Kuna ukweli kwamba matajiri wakubwa SANA duniani wote ni members wa freemasons/illuminati?

Panda pine 600 tu pale Mufindi katika ekari moja utakayoinunua kwa Laki Tatu tu...panda miti yako kila mche shilingi 100×600=60,000 , Labour charge wapandaji 50,000 JUMLA KUU ya mtaji ni 410,000...Subiria hiyo miti baada ya miaka 10 tu kila mti utauuza shilingi 20,000×600=120,000,000/- Tzs hiyo 120,000,000 ni Mtaji wa kuanza safari ya utajiri, baada ya hapo na wewe mleta mada utakuwa freemason....Concept imetolewa FREE OF CHARGE.
 
Wwe hakuna mtu hata mmoja atakaesema kweli pesa zake amepata kwa njia ya kishirikina kila mtu atakwambia nimepata kwa juhudi na maarifa yangu ushetani ni uwovu mbele ya jamii Usikute wwe unaejinasibu utafutaji wako ni kujipanga kwako kumbe ndio wa kwanza kuchoma udi kila ufunguapo biashara yako Ukweli anaujua mungu acha kuzuga watu
 
Kwenye Biblia kuna andiko linalosema chapa ya kuzimu ya 666 itapigwa kwenye mkono na paji la uso,unavyosema sisi ndyo wateja wakubwa wa products zao,nina wasiwasi na hizi touchscreen smartphone,siyo kwamba unapo-touch kutumia fingerprint yako siyo ndiyo unaungwa kwenye kundi la kuzimu bila kujijua?
haiwezekani kuungwa bila kujijua harafu ikakuletea madhara kiroho kitakachokuletea madhara kiroho lazima ujiunge kwa kujua.
 
