Kuna ukweli wowote kuwa kabich hazina vitamini yoyote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna ukweli wowote kuwa kabich hazina vitamini yoyote?

Discussion in 'JF Doctor' started by G spanner, Mar 4, 2012.

 1. G spanner

  G spanner JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wataalam mtusaidie khs hilo!
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,110
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  yap kuna ukweli huo.
  kabichi ni roughage.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nasikia zinasaidia kwenye digestion
   
 4. B

  BILLY2TRY Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  cabbage - combats cancer,prevents constipation,promotes weight loss, protects your heart, helps hemorrhoids
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  KABICHI:Kinga kubwa dhidi ya saratani Cancer

  [​IMG]
  Ugonjwa wa saratani (cancer) ni miongoni mwa magonjwa hatari yanayosumbua watu duniani hivi sasa, Tanzania ikiwemo. Wagonjwa wanaongezeka kila kukicha katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambayo ni maalum kwa ugonjwa huu.Katika makala ya leo, tutajifunza faida za kabichi katika mapambano dhidi ya

  ugonjwa huo, licha ya kuchukuliwa kama ni mboga ya kimaskini na ambayo huliwa kwa shida zaidi kuliko kimanufaa ya kiafya.
  Ingawa inaonekana kuwa kabichi ni miongoni mwa mboga za majani zinazolimwa kwa wingi na kusambazwa kwenye masoko mengi nchini, hasa katika miji mikubwa, lakini ni watu wachache sana

  wanaopenda kula mboga hii.
  Katika miji mikubwa, kabichi inatumika zadi kwa walaji wa chips. Hata hivyo hawaitumia ipasavyo kwa sababu huwa inapikwa na kukaangwa kwa mafuta kwa muda mrefu na hivyo kupoteza baadhi ya virutubisho vyake muhimu.KINGA DHIDI YA SARATANIMiongoni mwa faida nyingi

  zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni ile ya kutoa kinga dhidi ya ugonjwa hatari wa saratani.
  Inaelezwa kuwa zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kuwa vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine kutibu.Kabichi

  imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee katika kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za virutubisho;
  ‘A‘Anti- ntioxidant inflammatory' na ‘Glucosinolates,, ' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa nyemelezi kadhaa ambayo husababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.Kwa

  kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuzia ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.
  AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO Mbali ya kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda

  vya tumbo
  (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao. Hali kadhalika mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara. HUIMARISHA MFUMO WA MOYO Utafiti mwingine uliofanyika kuhusu kabichi umeonesha kuwa mboga hii huimarisha mfumo mzima wa moyo kwa kudhibiti utengenezwaji wa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini ambayo inapozidi mwilini, husababisha matatizo ya moyo.VITAMINI ZINAZOPATIKANA KWENYE KABICHIN dani ya kabichi, kuna

  kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin, hususan Vitamin K, Vitamin B1, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.Ili kupata faida za kabichi na

  kujenga kinga imara dhidi ya magonjwa ya
  saratani, weka mazoea ya kula kabichi mara kwa mara, angalau mara tatu kwa wiki, kwa namna ambayo utaona mwenyewe inafaa, iwe kama mboga au kachumbari.
   
 6. G spanner

  G spanner JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Akhsante kwa somo mzizi mkavu.
   
 7. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 801
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Lakini roughage ni sehemu ya balance diet ambayo inasaidi to prevent constipation
   
 8. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 801
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  hapo ni sahihi mkuu.Kabichi uwa wanai-group kwnye kundi la "roughage" na kazi kuu za roughage ni mbili:-
  1.help us in digestion.
  2.prevent frm constipation.
  Nafikiri nipo sawa.
   
 9. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa wale waliokuwa wanasumbuliwa na High LDL na Triglyceride wanaweza kutumia Cabbage kama kachumbar ikiwa imewekwa Olive Oli kwa kupunguza High bad cholesterol.

  Kula kama kachumbar au raw vegetables na olive oil with lunch. Inasidia saaana.
   
Loading...