mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Lengo kuu lililo kwenye Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu, 2020 ni UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.
Suala la tafsiri sahihi na ya kiuhalisia ya maendeleo imezungumzwa sana. Hivyo, basi najikita kwenye Uhuru na Haki.
Kwenye Ilani hiyo ya CHADEMA, naamini msingi wa kuwa na lengo la Uhuru na Haki, ni kama lilivyoainishwa, nanukuu: Leo Tanzania inashuhudia, hususani katika Serikali ya Awamu ya Tano, vitendo vya watawala vinavyolenga kuwapunguzia wananchi “uwezo wao wa kuamua mambo yao wenyewe na
kutawala maisha yao wenyewe” na hivyo kujikuta wakilazimika kuwa sehemu ya vuguvugu la ukombozi awamu ya pili.
Kulingana na yaliyomo kwenye hiyo Ilani, na jinsi lengo hilo linavyositizwa kwenye kampeni za wagombea wao, hasa na mgombea Urais, ni wazi ukombozi awamu ya pili, siyo ukombozi wa kiuchumi. Swali, je Tanzania bado watu wake hawako huru na hawana haki? Huyu Mtanzania anakombolewa kutoka kwa nani na nani anamnyima uhuru na haki?
Ili kujibu swali la msingi la kama ni kweli Tanzania hakuna Uhuru na Haki, ni vyema kurejea kwenye Katiba ya JMT (1977). Uhuru na Haki vimeanishwa kwenye Sehemu ya Tatu ya Katiba: HAKI NA WAJIBU MUHIMU. Sehemu hii ya Katiba ina Ibara nyingi tu kuhusu:
√ Haki ya Usawa;
√ Haki ya Kuishi;
√ Haki ya Uhuru wa Mawazo;
√ Haki ya Kufanya Kazi; na
√ Masharti ya Jumla.
Kwa muktadha huo, je, ni sahihi kudai kuwa Watanzania wanahitaji ukombozi mwingine wa kudai Uhuru na Haki, au nyuma ya pazia kuna agenda zilizofichwa? Labda ni kwa sababu Rais Magufuli alipoingia madarakani alipiga marufuku siasa za majukwaani ili nguvu za Watanzania zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo?
Jibu lolote katika maswali hayo inabidi lizingatie mahitaji ya Katiba, Ibara ya 29(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanuliwa katika
ibara ya 12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hii ya Katiba;
na
Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Yawezekana Ibara hizo zina mapungufu km kuminya uhuru na haki ya watu wanaotaka Uhuru usio na mipaka au Haki bila kuwajibika. Ama sivyo CHADEMA wanaimba ngonjera isiyoeleweka kwani, hata kikifanikiwa kuwa chama tawala, hakitapenda hali ya uhuru na haki katika misingi wanayodai.
Kamwe mtu maskini hatajisikia huru na haki zake mara nyingi zitabanwa na walio nacho (matajiri). Sauti ya maskini dunia kote haiwezi kusikika. Hivyo kwa sasa tunahitaji ukombozi wa kiuchumi ili kila Mtanzania aone fahari ya kuishi katika nchi hii. Ndipo hapo tu sauti ya kila Mtanzania itasikika na si vingenevyo.