Mkuu kwa nini uhofie?Mpe Yesu maisha yako utaishi kwa amani.Mpokee yesu utafahamu mengi ambayo watu wasomi kama...(taja mwenyewe wale ambao hawaamini kuna Mungu hapa JF) yamefichwa kwao.
Concept iko hivi shetani anataka kukamata watu na kuleta mambo yake,nitaanza na viongozi wa nchi.
Raisi wa nchi ni kama mfalme kwa miaka ya zamani,kile kiti anachokalia si kiti cha kawaida hawezi akakaa mtu yeyote,kama ambavyo kuna baadhi ya magari ya wakuu fulani kama hayuko kwenye gari siti yake inakuwa wazi.
Kumbuka mkuu wa nchi akifanya maamuzi yanaathiri taifa zima kwa hiyo shetani anawahitaji sana watu wenye mamlaka na wanaofanya maamuzi au watu wenye ushawishi mkubwa(say wanamziki na watu maarufu).Akiwapata hao huwatumia kutimiza malengo yake.
Mfano kuna nchi nyingi tu ushoga ruksa matokeo yake watu wasiopenda tabia hizo wanaamua kujichukulia sheria mkononi,kama ni mfuatiliaji unajua issue iliyotokea kwenye night club moja Orlando Marekani.Ushoga ni kinyume na mapenzi ya Mungu lakini walioruhusu ni kina nani?hao wanaofanya maamuzi shetani anawahitaji sana ili awatumie,huu ni mfano mmoja wa mambo mengi itakuja siku zitapitishwa sheria hakuna kuhubiri habari njema kwa watu,kila mtu abaki na imani yake.
Matajiri ni wachache lakini wanacontrol maisha ya watu wengi kwa bidhaa wanazouza au huduma wanazotoa,wanaweza amua kama walivyoamua sukari ikakosekana na matokeo yake ikapanda bei huu ni mfano tu ya jinsi ambavyo hawa watu wanaweza athiri maisha yako.Shetani anawahitaji sana ili kufanikisha malengo yake kwa wanadamu,kwa mfano wanaotengeneza nguo,wakitengeneza vimini kibao au hijabu ambazo ni transparent hii imekaaje?Vipi nguo za heshima zikikosekana sokoni si unaweza ukakuta watu walio wengi wanavaa kinachopatikana?Kwani hizi fashioni za nguo inakuwa kama imechanika au nguo ina vitundu vitundu kibao na inaonyesha mwili wa mtu.Je mambo haya yalikuwepo enzi za mababu zetu?Kwa kifupi shetani anawahitaji sana matajiri wamsaidie,naongelea viongozi na matajiri wasiosimama katika mapenzi ya Mungu(Jehova).
Lakini kwa nini unahangaika na kundi dogo kisa ni viongozi ,wasanii au matajiri wakati devil worshipers ni wengi?Kama huenendi katika mapenzi ya Mungu na roho yako inakushuhudia,na unajijua matendo yako hayampi utukufu Mungu(in this case unampa utukufu shetani) wewe si ni mfuasi wa ibirisi?
Shetani ni super genius siyo simple kama unavyoweza mdhania,anaweza akakupa amani ya uongo anajua alipokukamata,kwenda kwako kanisani hakumwogopeshi,kutoa kwako sadaka hakumtishi kuna kiwango fulani cha imani ukiwa nacho anaogopa imani ile ambayo inaulizwa kwenye biblia "je Yesu akirudi ataikuta ile imani?"
Kuna nguvu fulani katika muziki,asiri ya muziki ilikuwa ni kutumika katika ibada za Mungu aliye hai,wanamziki wanaushawishi mkubwa,shetani alikuwa mtu wa mziki,ndiyo maana wanaohusika na mziki makanisani wasiposimama vizuri wengi huanguka dhambini kwa sababu shetani ana wivu kwani wamechukua kazi yake ya kumsifu Bwana.
Shetani anawatumia hawa watu(wanamziki) kwani wana ushawishi mkubwa kwa wafuasi wao,kuna nguvu fulani katika maneno unayotamka,sasa wewe usiyejua ukianza kuziimba nyimbo zao kwa kutamka maneno kuna vitu vinajengeka katika ulimwenge wa kiroho.
Labda nielezee kwa technique nyingine ili wale wasio amini kuna Mungu walau wapate kitu.
Shetani anashambulia nafsi zetu(our mind) kila muda,anaweka mawazo ndani yetu na kama haujui jinsi ya kumpinga matokeo yake unajikuta nafsi inautuma mwili kutekeleza mawazo yale.lakini nitumie lugha ngeni kidogon "our mind is very delicate,so be careful with whatever you feed your mind".Kile unacho soma au kusikiliza kinaathari nzuri au mbaya katika maisha yako.Chukua mfano wa watu waili mmoja anaangalia sana movie za mauaji au wizi au zile chuo walikuwa wanaziita "tutorial" na mwingine movie za mambo ya Mungu,hawa watu hawawezi kuwa sawa.Kile unachotazama,kusoma au kusikia kina athari hasi au chanya kwenye nafsi yako.Kuwa makini na vitu unavyosoma,sikiliza au kutazama,jiulize je vinamletea Bwana utukufu?
Chukua biblia soma 1Timotheo2:1-4 "Basi kabla ya mambo yote,nataka dua,na sala,na maombezi na shukurani,zifanyike kwa ajiri ya watu wote;kwa ajiri ya wafalme na wote wenye mamlaka,tuishi maisha ya utulivu na amani,katika utauwa wote na ustahivu.hili ni zuri nalo lakubalika mbele zaMungu Mwokozi wetu;ambaye hutaka watu wote waokolewe,na kupata kujua yaliyo kweli.

Soma vizuri andiko hilo utajua una wajibu wa kuwaombea watu wote ,viongozi na wenye mamlaka.Je umeikana nafsi yako?Kutamka namkataa shetani na mambo yake yote,wakati hujaikana nafsi yako hakumfanyi shetani akuache.Yesu alisema anayetaka kunifuata aikane nafsi yake,kisha ajitwishe msalaba wake anifuate.
nimeipenda hii asante kwa somo zuri
 
Mawazo haya ya freemasons ni product ya elimu dini ya utegemezi tupatayo mashuleni. Katika biblia twasoma watu matajiri kama: Ibrahim na Solomoni, je hao walikuwa ni mosons? Je Mungu aliwakabidhi wao kuhodhi mambo? Tujitahidini kutumia angalau 5% ya bongo zetu kujifunza jinsi ya kufanikiwa.
Rejea historia ya Freemasons, naona umemtaja Solomoni hapo!
 
FREEMASONS ni idea ya kijinga iliyotungwa na watu tu.

Ni story ya kusadikika kama ilivyo habari ya VAMPIRES na DRAGONS

Hakuna cha freemasons duniani.
 
