utumishi akasubmit copy ya vyeti vyake

Kisha itamlazimu aanze kuzunguuka huku na huko atafute kazi mwenyewe.

Kama sehemu zote hizo za serikali alizopita kuthibitishwa pamoja kukusanya nakala za vyeti vyake hazina msaada, Je kuna ulazima gani wa mlolongo wote huo kufuatwa?
 
Ni sahihi kabisa. Kuna baadhi ya vyuo vya nje Elimu yao haikidhi viwango vya Tanzania.
 
Mi naona kuna ka-usumbufu flani. Wangeunganisha 1 na 2. yaani ukishathibitishwa upewe namba ya utambulisho hapohapo. Kuhusu kwenda wizara ya kazi au utumishi, haipaswi kuwa lazima. kwani wanaomaliza kusoma vyuo vya hapahapa wanapelekaga vyeti vyao huko?
 
Mdoe mi nadhani mawazo yako yanaendana na mimi kwa sababu huo usumbufu ndio naona unacost kwa namna moja au nyingine.
Kwa mfano, mbali na kupita sehemu zote hizo, bado mtanzania huyu hapati msaada wowote kulingana na taaluma aliyoisomea.
Yaani ni usumbufu juu ya usumbufu.
THANKS.
 
Dushelele asante kwa maoni yako, tunachotaka ni kuijenga Tanzania inayojitambua na kutambulika popote Duniani.
 
Back
Top Bottom