True..... huwezi kuvuka anga flan hivi bila kua wao 90%
Mnaweza kuthibitisha haya madai yenu?
asilimia 80% ya manufactured product from west countries & europe wana izo logos za illuminati example carslogos ya mitusubishi, Bmw, na lexus ni product ambazo source yake iliianzia kuzimu, mbali na brand za vinywaj kama cocacola na vinginen ving tu
 
Hi members,

Nasikia kila kona kwamba matajiri wote wakubwa tunaowajua wapo chini ya mtandao wa Freemason/Illuminati. Wawe ni celebrities, wamiliki makampuni makubwa sana, au viongozi maarufu wa nchi mbalimbali duniani; wote naambiwa wamo mule..

Binafsi hii habari inanitisha sana na kunisikitisha nikiambiwa kwamba wamiliki wa makampuni kama Nike, Adidas, Sony, Apple, Airtel, Lg na mengine mengi sana nao ni devil worshippers coz mm binafsi cpendi hayo mambo ase!!

Mwenye taarifa kamili na uhakika kuhusu hili anisaidie.

Asanteni & Karibuni.
Kuna members ninaowajua mimi hapa TZ na wana maisha ya kawaida kabisa, sio matajiri, wanaishi maisha ya kawaida kabisa, by the way, temple zao hapa Dar pekee zipo nyingi msikariri ile ya pale town, kwa taarifa yenu, temple zingine zimo ndani ya mshule hayahaya ya ada kali watoto wetu huenda kusoma daily.
 
Hi members,

Nasikia kila kona kwamba matajiri wote wakubwa tunaowajua wapo chini ya mtandao wa Freemason/Illuminati. Wawe ni celebrities, wamiliki makampuni makubwa sana, au viongozi maarufu wa nchi mbalimbali duniani; wote naambiwa wamo mule..

Binafsi hii habari inanitisha sana na kunisikitisha nikiambiwa kwamba wamiliki wa makampuni kama Nike, Adidas, Sony, Apple, Airtel, Lg na mengine mengi sana nao ni devil worshippers coz mm binafsi cpendi hayo mambo ase!!

Mwenye taarifa kamili na uhakika kuhusu hili anisaidie.

Asanteni & Karibuni.

Hizi habari za freemason zinapatika saaana kwenye magazeti ya Shigongo,so nakushauri mtafute shigongo au mhariri wake wanaweza kuyajua mambo hayo.Humu sisi mnatuonea bure.
 
MASIKINI ndo hua tunasema na kuamini hivyo, kwa sababu ya wivu na pia kutotaka kuamini ukweli kuwa mwenzako amefight kwa nguvu na akili zake na kufanikiwa wakati wewe uko hivyo hivyo,

ni kama njia fulani hivi ya kujustfy umasikini wako
Kweli kabisa.
 
"Yani kama wewe nimfanyabiashara wa bidhaa na unahitaji kuuza internation na ili zikubalike na kusambaa ulimwenguni kote nilazima uwe na kibali cha hawa watu ambacho kikishawekwa kwenye bidhaa yako popote bale itauzika kutokana itaoekana ina hadhi, famous, na inayoenda na wakati example Hii label ya Tiffan unajua ni illuminati hata zile ishara za kwenye hii label zinaleta kauga kidogo"

You people you need to grow up kwakweli,dah!
 
Mawazo haya ya freemasons ni product ya elimu dini ya utegemezi tupatayo mashuleni. Katika biblia twasoma watu matajiri kama: Ibrahim na Solomoni, je hao walikuwa ni mosons? Je Mungu aliwakabidhi wao kuhodhi mambo? Tujitahidini kutumia angalau 5% ya bongo zetu kujifunza jinsi ya kufanikiwa.
Waafrika wengi wana ujinga wa imani za hovyohovyo.
 
asilimia 80% ya manufactured product from west countries & europe wana izo logos za illuminati example carslogos ya mitusubishi, Bmw, na lexus ni product ambazo source yake iliianzia kuzimu, mbali na brand za vinywaj kama cocacola na vinginen ving tu
omba mungu fanya kazi kwa maarifa na bidii...inamaana huko kuzimu kuna magari ya mistubish na lexus then yakaja dunia.
 
Mara nyingi watu masikini huwa wanawaza vitu vys ajabu...Naona ni kwajili ya kujifariji na umasikini wao
 
Back
Top Bottom